TLAWI AKONAAY
Senior Member
- Sep 16, 2016
- 110
- 62
Mtu kwenda shule ni kitu kizuri na mtu kupata elimu ni kitu kizuri zaidi ili mtu upate elimu siyo lazima uende shule.
NAOMBA TUSIKILIZANE VIZURI
nakumbuka zamani nilipokuwa mdogo baba aliniambia soma sna ili upate elimu. ukifaulu vizuri utakuwa na maisha mazuri.
Kibao cha shule ya msingi niliyosoma kilikuwa na maneno kuwa ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA. Nakumbuka motto wa shule ya secondary niliyosomea,nakumbuka motto wa chuo kikuu nilichosomea vyote hivi viliniahidi maisha mazuri na mafanikio baada ya kuhitimu masomo yangu.
Nakumbuka hotuba ya baba yangu kwenye mahafali ya sherehe yangu ya shahada ya kwanza alisema mwanangu, wajibu wangu mimi kama mzazi wa maisha bora kwako nimeshautekeleza.
Sasa kazi ni kwako. sikujua kwamba baba na walimu walionifundisha wangeweza kunifundisha makosa makubwa wakati mwingine. kumbe elimu bora niliyofundishwa ilikuwa ni kutafuta kazi badala ya kutafuta pesa na utajiri. hivi umewahi kuona kuwa tajiri ameajiriwa?.
Lakini watu hawa wangewezaje kunifundisha utajiri?. amini nakuambia maskini au mwalimu maskini hawezi kukufundisha utajiri.kamwe labda nikuulize ndugu yangu shule zote ulizoenda umewahi au umeshawahi kufundishwa utajiri au kukutana na walimu matajiri wangapi?.
Ndugu zangu sisemi kwamba elimu ni mbaya, ila elimu bila malengo ni mbaya sana. elimu ni nzuri pale mtu anapopata kwa makusudi maalumu.
elimu bila malengo au kusudi ni kifungo cha fikra.
Ninachomaanisha hapa ni kwamba shuleni walituambia elimu ni ufunguo wa maisha, sawa, ila kuwa na ufunguo bila kujua kitasa kilipo ina nini?
Elimu bora ni ile inayokupa ufunguo cha kukiona kitasa kilipo na siyo kweli kwamba hupatikana shuleni tu.
Nisikilizeni vizuri. Kuna dhana ya elimu na dhana ya shule na ikiwa elimu ni ufunguo wa maisha basi shule ni kitasa......narudia elimu inapatikana shuleni ila elimu bora haipatikani shuleni. Baba yangu aliamini kuwa kufaulu mitihani ya shuleni huu ndio mwanzo wa mafanikio yangu.
Lakini kumbuka wanaosahihisha hii mitihani shuleni huwa wanatummia kitu kinachoitwa marking scheme na endapo ukinyimwa marking scheme wanakuwekea kosa. Halafu ndio haohao wanakuambiia kuwa shuleni kuna taalum, kuna maono yako, akili na upeo wako wa kifikra. kivipi......kwa mfano hivi ninani asiyejua kuwa binadamu wote tuko tofauti?.....kwanini shuleni wanatupima kwa njia moja ya mitihani?..... na ujue kwamba kufaulu mitihani ya shuleni haikuhakikishii wewe kupata mafanikio mazuri ya kimaisha....
Mpaka hivi ninavyoongea na wewe sijawahi katika misha yangu ninayoishi sijawahi kutumia Logarithim, Pythegorus theory, Calculus,General quadriatic equation,na mpaka sasa sijajua hata thamani ya x.
Miaka yote niliyofundishwa kw akingereza mpaka leo kingereza changu ni chakuungaunga tu. Shuleni nilikaririshwa na kufundishwa vitu vingi sana ambavyo sivitumii katika maisha yangu ya kila siku.
SASA NIAMINI MIMI.
pamoja na shule niliyonayo ya shahada ya uzamili ya sayansi ya fedha , mafanikio ya msingi ya maisha yangu ni kilimo cha vitunguu saumu.niliyojifunza ndani ya wiki mbili tu. jamii inayonizunguka inaamini kwamba shule ndiyo kila kitu. Usiamini kila kitu ambacho jamii inakiamini. jifunze kufikiria peke yako na fanya maamuzi mwenyewe. kwa sababu jamii hiyohiyo inaamini kutoa mimba ni mbaya na ndiyo jamii hiyohiyo inayoamini, inashangaa watu kubeba ujauzito kabla ya ndoa.
wako wachungaji wanaohubiri kuhusu kuwasaidia masikini na kumtolea mungu ila wao wanamiliki ndege zao binafsi.....usiamini kila kitu ambacho jamii inakiamin. Elimu ni yale maarifa machache unayohitaji na kuyatumia kwenye maisha yako ya kila siku baada ya miaka yote ya kukaaa darasani.
mfumo wa elimu pamoja na mitaala tuliyonayo humfanya mwanafunzi kutumia muda mwingisana ambavyo haendi kuvitumia katika maisha yake ya kila siku au kumfanya kutumia muda mwingi sana kujifunza vitu vichache sana ambavyo ni muhimu katika maisha yake
.TAFUTA ELIMU USITAFUTE SHULE
.TAFUTA PES USITAFUTE KAZI
.TAFUTA MAARIFA USITAFUTE VYETI
Ndugu yangu tukubaliane kwamba ili binadamu aweze kuishi vizurina kuweza kuya mudu maisha yake , unapaswa kuwa elimu ya kutosha, ujuzi pamoja na ufahamu wa mambo mengi tofauti lakini elimu hiyohiyo au ujuzi huo unapaswa kuwa na uhusianowa moja kwa moja na mazingira ndipo utaweza kufanikiwa
watu wanachanga sana vitu.... kuna tofauti kati ya mtu mwenye elimu na mtu msomi?....yaani unaweza ukawa umesoma sana lakini huna elimu na maarifa ambayo yanaweza yakakufanya ukaishi vizuri. Lakini pia unaweza ukawa hujasoma shule kabisa ila ukawa na elimu na maarifa yakukufanya ukaishi vizuri. Hivyo basi mafanikio ya kimaisha ndiyo kipimo sahihi cha elimu na maarifa aliyonayo mtu.
Hapa ndipo utakapokuta profesa wa chuo kikuuu ana maisha magumu sana kiuchumi kulio mfanyabiashara aliyeishia darasa la saba tu.Mtu mwenye elimu bora ni yule anayejua kitu kutoka kwenye kila kitu na si anayejua kila kitu kwenye kitu.
ninaye rafiki yangu ambaye kwa zaidi ya miaka 5 alisoma na kubobea kwenye udaktari wa meno tu. hivi ukiacha menokwenye maisha kuna mambo mangapi muhimu ya maisha yakujifunza?. lakini cha ajabu ni kwamba huyu bwana kwa zaidi ya miaka miwili anafanya kazi na kulipwa kama meneja wa hospitali. Ni elimu aliyonayo
.TAFUTA ELIMU USITAFUTE SHULE
.TAFUTA PES USITAFUTE KAZI
.TAFUTA MAARIFA USITAFUTE VYETI
naomba nimalizie kwa kumnukuu marcum x yeye alisema " JUST BECAUSE WE HAVE COLLAGES ANA URNIVERSITIS DOES NOT MEAN WE HAVE AN EDUCATION"