Elimu juu ya pepo/mapepo

Elimu juu ya pepo/mapepo

Marko 16:17 na ishara hizi zitaandamana na wale wanaoamini, kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya.

Ndugu yangu Mshana Jr kuna vitu umegusia ila vingine huvifahamu.
Ysu alitoa pepo kwa watu wengi sana ukisoma zile injili utaona sema nimekosa mistari ningekuwekea hapa.
Pepo wapo na wanatoka kwa uweza wa Yesu Kristo Mwana wa MUNGU.
Uwepo wa manabii feki ni kweli hili limewekwa wazi kwenye injili pia kwa hiyo mkuu upo sahihi kabisa.
Naconnect dot na uzi wako huu Elimu juu ya pepo/mapepo - JamiiForums

Timeshajadiliana sana hapa jukwaani kuhusu hivi viumbe, asili yake tabia mienendo na utendaji wake.
. Hivi ni viumbe roho kwa maana ya kwamba havina umbo kamili la kimwili
. Huwinda miiili ya kufanya makazi yake sehemu za majini, makaburini milimani na hata kwenye misitu minene
. Kuna mkanganyiko kuhusu lifespan yake... Kuna dhana kuwa mapepo hufa lakini dhana nyingine ikipinga kwa muktadha wa kwamba hawa ni viumbe roho na roho haifi...
.Pepo bila kupata makazi ya kuishi hutaabika na kuwayawaya huku na kule mpaka yapate sehemu ya kutua

Hebu tuone pepo/mapepo kwa muktadha wa manabii na mitume.. Mapepo yatolewayo kwa waumini kwenye ibada zao
Case study ya Rose Mhando
Pepo ni viumbe roho wenye nguvu sana na anapoingia mahali na kufanya makazi basi kumtoa, kuwatoa si kazi rahisi.. Na unapomfukuza hapo alipo humwambii tu TOKAA bali inabidi umwambie aende wapi
Pepo anapoingia mahali huingia pekeyake lakini kadiri nuda unavyosonga huwaalika na pepo wengine kuja kuishi pamoja
Mazingira haya ya kuishi pamoja kuna wakati husababisha kuleta vita ya umiliki kwenye mwili husika..... Hapa mhanga mwenye mwili atapata tabu kwa vita isiyomhusu
Vilevile kuna wakati hawa waombeaji hufanya michezo ya kuwaalika mapepo kwa mkono mmoja na kuwafukuza kwa mkono mwingine... Hii humjenga na kuonekana ana karama kubwa....
Kwenye imani ya Kikristo tunaona Bwana Yesu akiwatimua mapepo.... Kwa kutumia mfano wake huu unaweza kupata maarifa mapya... Je alifanyaje?

Tunaambiwa akiwa NG'AMBO ya bahari alikutana na mtu aliyetoka MAKABURINI mwenye PEPO MCHAFU na makao yake yalikuwa MAKABURINI
Mtu huyu hakuna hata mmoja aliyeweza kumfunga tena hata kwa minyororo kwakuwa alishafungwa maranyingi kwa pingu na minyororo lakini akaikata minyororo na kuvunja pingu
Nuda mwingi alikuwa MAKABURINI na MILIMANI akipiga kelele na kujikatakata na mawe
Basi akamwona Yesu AKAMSUJUDIA kisha akasema NAKUAPISHA USINITESE..... Lakini Yesu akamwamuru PEPO amtoke mtu yule.... PEPO yule aliyejitambulisha kama LEGIONI (tafsiri ya wingi) akamsihi Yesu asiwapeleke nje ya mipaka ya nchi ile (kumbe hata wao wana mipaka)
Basi wakamsihi awapeleke kwenye kundi la NGURUWE, wapate kuwaingia wao.... YESU AKAWAPA RUHUSA... Nao wkawaingia NGURUWE wale na kutimkia bondeni majini.... Jumla ya mapepo/NGURUWE yalikuwa 2000

Hiyo ndio shughuli pevu ya mapepo... Pepo linalomtoka mtu ndani ya dakika 2 hilo ni feki ama la kualikwa... Lakini hata kama leo hii kuna mapepo basi ni malaini na nyoronyoro mno.... Mapepo yanayoruhusu mtu aoge na kuvaa vizuri, mapepo yanayoruhusu mtu ajitambue na kusimulia kila kitu... Haya ni mapepo ya kileo, kidigitali na kinyangema kweli....

Nimemaliza......
 
Hakika siwezi kufahamu kila kitu na nikisema nafahamu vyote itabidi nipelekwe kupimwa bulangata
 
Ni kweli mkuu dunia ina mengi sana... but ni vyema kusaidiana namna hii.
Yule akija ni hili akijazia hapa na mwingine akijazia hakika tutafika.
 
Mathayo 10:1-15 Tunaona Yesu anawapa uweoz mitume wake wakutoa pepo, kufufua wafu, kuponywa magonjwa na matatizo mbalimbali. Kwa hiyo kwa jina la Yesu yote yanawezekana... ila tusisahau manabii wauongo tunaambiwa watatenda miujiza mikubwa na yakushangaza ila Yesu hatawatambua siku ya kiama.
 
Kwa tafsiri ile ya Bible ni ngumu kuweza kutofautisha kwakuwa kwa asilimia 90 viashiria vinafanana
Lakini kwa tafsiri ya kileo tofauti ziko wazi kabisa
Kichaa utamkuta mitaani mchafu kabeba mizigo isiyoeleweka, anaongea pekeyake nknk
Mwenye mapepo utamkuta kaondoka nyumbani safi kabisa na akili zake, kaoga kapendeza akifika kwa nabii akianza kuombewa mapepo yanalipuka lakini baada ya misa anakuwq fresh kabisa mpaka siku nyingine
Hayo atakua kapewa na nabii feki mwenyewe kamrushia then kayatoa, usicheze na roho waovu ndugu.
 
Marko 16:17 na ishara hizi zitaandamana na wale wanaoamini, kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya.

Ndugu yangu Mshana Jr kuna vitu umegusia ila vingine huvifahamu.
Ysu alitoa pepo kwa watu wengi sana ukisoma zile injili utaona sema nimekosa mistari ningekuwekea hapa.
Pepo wapo na wanatoka kwa uweza wa Yesu Kristo Mwana wa MUNGU.
Uwepo wa manabii feki ni kweli hili limewekwa wazi kwenye injili pia kwa hiyo mkuu upo sahihi kabisa.
Naconnect dot na uzi wako huu Elimu juu ya pepo/mapepo - JamiiForums
Ni biblia gani hiyo yenye marko 16:17
 
Hahaha mkuu tukianza kuwalaumu wazungu kwa kutokufahamu kwetu, nikuwaonea. Nimesema hivyo kwa sababu. Kule wana tibu bipolar patients, hysterical patients, mental disabled patients, na hata depression na stress wanatibu. Huku vyote hivyo tuna sema huyo kichaa,kaheuka, karogwa, katupiwa jini, ana mapepo n.k. yani mapungufu yetu ya ufahamu tuna tafuta wa kumlaumu. Tatizo letu kubwa bado ni elimu ya ufahamu wa haya mambo, na hasa upungufu wa wataalamu, kama psychiatrist na clinical psychologist. Mtu anaanza kucheka hovyo, anapelekwa kuombewa eti anapepo, hiyo ndio early prognosis yetu, hatutaki kujifunza the science/physiology behind it. Tuna fanya simple conclusion kwa vitu vinahitaji scientific explanations, vingi vina hitaji proper diagnosis kujua what and why, lakini hatuna hizo diagnostic tools tuna simplyfy eti mapepo hayo, kichaa huyo. It shouldn't be like that mkuu. Sasa hapo ndio tunazalisha hawa manabii feki, wanatuibia tunawalaumu. Hatutaki ku invest kwenye R&D sisi tunataka wengine wafanye sisi tutumie. Ok hata reserch zilizofanywa na kuwa proved hatuzisomi tukazitumia, tukishindwa kutibu ama kwa kutokujua/kufahamu, au kushindwa kudiagnose tunasema, huu ugonjwa wa kienyeji, ohoo mapepo. Ningefurahi kama nasisi tungeshughulisha vichwa vyetu kwenye hayo mambo, tatizo yunayaona eti ni madogo, tunajidai sisi huwa tuna deal na mambo makubwa tu. Kumbe hata hayo makubwa bado hatuwezi. Mkuu ukiacha mbali taaluma yako ya MA yuo can be be a self made clinical psychologist. Tuendelee na mada.
Mzee mmoja alishafariki kwa sasa, Munga Tehenani alikuwa akiandika sana juu ya mada hizi. Na kwa kweli alikuwa vizuri. Mshana ana vitu ila........
 
Siyo mbaya ukishare nasi hizo mada, lengo humu ni kulimika sio kushindana.
 
Timeshajadiliana sana hapa jukwaani kuhusu hivi viumbe, asili yake tabia mienendo na utendaji wake.
. Hivi ni viumbe roho kwa maana ya kwamba havina umbo kamili la kimwili
. Huwinda miiili ya kufanya makazi yake sehemu za majini, makaburini milimani na hata kwenye misitu minene
. Kuna mkanganyiko kuhusu lifespan yake... Kuna dhana kuwa mapepo hufa lakini dhana nyingine ikipinga kwa muktadha wa kwamba hawa ni viumbe roho na roho haifi...
.Pepo bila kupata makazi ya kuishi hutaabika na kuwayawaya huku na kule mpaka yapate sehemu ya kutua

Hebu tuone pepo/mapepo kwa muktadha wa manabii na mitume.. Mapepo yatolewayo kwa waumini kwenye ibada zao
Case study ya Rose Mhando
Pepo ni viumbe roho wenye nguvu sana na anapoingia mahali na kufanya makazi basi kumtoa, kuwatoa si kazi rahisi.. Na unapomfukuza hapo alipo humwambii tu TOKAA bali inabidi umwambie aende wapi
Pepo anapoingia mahali huingia pekeyake lakini kadiri nuda unavyosonga huwaalika na pepo wengine kuja kuishi pamoja
Mazingira haya ya kuishi pamoja kuna wakati husababisha kuleta vita ya umiliki kwenye mwili husika..... Hapa mhanga mwenye mwili atapata tabu kwa vita isiyomhusu
Vilevile kuna wakati hawa waombeaji hufanya michezo ya kuwaalika mapepo kwa mkono mmoja na kuwafukuza kwa mkono mwingine... Hii humjenga na kuonekana ana karama kubwa....
Kwenye imani ya Kikristo tunaona Bwana Yesu akiwatimua mapepo.... Kwa kutumia mfano wake huu unaweza kupata maarifa mapya... Je alifanyaje?

Tunaambiwa akiwa NG'AMBO ya bahari alikutana na mtu aliyetoka MAKABURINI mwenye PEPO MCHAFU na makao yake yalikuwa MAKABURINI
Mtu huyu hakuna hata mmoja aliyeweza kumfunga tena hata kwa minyororo kwakuwa alishafungwa maranyingi kwa pingu na minyororo lakini akaikata minyororo na kuvunja pingu
Nuda mwingi alikuwa MAKABURINI na MILIMANI akipiga kelele na kujikatakata na mawe
Basi akamwona Yesu AKAMSUJUDIA kisha akasema NAKUAPISHA USINITESE..... Lakini Yesu akamwamuru PEPO amtoke mtu yule.... PEPO yule aliyejitambulisha kama LEGIONI (tafsiri ya wingi) akamsihi Yesu asiwapeleke nje ya mipaka ya nchi ile (kumbe hata wao wana mipaka)
Basi wakamsihi awapeleke kwenye kundi la NGURUWE, wapate kuwaingia wao.... YESU AKAWAPA RUHUSA... Nao wkawaingia NGURUWE wale na kutimkia bondeni majini.... Jumla ya mapepo/NGURUWE yalikuwa 2000

Hiyo ndio shughuli pevu ya mapepo... Pepo linalomtoka mtu ndani ya dakika 2 hilo ni feki ama la kualikwa... Lakini hata kama leo hii kuna mapepo basi ni malaini na nyoronyoro mno.... Mapepo yanayoruhusu mtu aoge na kuvaa vizuri, mapepo yanayoruhusu mtu ajitambue na kusimulia kila kitu... Haya ni mapepo ya kileo, kidigitali na kinyangema kweli....

Nimemaliza......

Kwa tafsiri yako ya mapepo. Ni kuwa mapepo ni majini.
 
Mzee mmoja alishafariki kwa sasa, Munga Tehenani alikuwa akiandika sana juu ya mada hizi. Na kwa kweli alikuwa vizuri. Mshana ana vitu ila........
Malizia tu usijali.... Kumbuka Munga alikuwa anaandika kwenye gazeti mimi naandika mtandaoni kwenye mijadala
 
Mshana Jr pepo kumtoka mtu kwa wepesi inategemeana na Nguvu za Mungu alizonazo mtu husika, tunaona Mtume Paulo kivuli chake tu kilitumia kuwatoa pepo, nguo zake tu watu walipona, dhana ya pepo kutoka ndani ya dk 2 napingana nayo
 
Uko sahihi kabisa ila hata hivyo mapepo ya siku hizi dhaifu sana
 
Nadhani kuna tofauti kwakuwa kiasili majini nafikiri yameumbwa kwa moto

Hapo sasa ndio utaona miujiza ya uumbaji.

Majini wana maumnile yao maalumu kwayo yanajitofautisha na viumbe wengine,lakin majini wamepewa uwezo wa kujibadilisha badilisha kimaumbile na yamepewa uwezo wa kumuingilia mtu na kusoma nae kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu.

Majini yamepewa umri mrefu wa kuishi,watu wanao jishughulisha ma kazi ya kuyatoa wanasema wamewahi kuwadiriki mpaka majini yaliyokuwepo zama za nabii Suleyman. Hii ni ziada.

Kaka hapa nahitimisha kwa kusema hivi sababu hizo umezitaja ni sifa anuai za majini waovu na wewe unasema sio kwa sababu ya asili ya malighafi zilizo tumika kuumbiwa kwayo.

Sasa nina swali la msingi hapa. Hayo mapepo yameumbwa kwa malighafi gani mpaka useme hayo mapepo si majini ?
 
Hahaha mapepo HUWA SIYAAMINI. Unajua kuna watu wako Hysterical, wanacheka hovyo, au kulia hovyo au mara kwa mara, na hawaogopi kitu. Makanisani wanasema huyo mtu ana Mapepo. Hospitali wataalam wa vichaa wana sema huyo mtu ana hysteria. Sasa wewe unasemaje?!
Hapo sasa, kwa mfano kuna rafiki yangu, alipata ajali ya gari, alijigonga kichwani.
Baada ya hapo alipoteza fahamu, hata baada ya kurudisha fahamu, amekua na tabia hizo wanazoziita mwezi mchanga, sasa huyu nae watasema ana pepo wa aina gani.
 
Hahaha pepo la magari labda, nchi hii wakishindwa kudiagnose ugonjwa eti unakua umerogwa, au unamapepo.
 
Back
Top Bottom