Elimu ya chuo kikuu ni kupoteza muda

Elimu ya chuo kikuu ni kupoteza muda

Mmmmmh! Swala la elimu bwana ni zito haswa mm nadhani huwa tunalalamika sana kuhusu Mitaji sijui serikali lakini elimu ni changamoto kubwa mno. Na mbaya zaidi elimu yenye maana zaidi wanufunzi huiona kuwa ni mahali pa mapito yaani nikufahulu mitahani na kutembea. Kumbe elimu ya chuo sometimes ni mzigo coz unasomea kazi ambayo bongo mambo hayo hayapo. Hafu kuyaanzisha ni ngumu kwasababu tumecopy na kupaste elimu ya kazi ko tunatembea nyuma ya waliotangulia then tunakua na hopes ambazo tangu uhuru na sio tz tu Bali ni Africa nzima. Mm naona nikupata basics then unajiaribu kumove forward. Yaani tz unakuta watu wanahangaika na matech wanasema fund hakuna nakati vitu vidogo ambavyo vipo kwenye elimu ya chini havifanyiki.
 
Inategemea na alichokisomea.. Kama alienda chuoni ilimradi tuu nayeye apate MKOPO basi matokeo yake ndio hayo.

Ila kama alienda haswaa kusomea anachokitaka/anachokipenda basi hawezi thubutu kusema hivyo!
Tuwe wakweli kweli kwa awamu hii mtu unaweza kwenda chuo eti kwa kitu unachokipenda? Labda kwa watoto wa kishua lakini kwa mtoto wa masikini, ki ukweli awamu hii imefanya hata wenye elimu ya chuo kikuu waonekane ndaza tu!! Mtu ana vyeti vyake vya u Daktari, vya uinjinia, bado anakula kwa kengere nyumbani?? Na tusidanganyane elimu yetu kumwambia mtu akajiajiri ni maneno ya ki siasa tu!!! Kama ni kusoma sawa, lakini kama huwezi kukabiliana na changamoto za maisha bado elimu haijakusaidia(hujaelimika)
 
1599257274458.png
 
Kama huna connection kweli utaona ni ya kipumbavu lakini pia kama huna akili za kujiongeza utaona ya kipumbavu
 
Kama huna connection kweli utaona ni ya kipumbavu lakini pia kama huna akili za kujiongeza utaona ya kipumbavu
utajiongeza vp mkuu Kama unafundishwa ku design machine hafu hakuna metals manufacture hata mmoja nchini kwako
 
"Kusoma elimu ya chuo kikuu ni upuuzi sana, ni kupoteza muda kijinga"

Nimenukuu jamaa akisema hayo maneno hapa Stationary nikiwa natoa copy sijui kwanini kaongea vile.


Hakuna ajira kwa wahitimu.
 
Swala ni kama ukiamua kuuza vitumbua au makande baada ya kuhitimu, utaifanya biashara kwa ufanisi
watu wana shahada zao ambao wameaanza kuuza chakula, matunda angalia hapo chini, usifikirie kuajiriwa tu




 
Back
Top Bottom