Elimu kabla ya mtoto kukaribia kubalehe na ya kiujumla

Amos David Mathias

JF-Expert Member
Sep 3, 2022
1,574
3,029
Salamu ndugu Wana JF

Wazazi ni jukumu lenu kuwalea watoto na kuwafundisha Kila waanachostahili ikiwemo na tahadhari zote wanazotakiwa kuzichukua katika maisha Ili kuishi vizuri.Mnapaswa kufanya hivi Kwa kuwa mna experience ya maisha ya kutosha kwahivyo mnajua vingi na hakuna jipya kwenu.

Wazazi pindi mtoto anapoanza kujitambua Inatakiwa umfunde unavyotaka akue.Maana mtoto ni kama boksi tupu ambalo unaaza kulijaza wewe utakalojaza ndicho kitakachoingia.Tabia zote ambazo hazifai zinatakiwa zikemewe na kurekebishwa tokea mtoto yupo mdogo mpaka anavyokuwa angalau Miaka 12.Naamini ulivyomshape mtoto awe tokea kipindi chote hicho hataweza kubadilika.Lakini ukimlea vibaya hapa ndipo atakapoharibika utashindwa kumrekebisha utamwona kichwa kigumu

Mtoto anapofika Miaka SITA tayari anajitambua anatakiwa aelekezwe mambo yafuatayo:

1 Anatakiwa kuishi maisha yake uliyomfundisha na sio kufuata tabia za watu zitakazompotosha Kwa maana yeye ndiye mwendeshaji wa maisha yake.Yaani asibadilike kuwa na tabia Mbaya.

2 Asipende sifa au Kusifiwa; Sifa ni kitu kibaya kimewaponza wengi yeyote anayefanya jambo Kwa sifa lazima ataharibu au kupata madhara Fulani.Anatikwa kufindishwa kuwa mtu wa kiasi.Asifanye kitu akazidisha kukifanya maana kitamletea madhara na pia asifanye jambo lolote Kwa mhemko ila alifikirie madhara na faida kabla ya kulifanya.

3 Asijishindanishe na mtu yeyote Wala kutaka kushindana na mtu yeyote; Akifanya hivi atajiletea stress zisizo na msingi na hata kuwa na msongo wa mawazo Kwa sababu ya kutaka kuwa kama Fulani.Pia inaweza kumpelekea kufanya jambo ambalo anaweza kujutia na maisha yake yote.

4 Afikirie mara mbili kabla ya kuongea neno lolote; asiwe anaongea ilimradi awe anaongea tu.

5 Jambo lolote likimshinda asiumize kichwa Sana Bali awe wa utulivu na kukubali kuomba msaada Kwa wengine.

6 Asiwe mchoyo na awe mtu wa huruma na kuwasaidia watu.Lakini pia awe na kiasi asizidishe wema.

7 Asifanye jambo ambalo ni zaidi ya uwezo wake

8 Ajue umuhimu wa elimu na asome Kwa bidii Ili afaulu lakini asisome Kwa kujishindanisha na mtu Fulani(Kutafuta sifa)

9 Mtoto pia tangia yupo mdogo Miaka mitatu afundishwe kusali Kadri anavyokuwa na kumuogopa Mungu.Aishi katika misingi ya dini.

10 Awe na marafiki wenye faida na sio watakaompotosha kimaadili yaani akimbie haraka rafiki yeyote anayetaka kumfundisha mabaya

Elimu Kabla ya mtoto kuanza kubalehe

1 Apewe elimu kuhusu kubalehe na namna ya kuishi katika kipindi hiki na aelimishwe kuwa mabadiliko yanayotokea kwenye mwili wake ni ya kawaida asishangae.

2 Anatakiwa atahadharishwe mapema kuhusu kuangalia picha za ngono sehemu yeyote na kuzikimbia popote.

3 Atahadharishwe kuhusu magonjwa ya ngono na kujitunza vizuri ikiwemo kuto kushiriki ngono kabla ya ndoa.Na kama amelekewa kidini itakuwa ni rahisi.

4 Aelimishwe kuhusu punyeto na atahadharishwe na kutishiwa vya kutosha kutokuingia katika mchezo huo mchafu.Pamoja na madhara yake ikiwemo kushindwa kuacha kupiga punyeto pindi tu atakapoanza.

5 Awe makini na marafiki zake anapoenda boarding; asishawishiwe kujihusisha na huu mchezo wa kujichua na pia asishawishike kushiriki ngono kabla ya ndoa.

6 Aelezewe maana ya punyeto au kujichua Kwa kina na matokeo yake nini kinachotokea anapojichua na atahadharishwe.Ikiwemo kupungua nguvu za kiume na hata kushinda kuzalisha na kuwa na majuto na kutamani kujiua.

7 Aishi Kwa kumuoga Muumba na kusali Kila siku na kuepuka dhambi.

8 Aepuke Pombe na kuvuta sigara na atahadharishwe madhara yake vya kutosha

9 Awe na mipaka Asifanye kitu Kwa kujitesa Ili kupata sifa.Awe na self control atahadharishwe madhara ya kucheza michezo kwenye simu ambayo inaleta uraibu na madhara ya kiafya kama mgongo kuuma sana na kupinda mgongo kutokana na kukaa muda mrefu kucheza hiyo michezo.

10 Aelezewe madhara ya kufikiria jambo Sana ikiwemo kupata vidonda vya tumbo na kupata mawazo ya kujiua.Chochote kinachotaka kumfikirisha kupindukia aombe ushauri Kwa watu sahihi.

11 Amtangulize Muumba wake Kwa yote anayofikiria kuyafanya.

Hivi VYOTE vikizingatiwa Kwa kiasi kikubwa utamtengeneza mtoto asiye na majuto katika maisha yake na kujilaumu au kukulaumu mzazi.

Lakini haya malezi yanafanya kazi Kwa watoto ambao hawatapelekwa boarding tangia wakiwa wadogo.Kumpeleka mtoto boarding tangia akiwa la kwanza atakosa malezi aliyotakiwa kupata kwako na atapata malezi ya wanafunzi anaoishi nao na walimu.Ambapo atafanya mambo mabaya Kwa uhuru Kwa kuwa hakuna wa kumkemea na kumuongoza.Atafundishwa kujichua akiwa anaanza kubalehe akiwa boarding.

Malezi ya watoto yanatakiwa yafuatiliwe Kwa Upendo bila kuona haya kumuadhibu panapostahili na kumkemea panapostahili Ili kumjenga.

Niseme tu “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo” .Ni vigumu Sana mtoto aliyelelewa vizuri kutokua Kwa Miaka 15 kubadilika .Ni vigumu pia kumbadilisha mtoto aliyelelewa vibaya Kwa Miaka takriban 15 kubadilika kirahisi inahitaji nguvu.

Hii nguvu kuiepuka unaanza kumfundisha mtoto mema tangia yupo mdogo.Maana Muumba anakupa mtoto asiyejua chochote wewe ndiye utakayechagua umjaze mabaya au mazuri, umfundishe matusi au kuongea lugha ya staha,Umfundishe kuvaa vizuri au kuvaa ovyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom