*JUA MUDA AMBAO MTEJA ANAPASWA KUFANYA UKAGUZI WA MTANDAO WA NYAYA NDANI YA NYUMBA*
*UKAGUZI UFANYIKE KUPITIA WAKANDARASI WALIOSAJILIWA*
Ili kuendana na matakwa ya Kanuni za Umeme za mwaka 2019 (The electricity Installation Service rules 2019), inayolenga kujiongezea usalama na kuondoa upotevu wa umeme, mteja aliyenganishiwa umeme anawajibika kufanya ukaguzi/uchunguzi wa mtandao wa nyaya (wiring) na vifaa vingine kwenye makazi yake kila baada ya muda uliotajwa kama ilivyoanishwa hapo chini.

Nyumba za kuishi *Ukaguzi ufanyike kila baada ya miaka 5*

Kiwanda *Ukaguzi ufanyike kila baada ya miaka 3*

Majengo ya biashara na hoteli *Ukaguzi ufanyike kila baada ya miaka 2*

Hospitali *Ukaguzi ufanyike kila baada ya miaka 5*

Shule na vyuo *Ukaguzi ufanyike kila baada ya miaka 5*

Maeneo ya starehe yenye mikusanyiko (Public entertainment) *Ukaguzi ufanyike kila baada ya mwaka 1*

Kuunganishiwa umeme kwa kipindi maalum (Temporary installation)
*Ukaguzi ufanyike kila baada ya robo mwaka*

Nyumba za ibada *Ukaguzi ufanyike kila baada ya miaka 5*

Vituo vya mafuta ( Fuel filling stations) *Ukaguzi ufanyike kila baada ya mwaka 1*

Maeneo makubwa ya Starehe (Leisure complexes) *Ukaguzi ufanyike kila baada ya mwaka 1*

Magari maalum ya kuhamishika yenye muundo wa nyumba *Ukaguzi ufanyike kila baada ya miaka 3*

Sehemu maalum za kufulia nguo kama mahospitalini na mahotelini *Ukaguzi ufanyike kila baada ya mwaka 1*

Kumbi kubwa za starehe hasa zilizojengwa maalum kwa kupiga disko *Ukaguzi ufanyike kila baada ya mwaka 1*

Taa maalum za dharura kwenye majengo makubwa *Ukaguzi ufanyike kila baada ya miaka 3*
*SAMBAZA KWA WENGINE ILI KUTOA ELIMU NA KUFUATA KANUNI*
*TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO*