Elimu na mapenzi vinaingiliana vipi?

Elimu na mapenzi vinaingiliana vipi?

habari ya hapa

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
12,788
Reaction score
8,755
JF ina magwiji na wabobezi wa kila aina, kuna magwiji wa mapenzi kama si mahaba, kutongoza, kukata viuno, kusimamia kucha dk 90 pasi na kuvuta pumzi, siasa na mambo kadha wa kadha.

Mara kadhaa nimeona matangazo ya watu kutafuta wenza lazima waweke na kiwango cha elimu, au mtu mmekutana huko kwa njia, lazima aulize elimu yako.

Elimu na mapenzi vinauhusiano gani?

Labda ingekuwa

Mapenzi bila pesa ningewaelewa ni sawa na nzi kwenye kidonda, mgonjwa na uji, vile vile huwezi tenganisha CCM na rangi yake ya kijani.

Mapenzi bila pesa hakuna?

Je, mapenzi bila elimu?

Nawasilisha kwenu magwiji
 
Wewe unaweza kuchukuwa MTU ambae hajui kusoma na kuandika ?

Elimu INA nafasi katika mapenzi kwa ajiri ya mawasiliano na uchumi pia !

Ni hayo tu ya kwangu Leo !
 
Elimu kwa maana pana ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa makusudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine.
Hivyo basi mapenzi ni maisha na maisha ni mapenzi, Katika hali ya kawaida ili kuleta tija kwenye mahusiano lazima kuwa na mtu ambaye mnaweza kuwasiliana,aliyejengeka kiakili,mwenye maarifa ili kuweza kusaidiana katika maisha ya ndoa. Kusaidiana kiuchumi, kiafya, kijamii, kielimu na Kujenga familia iliyo Imara, Bora na yenye matumaini.
Mfano: ukiwa na mwenza mwenye fani ya Daktari, Una uhakika kupata ushauri wa kiafya wakati wote.
Ni mtizamo na maoni yangu tu.
 
Comment yangu ya siku!
 
Hii kweli mkuu, na mimi nimekuwa nikijiukiza haya mambo sana yanavyo kwenda,

Alafu huwezi amini hao wanaouliza eti elimu wao ndio kajamba naani hawana lolote kichwani elimu hawana,
 
Basi oa bila kuuliza na kama unaemtongoza atakuuliza huyo achana nae mkuu, ndo utaona impacts ya elimu kwenye mapenzi dunia ya leo!
Nimewaona wengi waliooana wasomi, wako kawaida tu maisha yao kuliko hata wenye elimu za kawaida
 
Elimu kwa maana pana ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa makusudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine.
Hivyo basi mapenzi ni maisha na maisha ni mapenzi, Katika hali ya kawaida ili kuleta tija kwenye mahusiano lazima kuwa na mtu ambaye mnaweza kuwasiliana,aliyejengeka kiakili,mwenye maarifa ili kuweza kusaidiana katika maisha ya ndoa. Kusaidiana kiuchumi, kiafya, kijamii, kielimu na Kujenga familia iliyo Imara, Bora na yenye matumaini.
Mfano: ukiwa na mwenza mwenye fani ya Daktari, Una uhakika kupata ushauri wa kiafya wakati wote.
Ni mtizamo na maoni yangu tu.
Nakubaliana nawe lkn kuna wengine ushauri hawapi toka kwa wenzao isipokuwa kwa marafiki na ndg
 
Ili mtu aitwe msomi, anatakiwa kuwa na elimu ya kiwango gani?
 
Kutokujua kizungu nmekosa
Wake wengi sana wa university
 
Back
Top Bottom