MUSICAL NOTES -3 (SCALES -Cont'd)
Ili kuweza kutambua sauti za kutumia kwenye mzani mmoja katika octave yoyote inabidi tuingie ndani kidogo kwenye nadharia ya muziki. Nadharia hiyo hutoa kanuni mbili kuu kama ifuatavyo:
Kanuni ya Kwanza: Sauti asili kwenye kwenye OCTAVE moja zinatofautiana kwa
nusu hatua (
Half Steps) au
Semitones. Nusus hatua mbili zinaunda
hatua kamili (full step) au
Tone. Kwa hiyo Octave moja ina hatua tano na nusu kama inavyoonekana katika jedwali hili, iwapo utachukulia kuwa sauti ya kwanza ni hatua sifuli (Wengine hutafsiri kuwa sauti ya kwanza ni hatua ya kwanza pia, na hivyo kuwa na hatua sita na nusu).
Sauti | 1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 | 8 | 9 | 10 | 11 | 12 |
Hatua | 0 | 0.5 | 1 | 1.5 | 2 | 2.5 | 3 | 3.5 | 4 | 4.5 | 5 | 5.5 |
Kanuni ya pili: Sauti zinazokubaliana katika OCTAVE moja zinapishana kwa kufuata mipangilio ya aina mbili. Mpangilio wa kwanza unaitwa
major scale (mizani kuu), na mpangilio wa pili unaitwa
minor scale (mizani ndogo).
Mpangilio wa
major scale unakwenda kwa hatua za
KKN-K-KKN, yaani
K ni kuruka hatua kamili, na
N ni kuruka nusu hatua. Kila
KKN ni tetrachord moja, halafu -K- iliyopo kati ya tetrachord ya chini na tetrachord ya juu ni hatua kamili inayounganisha tetrachords hizo. Kwa hiyo iwapo sauti ya kwanza kwenye OCTAVE ni sauti asili namba 1, sauti asili zitakazoshabihiana katika octave hiyo kwenye major scale ni sauti za
1,3,5,6,8,10,12, (1). Wakati
(1) ni sauti ya kwanza kwenye OCTAVE inayofuatia. Major scale ina sauti zote zilizozungumziwa hapo juu: kupumizikia, mpito na kuchangamsha.
Minor scales pia zina sauti hizo tatu: kupumizikia, mpito na kuchangamsha. Ila sauti za kuchangamsha kwenye minor scale siyo kali sana kama zile za kwenye major scale; ndiyo maana nyimbo nyingi za minor scale huwa ni za majonzi. Kuna aina tatu za minor scales:
natural minor, harmonic minor, na
melodic minor. Scale ambayo ni maarufu zaidi ni ile ya Natural minor scale. Harmonic na Melodic minor scales ni modification ndogo tu kwenye natural minor kwa kuuongesa msisistizo ama sauti ya saba au sauti ya sita na ya saba kwa pamoja. Ingawa nyingi zinatumika zaidi katika nyimbo za kwaya za makanisani, wanamuziki wa pop music huzitumia pia katika vipande vifupi vifupi vya nyimbo zao.
Mpangilio wa Natural Minor kutoka kwenye sauti ya kwanza ni
KNK-KNK+K ambapo
K ni kuruka hatua kamili (
Tones), na
N ni kuruka nusu hatua (
Semitone) kama ilivyoelezwa hapo juu. Katika scale hii,
KNK ni tetrachord moja wakati ile
+K ya mwisho ni hatua nzima ya kuhamia kwenye Octave inayofuata. Kwa hiyo ukianza na sauti asili namba 1, sauti zake zitakuwa ni nyingine zitakuwa ni
1,3,4,6,8,9,11,(1). Scale hii haina leading note, kwa hiyo ni scale ambayo hutumika sana kwenye nyimbo ambazo zinatumia Octave moja tu na hutawalaiwa sana na sauti za
median, subdominant, dominant; sauti za
submendiant zinaingia kidogo sana kiasi kuwa wimbo unakuwa hauchangamshi kabisa. Mfano wake ni wimbo huu hapa; ingawa ni wimbo mzuri, msikilizaji wake anakuwa kama ana majonzi na huenda asiweze kunyanyuka kitinini kucheza.
Mpangilio wa harmonic minor kutoka kwenye sauti ya kwanza ni
KNK-KNK+H ambapo
K na
N zina maana kama ilivyoelezwa hapo juu huku
+H ikiwa na maana nusu hatua inyounganisha Octave inayofuata. Tetrachords za harmonic minor ni sawa kabisa na tetrachords za natural minor, yaani
KNK. Kwa hiyo iwapo sauti ya kwanza ya harmonic minor ni 1, basi sauti za scale hiyo zitakuwa
1,3,4,6,8,9,11,(1). Kwa upande wake, tetrachords za melodic minor ni tofauiti sana na tetrachords nilizokiwsha taja hapo juu, yaani wakati scale zote hapo juu zina tetrachords zinazofanana, scale hii ya melodic haitumii tetrachords za aina moja. Tetrachord ya chini inapanda kwa step za
NKK wakati tetrachoud ya juu inapanda kwa
KKN, yaani tetrachord ya kwanza inapanda kwa kasi na ile ya pili inapanda polepole. Scale hii huanza kuwa kuruka step kamili kutoka sauti ya kwanza, halafu huunganisha tetrachord mbili kwa muundo wa
K+NKK-KKN. Kwa hiyo ukianza na sauti asili ya kwanza, sauti za scale hii zitakuwa ni
1,3,4,6,8,9,10,(1) Sitatoa mifano ya hizi harmonic minor na melodic minor katika post hii ila nitazizungumzia tena huko mbele ya safari.
Maelezo hayo yanatosha kwa leo. Kwa wanaojua nadharia ya muziki watayaona ya kawaida sana ila kwa wale wanaotaka watoke kimuziki kwa kutumia sauti zao bila kuwa na shule yoyote, ni vizuri kuyajua haya wakati wakiwa wanatayarisha tungo zao.Katika post ijayo tutaanza kuangalia kwa undani zaidi jinsi ya kujenga mizani hizo za muziki.zaid.