SoC03 Elimu hubadili hadhi ya ulimwengu

Stories of Change - 2023 Competition

Legend46

Member
Aug 12, 2022
7
1
Kikawaida elimu yetu iko katika mtazamo ambao unawanufaisha wachache, mtazamo wangu unagusia maeneo manne (4) ambayo yakiangaliwa na kuboreshwa basi manufaa makubwa yatakua matokeo yake. kama vile:-

WAKATI WA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI
  • Kila kitu kinaanzia hapa ambapo kijana anaanza safari ya kutafuta elimu. Huu ni wakati ambao unamfikisha mwanafunzi miaka 13 hadi 20 mpaka kumaliza secondari, bado hajapata elimu atakayoweza kuitumia maishani kama sehemu ya ujuzi bali ni elimu ya kawaida. Huku ni kumcherewesha kijana kuzifikia ndoto zake kadri anavozidi kukua au kutofikia kabisa. ukizangatia kwa mtoto mwenye hali ya chini ya kimaisha tayari umri huo anahisabika ni mmoja ya watafutaji katika familia mfano kwenda shambani, kufuga, na kadhalika, anajikuta anajukumu kubwa la kifamilia. Hivyo kunapelekea vijana kupoteza hamu ya kusoma.

USHAURI
  • Kuna haja ya kupunguzwa madarasa, na kuna haja ya kuifanya elimu ya chekechea (nasari) kuwa lazima ili kila mtoto ajifunze kusoma na kuandika kabla umri wa kuanza kusoma msingi, mtoto ataingia elimu ya msingi akiwa anafahamu mengi tayari, hivyo tunaweza kupunguza madarasa kwa style kama hio. Pia Tuchunguze elimu ya SEKONDARI ina manufaa kiasi gani, kwa mtazamo wangu kidato cha 1 na cha 2 au cha 3 na cha 4 vinatosha. kwa maana anachosoma kidato cha 1 na cha 2 kinafanana anachosoma kidato cha 3 na cha 4. Hii miaka 2 ipunguzwe.
WAKATI WA ELIMU YA CHUO KIKUU
  • Huu ni wakati ambao unawagharimu Zaidi masikini, leo hii vyuo haviwaandai vijana kuwa wafanyakazi wenye ujuzi bali wenye vyeti vizuri. Vyuo vinazingatia Zaidi kupima wanafunzi kumbukumbu zao badala ya ujuzi wanaopata. Mafunzo ya vitendo yamekua chini kufundishwa katika vyuo vingi, mfano unakuta mwanafunzi wa TEHAMA, Computer Engineer, Computer Science hawa wote ni wanafunzi wambao tutegemee kuwaona wana ujuzi wa kutengeneza Programu za computa, simu, tovuti, vifaa vya electronic, nakadhalika, badala yake wanaishia kuitambua computer juu juu tu na wachache ambao walikua wakifuatilia nje ya mtaala wa elimu ya chuo kama vile internet ndio wanaojua, Imefika wakati wale ambao walifeli na kuamua kujiunga na Vyuo ufundi ndo wamekua bora kiujuzi kuliko hawa ambao walifanya vizuri secondary, wanaringia vyeti tu kua mtu ana degree na kadhalika.
Mafunzo ya namna hii yanapelekea vijana wasiweze kujiajiri ikiwa watakosa kuajiriwa, hata soko la ajira linawakataa. Inapelekea kijana alichokisomea sicho anachokifanyia kazi.

Kwa vile vyuo havizingatii mafunzo ya vitendo Zaidi, wanafunzi huwa na uelewa mdogo wa matumizi ya vifaa vya kisasa, Elimu hii huathiri hata katika sekta za viwanda na uchumi kwa sababu wale tunaowafundisha ndio wafanyakazi wa baadae,

Hivyo. inapelekea kutokua na Imani na bidhaa, kazi za kampuni zetu nchini Mfano kampuni za kigeni ndio ambazo zinapewa miradi mingi kufanya na michache midogo ndio wanaopewa makampuni ya ndani, hiyo humaanisha hata Serikali hazina Imani na uwezo wa kampuni za ndani. hata katika kazi au bidhaa za kitafiti, sayansi na teknolojia, raia nao hawana Imani nazo. Mfano dawa za matibabu, vifaa vya electronic na kadhalika. Yote hayo yameanzia kwenye utoaji wa elimu na yameleta madhara makubwa hadi kiwango hicho.


HAJA YA KULETWA WASOMI KUTOKA NJE YA NCHI KUJA NCHINI
  • Hii inalenga uongezaji nguvu kwa kuletwa wataalamu. bado naunga mkono hoja ya kuwapeleka wanafunzi nje. lakini kuna madhara yake kiupande fulani Kama ifuatavyo:-
  • Wanafunzi wanaokwenda nje ya nchi huchukulia kama ndio fursa kwao kutoka kimaisha, kitu ambacho kinapelekea kutokua na hamu ya kurudi nchini na kutamani kufanya kazi huko huko.
  • Kuhisi kua Elimu yake haiendani na mazingira ya nchini mwake na kuona kua hakuna mazingira mazuri ya kuitumia, hivyo atakaporudi hata ile hamasa ya kufanya kazi inakua haipo, mara nyingi huwa na dharau katika kuwasaidia wengine, kuwaelekeza na kadhalika.
USHAURI
  • Haja ya kuletwa wataalamu ni kubwa Zaidi maana kuisogeza elimu karibu na mazingira husika kunapelekea kuyaboresha mazingira hayo ili kuendana na elimu inayotaka kutolewa, mtaalamu mmoja anaweza kuwafundisha wanafunzi wengi Zaidi, tofauti na mwanafunzi mmoja kwenda kusoma nje. Idadi itakayopata elimu kwa kuletwa wataalamu itakua kubwa kuliko idadi ya wanafunzi watakaotolewa nje kusoma.
  • Mfano: BENJAMEN wa Nala. Alisoma marekani na sasa amefungua kampuni yake Kenya wakati ni yeye Mtanzania. Binafsi nahisi mbali na sababu nyingine zote, Pia ni kuwa ameona Makampuni makubwa duniani kama vile Microsoft, Google na nyenginezo zinafungua vituo vya teknolojia huko. Hivyo ameona kua vijana wengi watajifunza teknolojia na hivyo atafaidika kwa kupata wataalamu pia.
KUWAENDELEZA WENYE VIPAJI NA NDOTO

Tatizo kubwa la nchi za kiafrica ni kudharau uwezo wa wengine au ndoto zao, uzuri wa watu wenye vipaji na malengo ni kwamba wanafanya jambo ili kufikia matarajio yao ya utaalamu Zaidi kuliko ya kiuchumi. Ila hawafikii matarajio hayo kwa sababu hawapati kuungwa mkono katika kuendelezwa. Inafika wakati Maisha yanawasukuma kuachana na ndoto zao au vipaji ili wayakabili Maisha ya kweli. Mfano. ANATOLI KIIZA ni raia wa Uganda ambae alikamatwa mara kadhaa kwa kuiomba Serikali imruhusu kujaribu kombora lake. Tuachane na alichokitengeneza na tuangalie ndoto au kipaji alichokionesha, hili ndo swala muhimu. Serikali inatakiwa kujali juhudi zake hata kama si kwa kumruhusu lakini imuendeleze mtu huyu ili afikie ndoto zake na aweze kutengeneza kisomi Zaidi.

HITIMISHO
Msemo wa ‘Elimu ni ufunguo wa Maisha’ unaishia katika kupata pesa kupitia elimu tu, ndio ukomo wetu kwa nchi za Africa. Hatulengi kusoma ili tuweze kuwa WABUNIFU, WAVUMBUZI na kadhalika ili tuzidi kukua kielimu, Mwanafunzi huamua kusoma kazi zenye mishara mikubwa hata kama sio ndoto yake au kipaji chake. Kutokana na hilo hata vyuo vinageuka bishara badala ya kutoa elimu husika.

Natambua juhudi zinafanywa ila bado hazitoi matokeo bora, Kila kitu kinaanzia kwenye ELIMU. Ili tuweze kufikia malengo inabidi nchi izalishe wataalamu wa kutosha na sio wenye vyeti vizuri. Kwa mtazamo wangu, kama taasisi na bodi za Elimu wataweka tiketi ya kuingia chuo ni ndoto na kipaji cha mtu kwenye chuo husika badala ya cheti cha kidato cha 4 au 6, inaweza kuleta matokeo bora maana watu watasoma vile wanavyoviota na kuvipigania ili vitimie. Pia kuhakikisha vyuo vina wakufunzi walio bora.

Screenshot 2023-08-01 at 05.43.22.png

Picha ya NATOLI KIIZA akiwa na kombora lake.
Man Seeks Government's nod to Launch his Homemade Missile

NALA TEAM

 
Back
Top Bottom