Elimu peke yake sio ufunguo wa maisha

Elimu peke yake sio ufunguo wa maisha

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
65,015
Reaction score
111,416
Wakati nasoma shule ya msingi motto wetu ambao tulikuwa tukiusema kwa hisia kila siku asubuhi ulikuwa "elimu ni ufunguo wa maisha". Takribani miaka 20 tangu kipindi hiko maelfu ya waliokuwa wakisema motto huo ni maskini hoehae au watu wa kipato cha mlo wa siku tu pasipo kujua hatma ya kesho.

Ukweli ni kwamba elimu tu sio ufunguo wa maisha bali ikweka pamoja na NDOTO(kwa maana ya IMAGINATION), MAARIFA na UTHUBUTU ndio huwa ufunguo wa maisha. Bahata mbaya au nzuri sana hayo yote mara nyingi hupatikana nje ya kuta nne za madarasa.

Mabadiliko, utajiri na maendeleo yoyote makubwa yanakuja kupitia kuwa na ndoto kubwa, kuwa na uthubutu wa mambo na kutenda mambo kwa maarifa makubwa.Watu na mataifa makuu yametokana na mambo hayo, ukiona taifa au watu wake ni maskini ujue wanapungukiwa na hayo kwa kiasi kikubwa.
 
Nadhani watu wengi wamei narrow na kuielewa tofauti maana ya elimu inayozungumziwa hapo.

Mtu akisikia elimu anaifikiria hii formal education, ambayo hizo kuta nne za darasa zinahusika kwa kiwango kikubwa

Watu wakumbuke kuna informal na non formal education pia.

Ili utimize ndoto zako, upate maarifa na uthubutu ni muhimu uwe na taarifa sahihi kwa kile unachokiendea. Na katika kutafuta taarifa ndio kuelemika kwenyewe huko.

Hakika, elimu ni ufunguo wa maisha.
 
Back
Top Bottom