trip2dubai
Member
- Nov 4, 2014
- 5
- 2
Je unajua yakuwa mchunga mbuzi wa jangwani, ambayo tunajua sote haioti kitu na kavu, kajenga ghorafa ndefu duniani and mji wake umekuwa maarufu ulimwenguni?
Mie si mwamndishi wa habari wala philosopha, lakini kwa matokeo tunayoshuhudia mbele ya macho zetu miaka na miaka ambayo hayarudi nyuma ni kitu ya kukuna kichwa na kujiuliza kwanini mataifa ya Africa hayaendelei? Kwanini nchi kama ya Tanzania na zingine pia haziwezi kuhudumia umeme masaa 24 mpaka leo? Ingawaje tuna mali alisi kama mito, na vitenga vya maji ya mvua ambayo tunapata sana kuliko ile nchi ya jangwa kule Uarabuni.
Inakuaje mji kama wa Dubai ambayo ipo United Arab Emirates (UAE) inaweza kuhudumia wateja maji na umeme bila ya matatizo licha yukuwa inaendelea kila mwezi, mji kupanuka, na magorofa na matower marefu kujengwa, ambayo huwezi kufika ghorofa za juu ila kwa lifti zinazotumia umeme. Hawana mito na mvua kama Africa inayosaidia kutoa umeme na wanaweza kuendelea? Utasema wanayo petroli na hizo petroli dolar ndiyo inayoleta yote.
Mheshimiwa hapo umekosea, sikubaliani nawe, zipo nchi nyingi duniani zinatoa petroli na gasi kutoka Africa, Mashariki ya Kati pia na nchi nyingine, lakini hawaendelei na nchi maskini.
Kwa hivyo nini sababu? Elimu na Maarifa. Utasema, Elimu serikali zetu zimeeka mbele na tunayo, lakini, je tuna maarifa? je, tunatoka nje ya nchi zetu na kujifunza na kutafuta maarifa kutoka mataifa mbalimbali? Je vijana tunawachukulia kwa makini au tunawaacha kuuza karanga? Viongozi walio kaa kwenye viti je? wanayo Elimu ya kimataifa na Maarifa? au kwakua ni mkuu wa kabila, mkoa, kitongoji , ndiyo tunamchagua kuwa kiongozi?
Je Afrika ipo tayari kujifunza maarifa mpya na kuwapa vijana kila msaada wanohitahi ili kutekeleza maarifa hizo? Wananchi wengi wemeawachwa kwenye biashara za mitaani ambayo haiwezi hata kusaidia jamii zao acha nchi. Wananchi wamepewa elimu lakini ni ya kukamilisha tu mahitaji muhimu na si kuendelea na kutafuta maarifa zaidi.
Kujuwa kuandika na kusoma isiwe cheche na shawishi yakutafuta elimu. Iwe zaidi ya hiyo. Iwe Elimu na Maarifa tunazipata ni yakunyanyuwa jamii na nchi zetu.
Ikiwa mchungaji mbuzi ambaye anaishi jangwani kaweza kunyanyua nchi yake na kuwa namba ya kwanza duniani, kwanini sisi wenye rasimali nyingi nchini kwetu, misitu, mito - maji kwa wingi, madini, mazao na mambo mengi tunashindwa na mpaka sasa tunategemea misaada? Je tunachaguwa viongozi wetu kwa kutazama nani msemaji mzuri ili tupate misaada au tunatazama nani atatumia Elimu na maarifa kuinyanyua nchi kwa kutumia resousi zake.
Tunafanye kila njia kutafuta Elimu na Maarifa. Maana Elimu haina mwisho. Nimekupeni mfano wa mji wa Dubai, ni mji inapokea sasa watu kutoka duniani kote na hata kwa mara ya kwanza imechaguliwa kuwa mji mchaguliwa Expo2020. Kwa mara ya kwanza inafanjika Mashariki ya Kati. Expo2020 inafanyika kila baada miaka 5 katika miji inayochaguliwa. Hivi 2015 inafanyika katika mji mmoja Itali.
Inakuwa muda wa miezi 6, na nchi zote Duniani zinashiriki hata nchi za Africa. Na Ujumbe wa Dubai Expo2020 ni ""Connecting Minds creating future" ina maana tunashirikian kwa maarifa ili kujenga mustakbali ya jamii zetu. Mwaka 2020 haipo mbali, na nategemea nchi zetu za Mashariki ya Africa itachukuwa nafasi hii kushiriki na kutafuta maarifa.
Inaweza ikawa mtu binafsi, au mwenye biashara na serikali, wote wanakaribishwa Dubai. JiJi la Dubai ni ukurasa ambayo inakupa picha ya mji wa Dubai kwa lugha ya Kiswahili.
Narudia, Elimu Haina mwisho na Maarifa haina Upeo. Tafuta na utapata. Tumia internet kutafuta maarifa pia.
Shukran na Ahsanteni
Hassan Al Jabri
Founder
Tripiladubai.com