Elimu ya awali na UFUNDISHAJI unaozingatia syllabus ya Tanzania

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,075
1,864
NAMNA YA UFUNDISHAJI WA UJUZI WA KUSOMA KWA WATOTO KWA MJIBU WA SYLLABUS YA AWALI TANZANIA

Na mwalimu Lameck 0785663328

Elimu ya awali Tanzania, kwasasa inamwongozo mzuri Sana, tatizo limebaki kwa walimu wengi wa awali wasioujua mtaala na syllabus, hawa ndiyo wanadhani kufundisha chekechea ni KUJIBUNIA CHOCHOTE TU,😭😭 Hapana, elimu ya awali inawezekana ndiyo kuwa elimu ngumu kuliko hata elimu ya ADVANCE (FORM FIVE &SIX) haswa kwa mwalimu mfundishaji na mtoto mwenyewe, hii nikwasababu, mtoto huyu anakuwa haelewi chochote kile mwalimu anachofundisha. Hivyo, wizara kupitia taasisi ya elimu Tanzania, imepambana Sana kutafuta namna nzuri ya kutoa mwongozo wa namna nzuri ya kuwafanya watoto wa awali waelewe kwanini wanajifunza UMAHIRI FULANI.

Kwa shule za awali au daycare zinazozingatia mtaala wa elimu ya awali Tanzania , wanaelekezwa kufundisha MAHIRI SITA TU( Kwa mujibu wa mtaala wa awali Tanzania). MAHIRI ndiyo masomo kwa shule za awali, lakini sisi hatuiti masomo, ukikuta shule inaita masomo( SUBJECTS) kwa shule za awali/ daycares, ujue kuanzia mwalimu mpaka waanzilishi, hawatumii ama hawaujui mtaala wa elimu ya awali Tanzania. MAHIRI hizo sita ni pamoja na
1. KUHUSIANA/ RELATION
2. KUWASILIANA/ COMMUNICATION SKILLS
3. KUHESABU/ MATHEMATICAL SKILLS
4. KUTUNZA AFYA/ HEALTH CARE
5. KUTUNZA MAZINGIRA/ ENVIRONMENTAL CARE
6. SANAA/ ARTISTIC SKILLS

Ukiona kituo ama shule inafundisha masomo nje ya haya, hakika HUTOIKUTA NA SYLLABUS YA TANZANIA. Baada ya kuelimisha kuhusu mtaala, naomba nielekeze namna tunavyoelekezwa kufundisha watoto ujuzi wa kusoma, huu utaukuta kwenye UMAHIRI WA KUWASILIANA.

SYLLABUS inaelekeza kufundisha SAUTI ZA HERUFI 19 kwa shule zinazotumia kiswahili na herufi 26 kwa shule zinazotumia lugha ya kiingereza. Ipo hivi

Kwenye alphabets, Kuna herufi 26, lakini kwenye kiswahili, sauti c, q, x, hazipo.

Kwa kuwa tunapaswa kufundisha sauti za herufi, mwalimu anayejua kufundisha watoto, itabidi kabla hajafundisha sauti za herufi/ letter sounds, itabidi awaeleweshe watoto maana ya SAUTI. huu ni msamiati kwao, hivyo mwalimu hapaswi kukurupuka tu kufundisha sauti za herufi wakati mtoto hajua hata maana ya sauti, ndiyo maana syllabus ikaelekeza, mwalimu awafundishe watoto maana ya SAUTI/ SOUNDS kwa kuanza na
I. Sauti zitokanazo na MAZINGIRA. Mfano, viwanda au mashine hutoa sauti, mvua inyeshapo hutoa sauti au kukoroga maji hutoa sauti na sauti za wanyama mbalimbali
II. Sauti zitokanazo na vitu, mfano, ukiuzungusha ubao huvuma kwa kutoa sauti, ukigonga jembe au chuma, hutoa sauti
III. Sauti zitokanazo na ALA ZA MZIKI, Kama vile, gitaa, ngoma, vinubi, filimbi, vuvuzela, zeze, malimba, tarumbeta, radio, tv no
IV. Sauti zitokanazo na MIITIKIO YA MWILI. mfano, kupiga makofi, kutembea ,kusugua vidole no

Mwalimu akianza na kuelewesha maana ya SAUTI/ SOUNDS ndipo ataawaambia watoto kuwa, pia hata herufi hutoa sauti.

Syllabus inaelekeza kuanza kuchambua SAUTI ZA IRABU/ VOWELS ( a e i o u ) tena hizi sauti zinatakiwa ziwe kwa herufi ndogo, herufi kubwa Kama A, B, C ... siyo sauti, hayo ni majina ya herufi. Baada ya kufundisha sauti za irabu, mwalimu ataanza kufundisha sauti za consonants

Na utaratibu wa sauti wa herufi hubainika mwanzoni mwa herufi ya kwanza wa neno, mfano,

a - kwenye neno "andazi, acha, amka nk
e - embe, egemea nk
i - imba, igiza nk
O- oga, ogopa osha nk
U- ua, uza, unga nk

Ndivyo ilivyo hata kwenye lugha ya kiingereza

Hivyo hivyo Kama nilivyoonyesha kwenye irabu/ vowels hata konsonanti zinapaswa kufundishwa kwa huo mpangilio. Hapo mtoto ataelewa maana ya sauti/ SOUNDS

Mtoto akishajua maana ya sauti, ndipo hatua nyingine hufuata ya kuunda maneno na kusoma kutokana na sauti za herufi alizofundishwa.

Hapa tunaelekezwa kuanza na kwa kuunganisha sauti mbili kuunda silabi.
Mfano ( kwa lugha ya kiswahili)
b /buu/
a / aa/
Tunapata "ba"
Kwenye kiingereza
a/ aa/ & b / buu/ tunapata "ab"
Baada ya kufundisha kwa ufasaha silabi, ndipo mtoto hufundisha kuongeza sauti zaidi/ silabi na kupata neno, mfano
ba - ba= baba
ma - ma =mama
Kwenye kiingereza
C - at = cat
p- ot = pot

Mpaka unafikia hatua hiyo, maana yake watoto watakuwa katika viwango vizuri vya kujua sauti za herufi.

Ahaante kwa kufuatilia somo hili, ukiwa na maswali zaidi, karibu na jiunge na group letu la WhatsApp, huko utafundishwa kwa njia ya sauti.
Lipia tsh 1000 tu kupitia namba 0785663328
Jina HERMAN MANYILIZU
KARIBU SANA
 
Nikipata nafasi tena, nitakuja kueleza namna serikali na wizara ya elimu haswa kitengo Cha elimu ya awali kilivyoipotezea elimu ya awali katika shule za private, kiasi Cha watoto kufanya mitihani isiyokuwa level yao
 
Vizuri hizi zinaitwa phonetic based learning ni efficiency kuliko Ile tuliokuwa tunaimbishwa a for Apple bila kujua inamaanisha nin
Nahis shule za private angalau wanajitahidi ku adapt hii method,izi zetu bado Sana walimu wenyewe wa miaka ya 80 hawastaafu ,graduate wenye apdate skills wapo mitaani hawana ajira
 
Vizuri hizi zinaitwa phonetic based learning ni efficiency kuliko Ile tuliokuwa tunaimbishwa a for Apple bila kujua inamaanisha nin
Nahis shule za private angalau wanajitahidi ku adapt hii method,izi zetu bado Sana walimu wenyewe wa miaka ya 80 hawastaafu ,graduate wenye apdate skills wapo mitaani hawana ajira
Ahsante kwa kuliona hili
 
Back
Top Bottom