Elimu sio Siasa, Nyuma ya pazia Sekondari ya Mt. Francis Mbeya

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,865
Mengi yameongelewa kuhusu ufaulu wa safari hii wa ST Francis secondary yaani nusu ya darasa kupata division one za point 7.Point saba kwa kidato cha nne ndio kiwango kikubwa cha ufaulu, Wengi walipambana kwa kusoma lakini hawakupata Point 7,Division one

Nini kilichofanyika tangu shule hii ianzishwe na ni mambo gani ambayo watu hawayajui kuhusu ST Francis Girls Secondary Mbeya ```:

Hii shule ni moja ya shule ilizoziua shule nyingi za Mbeya mjini mpaka maeneo ya Tukuyu huko, Shule kama Sangu, Meta na Iyunga Technical Secondary ndio wahanga wakubwa wa mikakati ya ST, Francis

Shule kama Iyunga Technical Secondary ndio imekufa kabisa na kushindwa kusimama tena pale Mbeya mjini sababu ya ST.Francis Secondary

Mosi, Walimu wa Iyunga secondary hasa wale wa Physics na Mathematics waliwajenga vijana kwenye shule hiyo ya serikali kila mtu aone rahisi na kupata "A " Huku msemo wa Single digit ukitawala kwenye shule hiyo miaka mingi mfululizo

Hao walimu hapo Iyunga wa Physics na Mathematics hawakuwa wengi kulikuwa na walimu 4 wa Mathematics na 3 wa Chemistry kwenye shule ya serikali yenye wanafunzi zaidi ya 800

Meta Secondary kulikuwa na Mwalimu wa Chemistry aliyejulikana kama Rand "nickname" huyu aliwafanya watu waone Chemistry ni somo la kawaida sana hapo Meta na Mbeya mjini

ST Francis wakati huo iliumia sana kutokana na Division one nyingi za Iyunga secondary kila mwaka, Wakati Iyunga ni shule ya serikali na haina mchujo kabisa, Waliohudhuria graduation za Iyunga tunakumbuka mengi wakati huo :

Hawa walimu wa Physics, Mathematics na Chemistry walipewa zawadi toka kwa mkuu wa shule, Kwa kila mtu mmoja aliyepata "A" walipewa shilingi 5000 kwa kila "A"hivyo watu waliomaliza mwaka uliopita wakipata A wengi basi unazidisha kwa 5000 ,kila mwalimu wa hayo masomo aliondoka na pesa kubwa kwa wakati huo

ST Francis waliamua kuingia negotiations na uongozi wa shule waweze kutengeneza ratiba ili hao walimu wafundishe part time ST francis toka Iyunga Secondary, Kumbuka hao walimu ndio walikuwa wakihubiri Single digit Yaani Division one kuanzia saba mpaka 9 basi hapo Iyunga Mbeya

Yule wa Chemistry meta secondary haikuwa shida sana kwani Meta ni private school hivyo alinaswa mapema sana

ST Francis ilianza kuwalipa hao walimu toka Iyunga pesa ndefu na kuwaahidi watoto wao kusoma bure au ndugu zao kila mwaka mtu au ndugu mmoja anasoma bure

Walimu hao walianza wao pamoja na familia zao kuona ST francis ndio maisha na maisha ni ST francis, Watoto wao walisoma hapo bure kama fadhila kwao na shukrani

ST Francis ikawajengea nyumba hao walimu maeneo tofauti tofauti Mbeya mjini bure kabisa kama shukrani na Fadhila, Wakajikuta wanahama kota za nyumba za Iyunga secondary na kwenda kwenye nyumba zao binafsi walizopewa toka ST Francis

Huu mkakati baada ya kukamilika wakafuata walimu wa masomo ya English na Kiswahili toka Iyunga secondary ambayo ni shule ya serikali

Mafaniko waliyoyapata kwenye masomo ya science ambayo walikuwa wanazidiwa na Iyunga secondary mkakati ulikuwa umekamilika sana baada ya kushuhudia utitiri wa "A" na Iyunga kuanza kuzitafuta kwa torch hawapati

Ili kuweka mambo sawa wakati huo, Headmaster wa Iyunga mwanae wa Kike akapata ofa ya kusoma hapo ST francis bure kabisa, Sasa huyo Headmaster ni mstaafu na mwanawe aliondoka na Single digit hapo St Francis

Uwekezaji na pesa imetumika sana kuijenga hii shule kwa gharama ya shule zingine, Leo hii shule nyingi zimebaki majina hapo Mbeya mjini walimu wazuri hasa watu wazima huchukuliwa na St Francis kwa kupewa mazingira mazuri kuanzia nyumba, mpaka magari

Siasa inayofanyika kwenye shule za serikali ni ngumu kubadilisha muelekeo kwa sasa

Serikali inatakiwa iweke siasa pembeni na iwekeze kwenye walimu wenye ufaulu mkubwa kwa kuwaandalia mishahara mizuri,

Mtu mwenye akili anahitaji mambo mengi, Yaliyotokea Iyunga, Yatatokea kwenye shule nyingi zaidi

Huu mkakati wa St Francis ulianza rasmi mwaka 1999 leo hii wao wanafikiria Single digit tu katika mitihani yao yaani Division one ya 7 mpaka 9 basi```

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanapiga sana kelele kwa tuliokulia kwenye kanisa la watoto la Roma pale mbeya na kushinda mitaa ya stereo tunaijua vizuri hii shule namna ilivyojijenga kwa jasho na damu..

Meta, Iyunga, Sangu, Loleza, Mbalizi sec, zimekutana na fimbo za St.Franciss kwa walimu wake..

Mpaka sasa ukienda kanisani jumapili misa zote unawakuta wale wanafunzi wamevaa uniform zao nadhifu, siti za mbele wanaimba kila nyimbo na kushiriki ibada, nidhamu ya hali ya juu, just imagine wewe ni mzazi mtoto wako anasoma pale unaenda kanisani unamuona yule haurusiwi hata kumpungia mkono,

Ukiachana na single digit, mtoto akitoka pale akirudi home anakuwa mtakatifu kwelikweli..

LAKINI KUNA TATIZO MOJA KUBWA ,WATOTO WANAOMALIZA PALE WAKIENDA A LEVEL ASILIMIA KUBWA WANAFELI MTIHANI WA TAIFA WA FORM SIX..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha mbali teacher Rand kanifundisha tuition hapo Meta huyu teacher hata kama huipendi chemistry atafanya uipende na kuielewa ni comedy sana harafu anjua mbinu za ufundishaji. Anatembelea gongo lakini anakwambia disco anaenda kama kama kawaida atakuonyesha mbwembwe za kucheza hapo mtabaki vicheko tu, kwa kifupi huwezi kudoji kipindi chake
 
Watu wanapiga sana kelele kwa tuliokulia kwenye kanisa la watoto la Roma pale mbeya na kushinda mitaa ya stereo tunaijua vizuri hii shule namna ilivyojijenga kwa jasho na damu..

Meta, Iyunga, Sangu, Loleza, Mbalizi sec, zimekutana na fimbo za St.Franciss kwa walimu wake..

Mpaka sasa ukienda kanisani jumapili misa zote unawakuta wale wanafunzi wamevaa uniform zao nadhifu, siti za mbele wanaimba kila nyimbo na kushiriki ibada, nidhamu ya hali ya juu, just imagine wewe ni mzazi mtoto wako anasoma pale unaenda kanisani unamuona yule haurusiwi hata kumpungia mkono,

Ukiachana na single digit, mtoto akitoka pale akirudi home anakuwa mtakatifu kwelikweli..

LAKINI KUNA TATIZO MOJA KUBWA ,WATOTO WANAOMALIZA PALE WAKIENDA A LEVEL ASILIMIA KUBWA WANAFELI MTIHANI WA TAIFA WA FORM SIX..

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila wengi wanachukuliwa na Marian Girls na Mazinde Juu sasa sijui hizi shule nilizotaja kwa A level matokeo yake ni vipi??? Ninamfahamu ni one of the girls best A level schools.
 
Mengi yameongelewa kuhusu ufaulu wa safari hii wa ST Francis secondary yaani nusu ya darasa kupata division one za point 7.Point saba kwa kidato cha nne ndio kiwango kikubwa cha ufaulu, Wengi walipambana kwa kusoma lakini hawakupata Point 7,Division one

Nini kilichofanyika tangu shule hii ianzishwe na ni mambo gani ambayo watu hawayajui kuhusu ST Francis Girls Secondary Mbeya ```:

Hii shule ni moja ya shule ilizoziua shule nyingi za Mbeya mjini mpaka maeneo ya Tukuyu huko, Shule kama Sangu, Meta na Iyunga Technical Secondary ndio wahanga wakubwa wa mikakati ya ST, Francis

Shule kama Iyunga Technical Secondary ndio imekufa kabisa na kushindwa kusimama tena pale Mbeya mjini sababu ya ST.Francis Secondary

Mosi, Walimu wa Iyunga secondary hasa wale wa Physics na Mathematics waliwajenga vijana kwenye shule hiyo ya serikali kila mtu aone rahisi na kupata "A " Huku msemo wa Single digit ukitawala kwenye shule hiyo miaka mingi mfululizo

Hao walimu hapo Iyunga wa Physics na Mathematics hawakuwa wengi kulikuwa na walimu 4 wa Mathematics na 3 wa Chemistry kwenye shule ya serikali yenye wanafunzi zaidi ya 800

Meta Secondary kulikuwa na Mwalimu wa Chemistry aliyejulikana kama Rand "nickname" huyu aliwafanya watu waone Chemistry ni somo la kawaida sana hapo Meta na Mbeya mjini

ST Francis wakati huo iliumia sana kutokana na Division one nyingi za Iyunga secondary kila mwaka, Wakati Iyunga ni shule ya serikali na haina mchujo kabisa, Waliohudhuria graduation za Iyunga tunakumbuka mengi wakati huo :

Hawa walimu wa Physics, Mathematics na Chemistry walipewa zawadi toka kwa mkuu wa shule, Kwa kila mtu mmoja aliyepata "A" walipewa shilingi 5000 kwa kila "A"hivyo watu waliomaliza mwaka uliopita wakipata A wengi basi unazidisha kwa 5000 ,kila mwalimu wa hayo masomo aliondoka na pesa kubwa kwa wakati huo

ST Francis waliamua kuingia negotiations na uongozi wa shule waweze kutengeneza ratiba ili hao walimu wafundishe part time ST francis toka Iyunga Secondary, Kumbuka hao walimu ndio walikuwa wakihubiri Single digit Yaani Division one kuanzia saba mpaka 9 basi hapo Iyunga Mbeya

Yule wa Chemistry meta secondary haikuwa shida sana kwani Meta ni private school hivyo alinaswa mapema sana

ST Francis ilianza kuwalipa hao walimu toka Iyunga pesa ndefu na kuwaahidi watoto wao kusoma bure au ndugu zao kila mwaka mtu au ndugu mmoja anasoma bure

Walimu hao walianza wao pamoja na familia zao kuona ST francis ndio maisha na maisha ni ST francis, Watoto wao walisoma hapo bure kama fadhila kwao na shukrani

ST Francis ikawajengea nyumba hao walimu maeneo tofauti tofauti Mbeya mjini bure kabisa kama shukrani na Fadhila, Wakajikuta wanahama kota za nyumba za Iyunga secondary na kwenda kwenye nyumba zao binafsi walizopewa toka ST Francis

Huu mkakati baada ya kukamilika wakafuata walimu wa masomo ya English na Kiswahili toka Iyunga secondary ambayo ni shule ya serikali

Mafaniko waliyoyapata kwenye masomo ya science ambayo walikuwa wanazidiwa na Iyunga secondary mkakati ulikuwa umekamilika sana baada ya kushuhudia utitiri wa "A" na Iyunga kuanza kuzitafuta kwa torch hawapati

Ili kuweka mambo sawa wakati huo, Headmaster wa Iyunga mwanae wa Kike akapata ofa ya kusoma hapo ST francis bure kabisa, Sasa huyo Headmaster ni mstaafu na mwanawe aliondoka na Single digit hapo St Francis

Uwekezaji na pesa imetumika sana kuijenga hii shule kwa gharama ya shule zingine, Leo hii shule nyingi zimebaki majina hapo Mbeya mjini walimu wazuri hasa watu wazima huchukuliwa na St Francis kwa kupewa mazingira mazuri kuanzia nyumba, mpaka magari

Siasa inayofanyika kwenye shule za serikali ni ngumu kubadilisha muelekeo kwa sasa

Serikali inatakiwa iweke siasa pembeni na iwekeze kwenye walimu wenye ufaulu mkubwa kwa kuwaandalia mishahara mizuri,

Mtu mwenye akili anahitaji mambo mengi, Yaliyotokea Iyunga, Yatatokea kwenye shule nyingi zaidi

Huu mkakati wa St Francis ulianza rasmi mwaka 1999 leo hii wao wanafikiria Single digit tu katika mitihani yao yaani Division one ya 7 mpaka 9 basi```

Sent using Jamii Forums mobile app
duuu,,,akina mimi ni wahanga,,nilipitia advance pale iyunga juzi kati tuu 2015-2017,,,ofcorz yaaa kuna siasa ndani yake zipo kuhusu walimu,,walimu wengi walikuwa wanapiga part time sana kwenye shule za Pandahili,St francs,Meta,Uwata,Sangu na vijishule vingne vingine vya private e.g kuna teacher flani hivi daa yule alikuwa anafundisha shule nne yaani uwata,pandahili,Sangu na iyunga but kaajiriwa pale Iyunga,,,THIS IS HOW IYUNGA inapoteana,,,,
 
Watu wanapiga sana kelele kwa tuliokulia kwenye kanisa la watoto la Roma pale mbeya na kushinda mitaa ya stereo tunaijua vizuri hii shule namna ilivyojijenga kwa jasho na damu..

Meta, Iyunga, Sangu, Loleza, Mbalizi sec, zimekutana na fimbo za St.Franciss kwa walimu wake..

Mpaka sasa ukienda kanisani jumapili misa zote unawakuta wale wanafunzi wamevaa uniform zao nadhifu, siti za mbele wanaimba kila nyimbo na kushiriki ibada, nidhamu ya hali ya juu, just imagine wewe ni mzazi mtoto wako anasoma pale unaenda kanisani unamuona yule haurusiwi hata kumpungia mkono,

Ukiachana na single digit, mtoto akitoka pale akirudi home anakuwa mtakatifu kwelikweli..

LAKINI KUNA TATIZO MOJA KUBWA ,WATOTO WANAOMALIZA PALE WAKIENDA A LEVEL ASILIMIA KUBWA WANAFELI MTIHANI WA TAIFA WA FORM SIX..

Sent using Jamii Forums mobile app
kwa nini wanafeli form six?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa nini wanafeli form six?

Sent using Jamii Forums mobile app
Form six walimu hawatoshelezi na waliopo ndio hivyo wanamambo mengi,,,e.g class letu pale iyunga tulikuwa madarasa mawili PCB&PCM,pcb ilikuwa na wanafunzi 186 na pcm ilikuwa na wanafunzi 150 hii ni form six tuu,na form five nao walikuwa katika idadi inayoendana sawa na sisi,,,hivyo basi kulikuwa kama na wanafunzi 700 wa adavance tuu (madarasa manne),,,shida inakuja kwenye ufundishaji sasa kulikuwa na walimu wawili wa Physics na walimu wawili wa Chemistry,biology walimu wawili na Mathe walikuwapo kama watatu na wa BAM,,,sasa mfano kwenye Physics hao walimu wawili wanatakiwa wafundishe madarasa ya form five na form six,,alafu ikumbukwe kuwa kuna Practicals kwa masomo haya yote and ukija kwenye theory za Physics ni ndefu balaaa mfano Electromagnetism na Mechanics,,,,hapa wale walimu wetu wawili ndio walikuwa vichwa vinapataa motooo hadi sio poa.
 
Wewe umedandia gari kwa mbele.

Huyu niliye mkwoti amedai wanafunzi wa ST FRANSIS huwa wanafeli sana mitihani ya kidato cha sita sasa nikamuuliza kwa nini wanafeli mitihani ya kidato cha sita? Sijauliza kuhusu hiyo Iyunga yenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera ST Francis. it pays to the future what you owe to the past.😅naamin Walimu hawa hawahusiki hata kusimamia chaguzi zile😅
 
Mtoa mada umenikumbusha mwaka 1999 ulipomtaja mwalimu " Rand" aliyekuwa akifundisha Chemistry Meta Sec School. Nilisoma tuition kwake nikiwa Mbeya Sec School na nikawa kichwa cha Chemistry darasani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom