Elimu ya A-level ni kupoteza muda na malengo

Elimu ya A-level ni kupoteza muda na malengo

Elimu ya Tanzania inahitaji marekebisho.Kwanza choice sio nyingi.Kungekuwa na somo la Accounting,Economics,Psychology na masomo mengine,kuanzia ngazi ya chini,watu wangekuwa na choices nyingi,na pia ingetoa wasomi waliotukuka,ambao wanaweza kuajiriwa au kujiajiri,sio mtu anaenda kusoma Accounting and Finance,wakati hata excel hajawahi kufungua lol,halafu mnataka watu wajiajiri how?km hawana elimu ya kutosha?Elimu yetu iendane na dunia inavyobadilika,sio syllabus ya Enzi za mkoloni,sio lazima kusoma ma PCB,PCM,wastage of time.
 
inaweza kuwa kweli inategemeana na malengo yako,na changamoto unazokumbana nazo so kikubwa ni kujiandaa kiakili au kuwa na plan b.though kwel kitz ni shida kwa maana wote wenye ndoto kubwa tynategemea mkopo
 
Elimu ya Tanzania inahitaji marekebisho.Kwanza choice sio nyingi.Kungekuwa na somo la Accounting,Economics,Psychology na masomo mengine,kuanzia ngazi ya chini,watu wangekuwa na choices nyingi,na pia ingetoa wasomi waliotukuka,ambao wanaweza kuajiriwa au kujiajiri,sio mtu anaenda kusoma Accounting and Finance,wakati hata excel hajawahi kufungua lol,halafu mnataka watu wajiajiri how?km hawana elimu ya kutosha?Elimu yetu iendane na dunia inavyobadilika,sio syllabus ya Enzi za mkoloni,sio lazima kusoma ma PCB,PCM,wastage of time.
yap uko right kabisa huu umeshakuwa wimbo wa wa taifa kwamba watu wanaomaliza vyuo vikuu wajiajiri but sure Im telling you si kwa huu mfumo wetu mbovu wa enzi za elimu mtu kameza ma vitabu makubwa ya Chand ,Nelkon n.k halafu chuo anaenda kusomea kozi za biashara hapa tunazalisha mabomu .kwanza kuna asilimia wanamaliza Advance level hawapati nafasi ya kusomea vitu vinavyoendana na masomo waliyosoma advance na kingine ili kupata wasomi wenye uelewana ujuzi na wenye uwezo wa kuexploit fursa za kujiajiri tungekuwa na specialization tika ngazi za chini kabida kama elimu ya msingi kama nchi nyingine wanavyofanya na kuachana na kuproduce wasomi uchwara wasioweza hata kuandika proposal ya project zao ili kupata mikopo kwenye mabenki
 
Ukitizama hii elimu tuliyo letewa tayari ilikua ni li mzigo kwetu ilikua inatujenga kinadharia zaidi...na still tuna zidi kujiongezea mzigo zaidi unakuta mtu kasoma Advance Combination let's say Amesoma sayansi then anaenda kusoma Biashara chuo tena kapata chuo batch ya 4 apo na alicho omba sio alichopata ndo kuangukia biashara wengine wanasoma comb za biashara/sayansi wanaenda kusomea Utawala. Dah so sad
yap uko right kabisa huu umeshakuwa wimbo wa wa taifa kwamba watu wanaomaliza vyuo vikuu wajiajiri but sure Im telling you si kwa huu mfumo wetu mbovu wa enzi za elimu mtu kameza ma vitabu makubwa ya Chand ,Nelkon n.k halafu chuo anaenda kusomea kozi za biashara hapa tunazalisha mabomu .kwanza kuna asilimia wanamaliza Advance level hawapati nafasi ya kusomea vitu vinavyoendana na masomo waliyosoma advance na kingine ili kupata wasomi wenye uelewana ujuzi na wenye uwezo wa kuexploit fursa za kujiajiri tungekuwa na specialization tika ngazi za chini kabida kama elimu ya msingi kama nchi nyingine wanavyofanya na kuachana na kuproduce wasomi uchwara wasioweza hata kuandika proposal ya project zao ili kupata mikopo kwenye mabenki
Ningekua na Uwezo ningewashauri Madogo wanao piga vizuri O level waende Diploma tu wapitie uko mbele kwa mbele apo angalau kidogo uhakika wa Career Planning and Development ya Mwanafunzi inaweza ika fata mkondo kwa kiasi chake..
 
Wengi wanao support kutoenda advance ni wale waliofail form six wakashindwa kujiunga na chuo kikuu...Advance elimu yake ni for two years ukifaulu ndo unaenda chuo kikuu kuchukua degree,ila ukimaliza form four ukaenda diploma you will study for three years then ndo uende chuo kikuu,so wale tuliochemsha form six inabidi turudi kusoma diploma ili tusome degree so wanaona bora angeenda diploma moja kwa moja
 
Wakati mmoja anazingatia muda mwingine anazingatia fani.

Wa A'level atatumia muda mfupi hadi kusomea fani moja katika bachelor degree.

Lakini aliyepita diploma anaweza kusomea fani mbili tofauti katika level zote mbili (diploma na bachelor degree), anakuwa kwenye competition position nzuri zaidi kuliko yule mwenye fani moja.
Tofauti ya muda wa aliyepita A'level na diploma ni mwaka mmoja hadi kufika bach. degree

Na tofauti ya fani kwa aliyepita A'level na diploma ni moja pia hadi kufika bach. degree ikiwa mwenye diploma ataamua kubadili kozi.

Ila kila mtu apite njia ambayo anahisi itampa amani.
Wengi wanao support kutoenda advance ni wale waliofail form six wakashindwa kujiunga na chuo kikuu...Advance elimu yake ni for two years ukifaulu ndo unaenda chuo kikuu kuchukua degree,ila ukimaliza form four ukaenda diploma you will study for three years then ndo uende chuo kikuu,so wale tuliochemsha form six inabidi turudi kusoma diploma ili tusome degree so wanaona bora angeenda diploma moja kwa moja
 
Wengi wao wamebaki kusikitika na kujuta malengo yao yameyeyuka kama mshumaa.

Wapo waliotegemea kuja kuwa Madaktari, Injinia lakini wamejikuta wameangukia katika Ualimu na fani nyingine. Elimu ya bongo ni kukomoana tu mikopo shida, walimu wanadharaulika wanaitwa kila aina ya majina ya ajabu ajabu wanafikia hatua hadi ya kupigwa bakora mbele ya watoto. Inauma sana!

Mtoto wangu siwezi kumpeleka A-level ni bora akapige Diploma tu, elimu ya A-level ni pata potea kama kamari vile.
Pole sana.
Ikiwezekana mwanao aishie hata la saba tu elimu haina maana kabisa ni kupoteza muda na rasilimali tu!
 
Kwa uelewa wangu hatua za elimu zimepangwa kiufanisi zaidi kila hatua ipo kwa muendelezo wa hatua inayofuata.
Jiulize nini maana ya chekechea? Kwa nini darasa lisianzie la kwanza.
Kwa nini upoteze miaka saba ni nini hasa unapata ktk kipindi cha miaka 7 ya shule ya msingi. Ukweli hakuna profesional yeyote unayoipata ukimaliza miaka 7 ya shule ya msingi. Sasa kwa nini lzm udome?

Tuje secondary ambayo ni miaka 4. Sasa ukichukua mtu wa darasa la saba na aliye form 4 na kulinganisha. Wote hawa hawana taaluma lkn tofauti ipo na ipo ktk utayali.
Kwa mifano hii inaonyesha kutoka sehemu moja hadi nyingine pana umbali.
Na ili uhesabike kuwa umefanya umbali kadhaa itabidi tuhesabu hatua.
Na ili ufanye hatua inabidi uiandae.na unapokamilisha hatua inaleta mwendelezo wa hatua nyingine. Ukijumlisha unapata mwendo.

Ukiona hizo hatua sio muhimu hapo huna budi kuruka. Na mifano hai ipo wengi wameruka na wapo.

Na hitimisha kukuambia A level ni hatua kwa ajili ya kufanya hatua nyingine.
Umesomeka...
Elimu ya advance INA umuhimu wake mkubwa.
 
Mtoto wangu siwezi kumpeleka A-level ni bora akapige Diploma tu, elimu ya A-level ni pata potea kama kamari vile.
Kila ngazi ya elimu ina hiyo "pata-potea". Kuna vitu ambavyo ili vifanyike vinahitaji watu wenye elimu ya juu ya universities na kuipata hii njia kuu ni advance, degree, masters na phd kutegemea na mahitaji. Hivyo kimantiki kama nchi lazima iwe na mifumo ya kutoa elimu hizo au kupeleka vijana nje. Kuna shughuli ambazo diploma inatosha. Hivyo kila mmoja ana malengo yake na inabidi achague kinachomfaa kutokana na kile anachotaka. Kamari huwezi kuepuka labda kunatofauti ya kiwango cha kamari. Hata chuo wanadisco, masters wako wanaodisco na phd pia.
Ndio maana niliishia la saba nikaenda kuchimba madini, sasa hivi nimeajiri hao magraduate
Mkuu hapa naona umeteleza kimantiki. Wewe una uhitaji wa watu ambao ni graduates, wangefikiri kama wewe basi kazi zako zingekosa watu na zisingefanyika kwa weledi unaoutaka. Lakini pia ni wazi kuwa wengi wa darasa la saba ni dhoofu bin taabani (kitakwimu) ukilinganisha na graduates hata kama hii haimanishi kuwa darasa la saba hawafanikiwi. Mfano mzuri ni Luambo Makiadi Franco sidhani hata kama alimaliza darasa la nne baada ya kufiwa na baba yake lakini mafanikio yake ni makubwa sana, na wakina Diamond wanapita njia hiyo. Sasa huwezi ukawaangalia hao halafu useme elimu ni kupoteza muda.
 
Back
Top Bottom