Elimu nchini ipo mahututi

Elimu nchini ipo mahututi

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,283
Dodoma/Dar.
Baadhi ya wabunge jana walichachamaa wakisema elimu nchini ipo mahututi na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuunda tume ya kudumu ya elimu itakayochunguza mfumo wa elimu nchini.

Wabunge hao walikuwa wakichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka wa fedha 2014/2015 iliyowasilishwa na waziri wake, Dk Shukuru Kawambwa Jumamosi usiku.

Mbunge wa Longido (CCM), Lekule Laizer alipendekeza safari zote za wabunge na mawaziri nje ya nchi zifutwe na fedha zake zipelekwe kuboresha shule za kata.

Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Mageuzi), James Mbatia alizungumzia uduni wa vitabu na mitihani ya wanafunzi wa shule za msingi akisema inakosewa kutungwa.

"Nina mtihani wa majaribio wa darasa la saba ambao haufanyiki. Niliwahi kumpa profesa mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye alitumia saa mbili na nusu bila kupata jibu lolote la kuandika. Mtihani wenyewe haufanyiki," alisema Mbatia na kutoa ofa ya Sh10 milioni kwa profesa mwingine yeyote bungeni ambaye ataweza kufanya mtihani huo na kupata alama 100.

"Haya ni madudu ya kutisha. Mwaka jana nilivyotoa maoni yangu hapa na waziri akasema maoni yetu yamechukuliwa, alisema rasimu ya mwisho sera ya elimu imepelekwa Baraza la Mawaziri Machi 2013, lakini hadi sasa bado haijakamilika," alisema na kuongeza kuwa hiyo ni dalili ya Bunge kutoheshimiwa.

Pia alizungumzia ripoti za kamati zilizoundwa kuchunguza elimu lakini hazikufanyiwa kazi na badala yake zikawekwa kwenye makabati.

"Tumwombe Rais aunde Tume ya Kudumu ya Elimu kwa sababu kwa hali inavyokwenda ni mbaya sana na napendekeza tume hii ishughulike na kudhibiti mambo yote yanayofanya kutetereka kwa ubora elimu nchini.

Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba alisema elimu ya Tanzania iko mahututi na kuwaomba wabunge kuacha siasa katika elimu.

"Bajeti itapita lakini tunaua kizazi kijacho. Mheshimiwa mwenyekiti nenda darasa la kwanza mpaka la saba anayoyasema Mbatia yapo hata kama hatuyapendi lazima tuseme ukweli," alisema.

Alisema ukienda katika vyuo vikuu ni majanga. "Kama unajiangalia wewe na familia yako, basi tunaliua Taifa. Nimefanya utafiti kwenye nchi 35, Tanzania ni nchi ya mwisho kwa ufaulu," alisema na kuongeza kuwa nchi zote zilizoendelea kiuchumi, kiwango cha ufaulu ni juu ya asilimia 60.

Mbunge wa Ngara (CCM), Deogratias Ntukamazina alisema hakuna Wizara ya Elimu baada ya elimu ya sekondari na msingi kuondolewa.

"Mbele ya Waziri Mkuu niseme kuwa sasa hatuna Wizara ya Elimu… na sasa wanaondoa elimu ya watu wazima, shule zote za mazoezi zimeondolewa."

Mbunge wa viti maalumu (CUF), Magdalena Sakaya alisema anashangazwa na wizara kushusha madaraja ya ufaulu ambayo awali, kuanzia alama 34 ilikuwa ni daraja O lakini leo ni ufaulu.

"Kiukweli waziri aliyeko katika wizara hii ameshindwa kusaidia elimu nchini. Tangu ameshika wadhifa huo anazidi kubebwa. Kwa nini tunambeba mtu ambaye ameshindwa kusaidia elimu nchini?" alihoji.

Safari za nje

Laizer alitaka safari za mawaziri na wabunge nje ya nchi zifutwe na fedha hizo ziboreshe shule za kata ambako ndiko watoto wa maskini wanakosoma.

Alisema anashindwa kuunga mkono bajeti ya wizara hiyo wakati watoto wake wote katika jimbo lake wanafeli kutokana na shule za kata kutokuwa na walimu wa kutosha.

Akifanya majumuisho, Waziri Kawambwa alikiri deni la Sh61 bilioni la madai ya walimu, lakini akasema serikali imekuwa ikilipa.

Alisema kuanzia Agosti mwaka jana hadi Machi, jumla ya Sh16 bilioni zimelipwa na kwamba si kweli kwamba deni hilo limebakia kuwa Sh61 bilioni.

Imeandikwa na Sharon Sauwa, Daniel Mjema (Dodoma) na Julius Mathias (Dar).

Chanzo:Mwananchi
 
Haya ndio matokeo ya Big Results Now (BRN), nchi inazidi kuangamia na wanaoingamiza wanafanya kila waliwezalo kung'an'gania kubaki madarakani pamoja na kuwepo ushahidi wa kutosha kwamba uongozi wa nchi umewashinda kabisa.
 
Yaani ni kama kukomoana tu! !!!!!!
Mi nilipoona safu ya uongozi tu wakati wa mabadiliko ya baraza matumaini ya elimu bora yakikata!!!

Wabunge ndio wakulaumiwa zaid sababu hawana ukweli na umoja wa kuifanya serikali kuwa inayojali na inayotekeleza!!!!!!
Leo wako kama wana uchungu na nchi lakini hao wanaolia leo ndio hawataki katiba bora sasa haya si machozi ya mamba!!!!!!
 
Umeongea vizuri, ila hapo kwenue katiba bora ndo nini? Katiba si makaratasi tu.
 
Muheshimiwa supika jimbo langu lina matatizo kede kede ya elimu watoto hawana madawati vitabu havitoshi kwingine hakuna kabisa walimu nao ni tatizo kwan kuna shule nying jimbon kwangu zina upungufu mkubwa wa walimu. LAKINI MH WAZIRI NAOMBA NIKUHAKIKISHIE KUWA NAUNGA MKONO BAJETI ASILIMIA MIA MOJA(100% ) makofi pwa! Pwa! Pwa! Pwa!
 
Siasa katika elimu haifai.., elimu ya tanzania inazidi kupotea , suluhusho linaitajika natusipo kuwa makini tunazalisha wanafunzi wasio kuwa a manufaa kwenye jamii.,
 
Mbunge James Mbatia amepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la elimu nchini kwa kutoa ofa ya Tsh milioni 10 kwa profesa yeyote wa hesabu atakayefanya mtihani wa hesabu wa drs la saba (NECTA 2014) na kupata alama zote (100%).

Wakatia akichangia hotuba ya Wizara ya Elimu bungeni, Mbatia alisema kwamba mtihani huo ulitungwa ovyo kabisa ambapo maswali 31 kati ya 50 ni magumu sana kwa wanafunzi wa darasa la saba, 11 hayana majawabu na 4 yamekosewa. Mbali na somo la hesabu, masomo ya kiswahili na kiingereza nayo yanadaiwa kukosewa.

Source: Mwananchi

NYONGEZA:
Nilibahatika kuona mtihani wa majaribio wa hesabu na kiingereza wa mwaka 2012, ambao nakala yake imo humu JF. Mtihani huo ulikuwa na makosa mengi ya kiufundi na maswali mengi hayakuwa na majawabu.

MAONI YANGU:
Elimu yetu ipo ICU. Haya yote yanachingiwa na serikali yetu kuchanganya elimu na siasa kwa manufaa yao binafsi.
Nini kifanyike ili kuokoa jahazi la elimu yetu linalozidi kuzama kila mwaka. Tujadiliane jinsi ya kunusuru elimu ya watoto wetu.
 
Kama maprofesa hawataweza kufanya hesabu mbona watoto wadogo wanalazimishwa kufanya huo mtihani? Kweli CCM inaimaliza nchi hii kielimu......haya watanzania tujiandae kisaikolojia kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe
 
Mbona jibu umeshalitoa hapo? Ni kwamba tumechanganya taaluma na mambo ya siasa. Walimu hawana motivation, bajeti ya Elimu bado ni ndogo sana. Maboresho katika elimu kuanzia ya awali yanahitajika sana, kuanzia vyumba vya madarasa, maabara na vifaa vingine vya kufundishia, nyumba za walimu na malipo stahiki kwa walimu wetu. Zaidi ya hapo tutaendelea kutwanga maji kwenye kinu huku tukishuhudia elimu yetu inavyodidimia kwa kasi ya ajabu.
 
Mbunge James Mbatia amepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la elimu nchini kwa kutoa ofa ya Tsh milioni 10 kwa profesa yeyote wa hesabu atakayefanya mtihani wa hesabu wa drs la saba (NECTA 2014) na kupata alama zote (100%).

Wakatia akichangia hotuba ya Wizara ya Elimu bungeni, Mbatia alisema kwamba mtihani huo ulitungwa ovyo kabisa ambapo maswali 31 kati ya 50 ni magumu sana kwa wanafunzi wa darasa la saba, 11 hayana majawabu na 4 yamekosewa. Mbali na somo la hesabu, masomo ya kiswahili na kiingereza nayo yanadaiwa kukosewa.

Source: Mwananchi

NYONGEZA:
Nilibahatika kuona mtihani wa majaribio wa hesabu na kiingereza wa mwaka 2012, ambao nakala yake imo humu JF. Mtihani huo ulikuwa na makosa mengi ya kiufundi na maswali mengi hayakuwa na majawabu.

MAONI YANGU:
Elimu yetu ipo ICU. Haya yote yanachingiwa na serikali yetu kuchanganya elimu na siasa kwa manufaa yao binafsi.
Nini kifanyike ili kuokoa jahazi la elimu yetu linalozidi kuzama kila mwaka. Tujadiliane jinsi ya kunusuru elimu ya watoto wetu.

I real admire the man. Huyu Mbunge ananikosha sana kwa michango yake inayosimamia sana katika elimu. Nakumbuka sana ile hoja yake aliyoitoa bungeni kuhusu kumtaka Waziri wa Elimu au yeyote alete CURRICULUM ya nchi yetu na kinyume chake watu wakaleta Syllabus. Sera ya elimu ya elimu(ESR) ya mwaka 1967 mpaka leo haijabadilika at the sametime sera hyo haifanyiwi kazi. Bado waziri anaulizwa ipi educational policy ya nchi yetu hata hajui. Waziri mzima anashindwa kujua tofauti ya policy of education, vision and mission of education pia Curriculum na Syllabus. Too sad.
 
Uhai wowote wa taifa unatokana na Elimu bora kwa wananchi wake hasa watoto - taifa linalodharau elimu ni taifa MFU - ni taifa linaloelekea kaburini - ondoa CCM haraka sana kuinusuru elimu ya nchi yetu.
 
Mkuu CHAMVIGA upo aiseee, karibu sana UKAWA..
 
Usiwasumbue maprofesa wote humo bungeni bali wape Kawambwa na Jenister Mhagama wakisaidiana na lukuvi hao watatu wanatosha kugombea mil 10/-
 
Uhai wowote wa taifa unatokana na Elimu bora kwa wananchi wake hasa watoto - taifa linalodharau elimu ni taifa MFU - ni taifa linaloelekea kaburini - ondoa CCM haraka sana kuinusuru elimu ya nchi yetu.

Mbele ya CCM elimu yako si kitu......haya uliyoyasema utaambiwa wewe ni mjinga.
 
Back
Top Bottom