JFK wabongo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2015
- 3,887
- 3,200
- Thread starter
- #21
Ni ahadi ngumu kutimiza lakini Mungu akijalia ikatimizwa basi umasikini utakua umepunguzwa kwa asilimia kubwa sana. Hali ya mzunguko wa fedha nchini ni mbaya sana jambo linaloathiri biashara zote na si kwamba watu hawana pesa ila kutokana na mwamko wa elimu kipaumbele cha kila mzazi ni kugharamia elimu ya mwanae. Endapo atabebewa mzigo huo basi angalau atamudu kula milo miwili, ataweza kujenga makazi bora, na hata kuweza kunywa soda wikendi kama si bia. Fedha zitarejea kwenye mzunguko na biashara nyingi zitapata uhai.
Elimu bure vyuo vikuu itawezekana kuanzia 2020 siyo kuanzia j3 tar 29 kama lowasa anavyoahidi. Huko ni kuongopea watu.