Elimu ya Bure ya Lowassa ni Kiini Macho

Elimu ya Bure ya Lowassa ni Kiini Macho

martyr2012

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2012
Posts
603
Reaction score
245
Ndugu wana JF leo gazeti la Nipashe limetoa mchanganuo wa gharama za Elimu ambazo Lowassa anasema anaweza kuzikabili na hatimaye watanzania wakasoma bure hadi chuo kikuu . Ingawa naipenda Ukawa lakini dosari hizi za wazi katika kuchanganua mambo hazipaswi ziachwe bila kutolewa tahadhari ili mgombea wetu wa Ukawa apate kuaminiwa kwa kile anachokisema.

Kiukweli upembuzi ule umeacha maswali mengi bila majibu huku nikihoji uwezo wa serikali ya Ukawa kutoa Elimu hiyo bure kwa ngazi zote za Elimu kuanzia chekechea. Gharama za Elimu ya juu pekee ni 6% ya budget ya 2014/2015. Na ukweli hizo ni fedha za kujikimu za wanafunzi 300,000 tu kwa mwanafunzi mmoja kupewa TZS 4.5m. Hapo hatujazingatia mishahara ya waalimu, tuition fees na vifaa vya kufundishia. Katika hali hii ni dhahira serikali itaelemewa na kutoa bora elimu kuliko elimu bora. Mzigo huo wa gharama ya elimu ukijumlishwa na shule za sekondari, msingi na chekechekea ni dhahiri elimu itachukua zaidi ya asilimia 20 ya budget ya nchi. Kama hii itakuwa hivyo ni dhahiri sekta nyingi muhimu zitaathirika na kupunguz a ufanisi wa serikali.

Tunahitaji majibu kutoka kwa ukawa kama kweli hii sera inaweza kutelezeka na kwa namna gani. Tusifanye masihara na hili. Lakini lazima watueleze kuhusu Tertiary Education nayo itakuwa buree au vipi?
 
wewe ndio kiini macho. kama twiga anapanda ndege elimu bure itashindikaneje? kama milioni kumi ni hela ya mboga titashindwaje? kama mtu anachangia harusi milioni mia nne tutashindwaje? kama watu wanabeba fedha kwenye vyandarua na mabox tutashindwaje? badilika weewe.
 
Elimu ya bure ya lowassa inawezekana sana tena sana...nyerere aliwezaje bila tanzinite gesi etc...muulize mtu wa zamani hadi nauli za kurudi makwenu zilikuwa zinapewa mashuleni
 
Hii issue ya elimu bure kwa vyuo vikuu ni dhana ya wajerumani na lengo lao ni kivutia wasomi kitoka nje ambao wanaleta fedha za kogeni.

UKAWA wanacopy na kupaste tu bila analysis!

Elimu bure afya bure huku ukitegemea wahisani ni upuuzi na sio mabadiliko.
 
Elimu bure inawezekana sana kama kutakuwa na dhamira ya kweli. kama mbunge analipwa mafao ya milioni 200 baada ya miaka mitano. kama mawaziri wanalipwa mamilioni kwa kuishi hotelini. nini kinachoshindikana?
 
martyr2012

Usijitoe ufahamu kwa kuruhusu ubongo wako kulala. Nyerere aliweza hilo unalosema haiwezekani tena bila kuuza madini yetu wala gesi yetu wala mafuta yetu pamoja na kusaidia uhuru wa nchi kibao za Africa. So ni mwendawazimu tu narudia ni mwendawazimu tu atasema Tanzania haiwezi kusomesha wananchi wake bure kwa rasilimali tulizonazo. Tatizo lako ni ubinafsi uliojaa moyo na kichwa chako na wanaokuzunguka ndio unakusumbua
 
Last edited by a moderator:

je zamani nyerere alikopi wapi sera ya elimu bure? haa haa je na ccm wamekopi wapi sera yao ya elimu bure mpaka kidato cha nne?
 
Home shopping centre wanakwepa sana kodi huku wakitoza gharama za juu sana kwenye usafirishaji! Hujaweka gesi na mianya kibao ya ukwepaji kodi! It's very easy to control it by the way!
 
Hivi unategemea majibu ya maana tola ukawa au toka kwa fisadi lowasa, Lowasa anadhani uraisi unachukuliwa tu kwa kudanganya wananchi.
martyr2012
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wana JF leo gazeti la Nipashe limetoa mchanganuo wa gharama za Elimu ambazo Lowassa anasema anaweza kuzikabili na hatimaye watanzania wakasoma bure hadi chuo kikuu . Ingawa naipenda Ukawa lakini dosari hizi za wazi katika kuchanganua mambo hazipaswi ziachwe bila kutolewa tahadhari ili mgombea wetu wa Ukawa apate kuaminiwa kwa kile anachokisema.

Kiukweli upembuzi ule umeacha maswali mengi bila majibu huku nikihoji uwezo wa serikali ya Ukawa kutoa Elimu hiyo bure kwa ngazi zote za Elimu kuanzia chekechea. Gharama za Elimu ya juu pekee ni 6% ya budget ya 2014/2015. Na ukweli hizo ni fedha za kujikimu za wanafunzi 300,000 tu kwa mwanafunzi mmoja kupewa TZS 4.5m. Hapo hatujazingatia mishahara ya waalimu, tuition fees na vifaa vya kufundishia.

Katika hali hii ni dhahira serikali itaelemewa na kutoa bora elimu kuliko elimu bora. Mzigo huo wa gharama ya elimu ukijumlishwa na shule za sekondari, msingi na chekechekea ni dhahiri elimu itachukua zaidi ya asilimia 20 ya budget ya nchi. Kama hii itakuwa hivyo ni dhahiri sekta nyingi muhimu zitaathirika na kupunguz a ufanisi wa serikali.

Tunahitaji majibu kutoka kwa ukawa kama kweli hii sera inaweza kutelezeka na kwa namna gani. Tusifanye masihara na hili. Lakini lazima watueleze kuhusu Tertiary Education nayo itakuwa buree au vipi?

Ni jambo gumu lakini jema kwa maana serekali ya ukawa itafanya kila njia zikiwemo njia za kuziba mianya yote ya matumizi mabaya na kukusanya kodi ili watekeleze hilo. Jambo hilo likifanikiwa itakuwa faida kubwa sana kwa watanzania si kwa watoto wetu kupata elimu tu bali litaongeza mzunguko wa fedha nchini na angalau afya za wa tz zitaimarika. Familia za tz sasa hivi hazili vizuri kwa kuwa kila wanachopata wanatumia kusomesha watoto.

Zamani biashara zilikua zinafanya vizuri kwa kuwa utamaduni wa kupeleka watoto shule au mwamko ulikua si mkubwa kama sasa. Kwa hivyo mabaa yalijaa maduka yaliuza sana nk nk. Wakifanikiwa kubeba hilo la elimu pekee ndio mwanzo mkubwa sana wa kuondoa umasikini kwa kuwa fedha za wa tz angalau zitaelekezwa kwenye mambo mengine ikiwa pamoja na makazi bora nk.
 
Usijitoe ufahamu kwa kuruhusu ubongo wako kulala. Nyerere aliweza hilo unalosema haiwezekani tena bila kuuza madini yetu wala gesi yetu wala mafuta yetu pamoja na kusaidia uhuru wa nchi kibao za Africa. So ni mwendawazimu tu narudia ni mwendawazimu tu atasema Tanzania haiwezi kusomesha wananchi wake bure kwa rasilimali tulizonazo. Tatizo lako ni ubinafsi uliojaa moyo na kichwa chako na wanaokuzunguka ndio unakusumbua

unajua tatizo la watu wengi hawaelewi maana halis ya mabadiliko tuyatakayo. mabadiliko tunayoyataka hayawezi kpatikana ccm kamwe. elimu bure inawezekana kama serikali itaamua kubana matumizi katika idara zake. hivo tukifuata mfumo wa katiba mpya tunaweza kabisa...
 
Elimu bure inawezekana sana kama kutakuwa na dhamira ya kweli. kama mbunge analipwa mafao ya milioni 200 baada ya miaka mitano. kama mawaziri wanalipwa mamilioni kwa kuishi hotelini. nini kinachoshindikana?
Kutoa elimu bure kwa mchanganuo usioleweka na usio na ukweli!... Kusanya pesa kwanza kabla ya kuzipangia!
 
Hii issue ya elimu bure kwa vyuo vikuu ni dhana ya wajerumani na lengo lao ni kivutia wasomi kitoka nje ambao wanaleta fedha za kogeni.

UKAWA wanacopy na kupaste tu bila analysis!

Elimu bure afya bure huku ukitegemea wahisani ni upuuzi na sio mabadiliko.

Sema amekopi kutoka serikali ya awamu ya kwanza ya mwalimu Nyerere. Na ni jambo linalowezekana kabisa. Na enzi za mwalimu Nyerere si tu elimu bali kulikuwa na huduma nyingine za bure. JKT watu walikuwa wanakula vizuri na kusafirishwa na serikali. Ni uamuzi tu.
 
Ndugu wana JF leo gazeti la Nipashe limetoa mchanganuo wa gharama za Elimu ambazo Lowassa anasema anaweza kuzikabili na hatimaye watanzania wakasoma bure hadi chuo kikuu . Ingawa naipenda Ukawa lakini dosari hizi za wazi katika kuchanganua mambo hazipaswi ziachwe bila kutolewa tahadhari ili mgombea wetu wa Ukawa apate kuaminiwa kwa kile anachokisema.

Kiukweli upembuzi ule umeacha maswali mengi bila majibu huku nikihoji uwezo wa serikali ya Ukawa kutoa Elimu hiyo bure kwa ngazi zote za Elimu kuanzia chekechea. Gharama za Elimu ya juu pekee ni 6% ya budget ya 2014/2015. Na ukweli hizo ni fedha za kujikimu za wanafunzi 300,000 tu kwa mwanafunzi mmoja kupewa TZS 4.5m. Hapo hatujazingatia mishahara ya waalimu, tuition fees na vifaa vya kufundishia. Katika hali hii ni dhahira serikali itaelemewa na kutoa bora elimu kuliko elimu bora. Mzigo huo wa gharama ya elimu ukijumlishwa na shule za sekondari, msingi na chekechekea ni dhahiri elimu itachukua zaidi ya asilimia 20 ya budget ya nchi. Kama hii itakuwa hivyo ni dhahiri sekta nyingi muhimu zitaathirika na kupunguz a ufanisi wa serikali.

Tunahitaji majibu kutoka kwa ukawa kama kweli hii sera inaweza kutelezeka na kwa namna gani. Tusifanye masihara na hili. Lakini lazima watueleze kuhusu Tertiary Education nayo itakuwa buree au vipi?

Mwanzoni umesema ninaipenda ukawa mwishoni naomba msaada toka kwa wana ukawa waje akusaidie DUH!!

"UKIWA MUONGO UWE NA KUMBUKUMBU"

martyr2012
 
Last edited by a moderator:
Kutoa elimu bure kwa mchanganuo usioleweka na usio na ukweli!... Kusanya pesa kwanza kabla ya kuzipangia!

Wacha kuishi maisha ya enzi za mawe! Inaonekana hata hujui ni nini maana ya bajeti na inavyopangwa
 
CCM wanajua kuna vijisenti,hela ya mboga,kubeba kwenye lumbesa,
 
sio rahisi kiivo unavoongea ndugu, nchi matajiri duniani na wenye mipango iliyoenda shule mara milioni 100 ya kilaza wa sanaa fisadi lowasa hawatoi elimu bure mpaka chuo kikuuu!!!!. Kwa hiyo hii inadhiirisha mgombea wa ukawa fisadi lowasa ni wa kuogopwa kama ukoma maana hana dhamira safi na maendeleo endelevu ya nchi yetu Tanzania

Home shopping centre wanakwepa sana kodi huku wakitoza gharama za juu sana kwenye usafirishaji! Hujaweka gesi na mianya kibao ya ukwepaji kodi! It's very easy to control it by the way!
 
Hivi unategemea majibu ya maana tola ukawa au toka kwa fisadi lowasa, Lowasa anadhani uraisi unachukuliwa tu kwa kudanganya wananchi.

haa haa hakuna chama kinachoongoza kudanganya wananchi wakati wa uchaguzi kama ccm. nitatoa mifano ifuatayo: mwaka 2005 rais kikwete aliwahaidi watanzania kwamba tanzania itakuwa ni nchi ya viwanda. je leo hali ikoje? pia ni rais kikwete aliyewahaidi watanzania maisha bora kwa kila mtanzania. je yako wapi? zaidi ya marafiki na ndugu kugawiwa vyeo kama njugu? mbaya zaidi maghufuli anahaidi mambo yaleyale. hakuna jipya zaidi ya ulaghai..
 
Back
Top Bottom