Michael Ngusa
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 1,637
- 463
Leo nimeamua nimwagike kuwahusu Bongo movie, wanaofanya hii shughuli hasa kampuni zilizoshika soko. Sitaki kuamini yasemwayo kuwa wengi wenu hamkwenda shule na hii kazi mnaifanya kiujanja ujanja (kwa ubunifu wa kujifunza kupitia tutorials za Youtube), lakini hata kama ni hviyo, huko mnakojinfunzia hamkuwahi kufunzwa "Art Direction & Photography"? Eneo hili ndio linahusisha utengenezaji wa theme ya cover la movie pamoja na shughuli zote za photography kwenye utengenezaji wa filamu.
Kwa uzoefu wangu na filamu za bongo, cover/picha za makasha/poster hazina uhalisia wa movie yenyewe. Yaani hawa watu baada ya kushoot na kuproduce filamu, wanaenda photography session kwa ajili ya kutengeneza cover...matokeo yake ni cover la filamu ambalo wahusika wamekaa mapozi ya passport size, au mapozi yanayotokana na command za mpiga picha wa harusi i.e. "smiiiile..!", na mikao ya mwili na nyuso ambapo unaona kabisa huyu mtu hapa aliambiwa "betua vidole, pindisha mdomo! n.k.
Sawa wanatumia Photoshop, the world champion, hig-end Adobe flagship for Graphic Design lakini hawana "deep editing capabilities" au hawaijui kwa undani Adobe photoshop kiasi cha kuproduce "real-life images" kwa kuzingatia vivuli (kama wahusika wa cover wamesimama), background integration n.k., ili mradi tu wamepigwa picha, wametolewa background na kupachikwa mbele ya wallpaper iliyodownloadiwa kwenye Google images.
Hivi ndivyo cover inavyotakiwa kuwa:
Option ya kwanza: Cover itokane na scenes za movie husika, yaani anaexport some frames na kuziedit kuproduce cover, kama itahusisha thirdy party photographies ni sawa lakini iwe kidogo na sisi tusijue kuwa hii picha ilipigwa kwa kujitegemea, angalia makasha ya movie za nje ndo utaelewa ninachomaanisha...the cover should live the film, should draw attention (sio attention fake za suggestions za mpiga picha ati kwamba "kumbatianeni, kaa chini ufanye kama unamuomba msamaha, kunja sura...aa aaa), ukichukua stills za kwenye movie husika ndio zitakuwa na ile exact attention ya tukio halisi. Producers najua wanalijua hili, lakini kwanini hawafanyi hivyo? nahisi ni kwasababau ya low quality cameras wanazotumia, zile stills hazitakuwa HD.
Basi nawashauri elimisheni madesigner wenu namna ya kuproduce film covers/posters zenye uhalisia wa maudhui ya filamu husika, sio kwenye kasha la CD naona choppers na milipuko ya mabumo wakati ndani ya movie sioni bullet hata moja isipokuwa milio tu ya risasi, acheni kuibia halaiki kwa kuuza "polished CD covers" wakati movie hata 720p haifiki...achilia mbali 1080p au vitu vidogo vidogo kama Sound editing, Color grading na Visual effects.
Mkiendelea hivyo bongo movie haivuki border nawaambieni. Jifunzeni kwa Bongo fleva. Msizalishe kazi kama njugu bila kuzingatia ubora wa vitu kama hivi maadamu mpate hizo fixed amounts za Steps Entertainment eti kwasababu Marketing chain inazunguka...hiyo marketing chain inayowapatia hela ya kula ya uhakika ni ile "low profile individuals" accross the country maana mtu anayejitambua hawezi hata kutazama hizo movie zenu, achilia mbali kuinunua kwa buku.
Ni hayo tu.