Elimu Bure Vyuo Vikuu, Lowasa kalenga mbali

Elimu Bure Vyuo Vikuu, Lowasa kalenga mbali

Aiseee yaani billions zipatekane watu kugawana ila elimu haiwezekani.????

Mkataba wa Richmond unatugharimu mil 150 kwa siku. Mhuskika wa Richmond ndo huyo mnantaka. Aliye lazimisha mkataba wa buzwagi ukasainiwa hotelin uingereza ndo huyo mnamtaka halafu mnaimba mabadiliko, zimewatimia kweli?
 
Ndio maana halisi ya mabadiliko.nyie mlidandia hiyo kauli mbiu mkagundua kwenu inaleta ukakasi.maana ccm ni ile ile.
 
Kwa maelezo yako bandiko la kwanza elimu bure iliwezekana sababu ilikuwa idadi ya wanafunzi husika.maana yake kwa sasa haiwezekani sababu wanafunzi wamekuwa wengi.

Wakati huo huo unasema labda miaka ya baadae huku ukisahahu kama ilishindikana mwaka huu kwa sababu ya uwingi Wa wanafunzi,basi miaka ya baadae haitawezekana hata elimu bure kwa shule za chekechea.

Kwa wizi wa escrow,iptl,Richmond,misamaha ya kodi,bajeti kubwa za safar za mh,mikataba mibovu ya madini,
Ni miujiza gani unahiyajika zaidi ya maamuzi kuwa kuanzia sasa elimu bure.

Najua ndani ya ccm haitawezekana miaka 10000,ndio serikali unayoizungumzia hapa??
Ukisoma mabandiko ya wadau utagundua serikali ya ccm iliwahi kutoa elimu bure hadi chuo kikuu. Mzee mtei wa cdm ni mmoja wa watu waliochangia serikali iachane na elimu bure kwa kushnikiza masharti ya IMF na WB. Kwa hiyo cdm hawana moral authority kuadvocate elimu bure.
Hayo madhambi uliyoyataja nitajie hata mojawapo ambao halimgusi rafiki wa lowasa/ wanamtandao aliounzisha lowasa au lowasa mwenyewe? Mpaka hapo naye hana moral authority kupambana na ufisadi.
Niseme nini tena uamini kuwa alipo edo, pia yupo rostam,chenge,et al.?
 
Tanzania bila CCM inawezekana na Vyuo vikuu bila mikopo inawezekana.Ukipunguza Safari za Mkulu kwenda Ulaya kwa asilimia 60 tu unalipa ada na mazagazaga yooote. Hapo bado hujawabana wakina Ridhwani na marafikize wakwepa kodi mashuhuli..Lowassa ni kama gogo la choo!!
 
Mkataba wa Richmond unatugharimu mil 150 kwa siku. Mhuskika wa Richmond ndo huyo mnantaka. Aliye lazimisha mkataba wa buzwagi ukasainiwa hotelin uingereza ndo huyo mnamtaka halafu mnaimba mabadiliko, zimewatimia kweli?

hapana, ziko nusu.
 
hapana, zingine zimelegea.
 
Yawezekana piakwa maoni yako lakin wenye maono ya mbali wanajua fedha ziliko ndiyo hizo wanachezea kwakutupatupa nakutafuta namna yoyote ya kuhujumu uchaguzi na safari zisizo za lazima il mardi héla imetumika.
 
loanboard ni serekali pia, na mkopo unaotolewa ni pesa ya serekali pia so kutolewa bure inawezekana, jamani ifike mahali tuwaze utajiri wa rasilimali na huduma tunazopatiwa kwa takwimu fupi tu mlima kilimanjaro mapato yake kwa mwaka yakizibitiwa yanatosha kugharamia wizara elimu ya Tanzania na kubakiwa na salio
 
Ulipaswa kwenda zaidi ya kuangalia idadi ya wanafunzi tu. Ni vyema ukaangalia population nzima na uwiano wake k umuri.

Ccm imekuwa zero katika matumizi sahihi ya raslimali kwa mustakabalisahihi wa maendeleo ya nchi na hivyo kuendup kuwa na idle resources and man power kubwa, ama uzalishaji usio na tia kwa taifa.

Mchakato wa kutoa elimu bure haukai kisiwani peke yake ni interrelated mpango unaotegemeana sana kwa karibu na mipango mingine kwa ujumla yake ikiwemo kuongeza uzalishaji wenye tija, ukusanyaji sahihi wa mapato na matumizi bora ya raslimali zote ikiwemo watu, na magawanyo sahihi wa mapato ya serikali.

Suala la elimu bure haliwezi kuwa halisi bila kupunguza mianya ya ukwepaji kodi iliyolelewa na serikali ya ccm.

Ni vigumu kuongeza mapato bila kuwekeza kwenye uzalishaji bora na masoko kwa ngazi zote likwemo swala la kufufua sector ya viwanda ambayo ccm imeua na kuzika, kuimarisha uzalishaji kilimo kitu ambacho kimekuwa midomoni na si mioyoni mwa ccm na elimu ambayo ndiyo mwanga katika kila hatua.

Lakini ni jambo lisiloeleweka mtu aseme anaboresha viwanda bila kujua wala kuzingatia upatikanaji wa nishati. Viwanda vinahitaji nishati. Nishati hiyo ya kufanikisha viwanda inatoka wapi ikiwa ccm wanampango wa kuzima hata hivi vimuli muli vya tanesco vya sasa? Hawana hata habari kama viwanda vinamahitaji yake. Ccm wamebaki kunakili kwa juujuu mipango ya UKaWA.

Yako mengi sana ambayo yanahitaji akili nyingine na SIYO CCM ambayo imeyatengeneza eti ijiadai kuyamaliza. Huu utakuwa wehu.

Mfano. UKAWA vipaumbele vyao ni elimu, elimu , elimu katika maeneo yote ya raslimali watu, matumizi na hifadhi ya ardhi yetu na vyote vilivyomo, siasa safi wakianzia na muundo wa katiba mpya ya nchi kwa ajili ya Watanzania na Tanzania yao waitakayo, uongozi bora na matumizi halali, sanifu na sahihi ya nyenzo hizi juu kwa kusukuma mbele ustawi wa taifa la Tanzania katika nyanja zote.

HATUTEGEMEI KUPATA TAFSIRI SAHIHI YA MKAKATI HUU KUTOKA CCM KWA KUWA SI MAONO WALA NIA YAO NA UWEZO HAWANA WA KUBORESHA KITU ZAIDI YA KULINDA MASLAHI YAO TU. KUIGA KOTE HUKU KUTOKA UKAWA NI KUKOSA DIRA, KUTOKUKUBALIKA NA KUTOKUWA NA DHAMIRA SAFI KWA CCM JUU YA TAIFA.

Ninaomba, unapokuwa na swala usilolielewa, kitu ambacho si dhambi, badala ya kujifanya unajua na kutoa hitimisho kwa kuwa hufahamu, jaribu kuuliza kwa kuwa hakuna mtu anajua vyote na huwezi kutoa jibu kwa kitu kiko moyoni kwa mwingine.

MABADILIKO YA TANZANIA NI UKAWA TU NA WALA SI CCM AMBAYO IMESHINDWA MIAKA YOTE NA BADO HAINA MAJIBU, UWEZO WALA NIA YA KUFANYA LOLOTE LA KUIPELEKA TANZANIA KATIKANJIA SAHIHI.

CCM IKAE PEMBENI IONE WENGINE WANAFANYAJE KATIKA KULIONGOZA TAIFA BADALA YA KUJIFNAYA WANAJUA WAKATI WAMESHINDWA.
Unajua maana ya kusema elimu bure mpaka level flani? Kwa taarifa yako, unapoifanya elimu ya chuo kikuu bure technically inakuwa ndo elementary education. Unaposema elimu bure mpaka chuo kikuu maana yake ni elimu ya msingi,sekondari, vyuo vya kati vinavyomwezesha mtu kujiunga na chuo kikuu, na hatimaye elimu ya chuo kikuu yenyewe...
Ili kufikia hapo umetaja mlolongo wa mambo ambayo lazima yafanyike ndipo tuipate. Nikupe hadhi ya kusemea mipango ya mgombea wako, nipanganie time schedule ya utekelezaji wa mambo yatakavyo tupeleka kuwa na elimu bure hadi chuo kikuu.
 
Km serikali ni makini elimu bure inawezakana coz garama haikuvuka trln 1 kwa mwaka
 
loanboard ni serekali pia, na mkopo unaotolewa ni pesa ya serekali pia so kutolewa bure inawezekana, jamani ifike mahali tuwaze utajiri wa rasilimali na huduma tunazopatiwa kwa takwimu fupi tu mlima kilimanjaro mapato yake kwa mwaka yakizibitiwa yanatosha kugharamia wizara elimu ya Tanzania na kubakiwa na salio

Hiyo ya mlima Kilimanjaro kugharimikia elimu ni ngumu maana utalii ni biashara isiyotabirika, pia bajeti ya elimu kwa viwango vya kimataifa inabidi above 20% ya bajeti yote ya serikali. Mlima Kilimanjaro hauna mapato hayo. Tusinunulike kwa ahadi nyepesi, hapa 2015 to 2020 twende na elimu bure secondary, huku tukiandaa mipango ya elimu bure kwa degree za vipaumbele ili kuanzia 2020 ndo tuzianzishie hizo.
 
Yawezekana piakwa maoni yako lakin wenye maono ya mbali wanajua fedha ziliko ndiyo hizo wanachezea kwakutupatupa nakutafuta namna yoyote ya kuhujumu uchaguzi na safari zisizo za lazima il mardi héla imetumika.
Unajua kuwa familia ya lowasa inachunguzwa na serikali ya uingereza kwa money laundery?
 
Tusibishane wakati calculation zipo garama ya kumsomesha mwanafunzi mmoja miaka mitatu haizidi 10m
 
Tanzania bila CCM inawezekana na Vyuo vikuu bila mikopo inawezekana.Ukipunguza Safari za Mkulu kwenda Ulaya kwa asilimia 60 tu unalipa ada na mazagazaga yooote. Hapo bado hujawabana wakina Ridhwani na marafikize wakwepa kodi mashuhuli..Lowassa ni kama gogo la choo!!

Huwezi ukakwepa safari za nje za rais maana zipo pia za matibabu.
 
Tusibishane wakati calculation zipo garama ya kumsomesha mwanafunzi mmoja miaka mitatu haizidi 10m
Level ipi? Msingi, sekondari, vyuo vya kati, Undergraduate au postgraduate? Soma mabandiko yangu kuhusu maana ya elimu bure mpaka level flani..
 
Huenda ni kwa kukosa uelewa kamili au ni kwa kukusudia ila atakuwa kalenga mbali na kukosa shabaha. Gharama za elimu ya chuo kikuu ni kama:-
1. Tuition fee
2. Meals and accommodation
3. Practical training/industrial practices nk
4. Special faculty requirements.
Je ikiwa bure ni kipi kitatolewa bure au vyote.
Je, loans board itafutwa?
Je, kama ikifutwa, mbona hatusikii kuwa wadaiwa wa loans board watafutiwa madeni yao, maana hakutakuwa na wakuyakusanya.
Hii ahadi imepakwa rangi ila ni sawa na kumpa mbu kazi ya kutibu malaria.
Mchague Lowassa kwanza ndo utajua nini kitaondolewa... acho kujiuliza na kujijibu mwenyewe kiufinyu wa mawazo yako
 
Ndio maana halisi ya mabadiliko.nyie mlidandia hiyo kauli mbiu mkagundua kwenu inaleta ukakasi.maana ccm ni ile ile.

Mneamua kumpa mbu kazi ya kutibu malaria bila kujua kuwa kitendo cha kuwang'ata ni tiba kwake ya malaria hiyo hiyo anayowaambukiza nyie. Akiacha kung'ata anakufa yeye..!
 
Mchague Lowassa kwanza ndo utajua nini kitaondolewa... acho kujiuliza na kujijibu mwenyewe kiufinyu wa mawazo yako

Mimi si mtu wa level ya ahadi hewa. Wakati wa uchaguzi ni wakati wa kuahidiwa. Kwa mpiga kura makini lazima azichuje ahadi za wagombea kabla ya kuamua kura ampe nani. Tuache ushabiki lowasa hana mipango ya kufanikisha elimu bure hata kwa level ya chekechea.
 
Back
Top Bottom