Hiyo inatokana na maumbile ya miili kati ya wanaume na wanawake. Binadamu wote wanatoa sauti zao kwa kutoka kwenye vocal tract, yaani koromeo. ambayo kwa watoto wadogo ni fupi sana ndiyo maana wanakuwa na sauti za juu zaidi. Kwa watu wazima, wanaume wana vocal tract zenye urefu wa kama cm 17 wakati za wanawaek zina urefu wa kama cm 14 tu. Karibu na mwishoni mwa vocal tract, kuna misuri ijulikanayo kama vocal chords; misuli hii inapocheza cheza (vibrate) ndiyo hutoa sauti. Sauti inayiskika kutoka kinywani mwa mwimbaji inategema sana na urefu wa vocal tracts zake, ulaini wa wa vocal chords zake, na vile vile kipenyo cha vocal chords zake. Sasa wanawake maumbile yao yana vocal chords laini, zenye kipenyo kidogo na vile vile vocal tracts zao ni fupi. Hivyo kiasili sauti zao zinakuwa na pitch ya juu zaidi kuliko wanaume.
Maelezo hayo unaweza kuyatafrisi kivitendo kwa kuangalia muundo wa aina mbali,mbali za saxophones. Bass saxophone inatumia reed (vocal chords) ngumu, na saut inasafiri umbali (vocal tract) mrefu kutoka kwenye reed hadi kwenye kinywa cha saxophone hiyo ukilinganisha na Soprano saxophone.
View attachment 1302763