ELIMU YA AWALI: Serikali ni wakati sasa ihakikishe kila shule ya msingi inakuwa na darasa la awali

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,533
Kumekuwa na changamoto miongoni mwa baadhi ya vijana wadogo kuhitimu shule ya msingi wakiwa hawajui kusoma na kuandika...sasa mimi naishauri serikali iweke mkakati wa kuhakikisha kila Halmashauri inaweka mkazo kuhakikisha shule za msingi zote zinakuwa na darasa la awali na kuhakikisha walimu waliofuzu kufundisha watoto wadogo wanaajiriwa kufundisha madarasa hayo.

Tusipolitilia mkazo suala hili tutaendelea kutengeneza gap kubwa la kielimu kati ya wenye nacho na wasio nacho...maana wenye nacho watoto wao wanasoma shule za awali zenye viwango, hata viwango vya kimataifa....tunahitaji sana kuboresha elimu yetu ikiwa tunataka taifa lililoendelea.

Sambamba na hilo nashauri ule mpango wa MEMKWA uendelee...

REJEA/CASE STUDY/ Wanafunzi 10,273 shule za msingi hawajui kusoma | East Africa Television
ONGEZEKO LA UFAULU DARASA LA SABA LABEBA WASIOJUA KUSOMA, KUANDIKA | Gazeti la Jamhuri
Wanafunzi 107 Chalinze hawajui kusoma, kuandika - Tovuti ya habari za mikoa na wilaya zote Tanzania
Wasiojua kusoma na kuandika waongezeka
 
Back
Top Bottom