Elimu bure iondolewe, watu waanze kulipa Ada

Elimu bure iondolewe, watu waanze kulipa Ada

Uongezee kuwa kwa sasa tz haina uaba wa wasomi kusema kuwa isipowasomesha bure watashindwa kupata wasomi wa kufanta kazi zao na mwisho labda ada ingebaki mjini tu vijijini ndio wasome bure.

Maana kijijini ukiweka ada watakimbia😀😀😀
 
Sihitaji kuambiwa idadi ila ninachojua kila mtu ana mchango katika kodi iwe directly ama indirectly.

Hamna aliye bora dhidi ya mwenzie nyie wenye hela za kulipa ada za shule bora, mbona shule zipo kuna IST pale Masaki mnaweza kupeleka watoto hapo au hata Feza schools.
Mkuu, unajua ni watanzania wangapi wanalipa kodi hasa ile Direct Tax?
 
Elimu Bure imeathiri sehemu nyingine zikiwemo;

1. Wazazi wamekuwa wavivu kuhudhuria mikutano Shule.

2. Wazazi kukosa uchungu wa kufuatilia maendeleo ya watoto wao. Sasa hivi hawatofautishi Shule ya msingi na sekondari

3.Kupunguza ziara za ukaguzi wa Shule na wakaguzi elimu.

4. Shule kuongeza madeni ya wazabuni

5. Hakuna masomo ya ziada/remedial

6.Serikali kushindwa kuajiri walimu wapya licha ya uhaba wa walimu.

7.Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) kushindwa kutimiza majukumu yake na baadhi ya malipo na hivyo kutupia walimu majukumu ikwemo-
i. Kugeuza walimu maafsa TEHAMA wa kusajili wanafunzi
ii.Kugeuza walimu/kuwapa walimu kazi ya kuchapa na kuingiza data na majina ya watahini
iii. Kugeuza walimu kuwa wapiga picha tena bila malipo
iv. Kutupa jukumu la kuchapa leaving certificate kwa Shule.

Kuna mtu atazungumzia nchi za ulaya, yaani mtu anailinganisha Tanzania na Ulaya, inachekesha kweli,

wenzetu wanapunguza mpaka muda wa kazi kwa sababu tayari mataifa yao yameendelea. Ati na sisi tuige😀😀😀😀😀
 
Sihitaji kuambiwa idadi ila ninachojua kila mtu ana mchango katika kodi iwe directly ama indirectly.

Hamna aliye bora dhidi ya mwenzie nyie wenye hela za kulipa ada za shule bora, mbona shule zipo kuna IST pale Masaki mnaweza kupeleka watoto hapo au hata Feza schools.

Sijasema mtozwe hela nyingi😀😀😀 naona ushaanza kulia lia hapa.

Lazima mtoe ada acheni kupenda vya bure,
 
ELIMU BURE IONDOLEWE, WATU WAANZE KULIPA ADA

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Hakunaga kitu cha bure kikawa na thamani, sijawahi kuona popote pale tangu nimezaliwa; hivyo ndivyo naweza anza makala hii.
Kitu cha thamani lazima kigharamiwe, na uthamani wa kitu upo kwenye gharama. Kusema elimu iwe bure kwa kweli ni kujidanganya, ni kushusha thamani ya elimu. Vitu vya bure vinatoka kwa Mungu pekee, lakini kwa sisi binadamu kwa kweli hakuna cha bure. Kama unataka cha bure mwambie aliyekuumba akupe, sisi binadamu hatunaga vya bure. Nikikupa lazima ulipie, ukinipa hakikisha nalipia, mambo ya bure yapo kwa Mungu tuu.

Kitu cha bure hakithaminiwi huo ndio ukweli, hakuna kitu cha bure kikathaminiwa labda kitoke kwa Mungu, lakini vya binadamu sio kweli.

Kwanza kwa nini iwe bure?
Utanijibu ni umasikini, ikiwa umejibu hivyo basi wewe ni mjinga, kwa hiyo kwa vile mtu watu/jamii ni masikini ndio maana utoe elimu bure, alafu unajiona umetoa umeisaidia jamii? Badala ungetengeneza mazingira ya kuuondoa umasikini ndani ya jamii watu waweze kulipa ada, ati wewe unaondoa ada, ajabu sana hii. Hivi utaondoa vingapi? mwishowe utaondoa nauli watu wasafiri bure, watu watibiwe bure mahospitalini, utaondoa Zaka watu wasali bure misikitini na makanisani, bure! bure! bure!

Kwa nini iwe bure? Mtu yeyote mwenye akili timamu lazima ajiulize swali hili; Kwa nini bure? Ukipewa bure inamaana wewe ni wa bure. Upewe bure imekuwa Zawadi? Zawadi ndio huwa bure na sio zaidi ya hapo.

Kwa nini iwe bure? Kwa nini serikali isitengeneze mazingira ya watu kuweza kulipa ada na sio kuondoa ada. Unaondoa ada alafu waalimu wanalia mishahara, hii ni akili ya wapi asee?
Unatoa ada alafu shule haina maabara, na maabara zikiwepo hazina apparatus. Unatoa Ada alafu shule hazina maktaba, na kama maktaba zipo basi hazina Mkutubi, hazina vitabu zaidi ya majarida ya Fema,hii ni akili ya wapi ndugu zangu. Unatoa ada alafu shule haina madawati, hii imekaaje?

Alafu waliotoa ada ukiwasikiliza wanavyojieleza utabaki mdomo wazi, kuna mmoja nilimsikia akisema; tumetoa ada na elimu ni bure ili kusaidia Kaya Masikini, badala wasaidie kuutoa umasikini watu waweze kulipa ada wao wanaondoa Ada, nani alisema umasikini unaletwa na watu kulipa Ada? Oooh! unajua hawawezi kulipa ada hawa sasa hawatasoma ukiiweka" Hivi mtu anashindajwe kulipa 20,000 au 50,000 kwa mwaka? Au ndio kufundishana uvivu na kulemazana.

Haya unaondoa Ada, alafu unashindwa kuongeza mishahara ya waalimu, unafikiri watawafundisha vizuri hao wanafunzi? Elimu ya bure huzalisha wanafunzi wa bure vichwa vikiwa bure kabisa.
Haya usiongeze mishahara ya waalimu, basi kuwepo na Posho, napo hakuna. Unatoa Ada alafu walimu haumpi Posho, ajabu sana hii. Alafu matokeo yakitoka watoto wamefeli unakuwa wakwanza kuwalaumu walimu, ajabu sana hii!

Kuna Member mmoja wa Jf Anaitwa FaizaFoxy hupenda kusema, huko shule mmeenda kusomea ujinga. Bure huzalisha ujinga ujinga. Sio ajabu vijana wa siku hizi wengi akili zao ni bure bure, hufuatilia mambo ya bure bure, udaku udaku kwa sababu udaku hauna gharama, ni bure kabisa.

Watu walipe Ada
Serikali ifanye utafiti ione ni kiasi gani cha Ada iwekwe kwa ajili ya watu kulipia ada kwa watoto wao.

Napendekeza kwa shule ya msingi Ada iwe 20,000 kwa mwaka. Muhula wa kwanza 10,000 na muhula wa pili 10,000
Shule ya sekondari (O' Level) iwe 50,000 kwa mwaka. Muhula wa kwanza 25,000 muhula wa pili 25,000
Shule ya sekondari ya juu (A'Level) Iwe 100,000 kwa mwaka. Muhula wa kwanza 50,000, muhula wa pili 50,000
Vyuoni kubaki kama kulivyo, watu wapewe mikopo ya riba nafuu.

Sasa wewe unajijua kabisa ni fukara, alafu unajitia kuzaa kama kuku ili uonewe huruma na serikali, ajabu sana hii. Ati sina uwezo wa kusomesha lakini una uwezo wa kuzaa, ajabu sana hii. Kama unauwezo wa kuzaa basi ongeza nguvu ya kuzalisha upate pesa ya kuwahudumia watoto wako.

Mtoto wa O'level hasa nyakati za likizo hashindwi kufanya kazi akapata hiyo 50,000 kwa ajili ya kujilipia ada. Ni kuendekezana tuu, tunafundisha watoto wetu uvivu, unakuta toto ipo likizo labda ni ya mwezi wa sita, kusoma halisomi, kufanya vibarua halifanyi, kazi kukaa tuu nyumbani, kuangalia muvi, kwa nini lisione maisha ni bure, kazi kukaa vijiweni, kwa nini lisijifunze uhuni, wapo watoto ninaowajua hivi leo wamefika mpaka elimu za juu na wamefanikiwa na walikuwa wanajisomesha. Na kwa waliofeli shule kwa sasa wanamaisha yao kwani tayari wanajua kufanya kazi za vibarua.

Elimu bure huzalisha kizazi cha bure bure.

Mwanafunzi wa A' level hashindwi kuipata 100,000 kwa ajili ya ada yake. Akishamaliza kidato cha nne mwezi novemba, anakaa nyumbani zaidi ya mieiz sita, kama ni mtu wa kujishughulisha anakosaje hiyo 100,000? Lakini kwa vile wazazi ni wavivu si ajabu watoto wakikosa hiyo laki moja. Unajua mtu mvivu haoni kazi ya kufanya hata kama kazi zipo zimemzunguka. Wewe angalia hata wavivu wa nyumbani, unakuta limekaa tuu lakini vyombo vichafu, sebule chafu, nguo zake chafu, ukimuuliza huoni kazi sio ajabu akakuambia haoni. Ndivyo hata katika kazi za uzalishaji, wavivu husema hakuna kazi kwani hawazioni. Mvivu hupenda rahisi.

Serikali irudishe Ada, watu walipie Ada.

UMUHIMU WA ADA
1. Chanzo cha mapato ndani ya serikali
2. Kuongeza thamani ya elimu katika jamii
3. Kuondoa uvivu katika jamii,watu watafanya kazi kwa ajili ya kulipa ada
4. Kuongeza Ari ya kujifunza kwa wanafunzi kwani watakuwa na uchungu wa hela zinazotolewa na wazazi wao.
5. Ada inaweza kutumika kuongeza mishahara au posho kwa walimu
6. Ada inaweza kutumika kununua na kuboresha vitendea kazi na miundo mbinu ya shule
7. Ada ni sehemu ya uzazi wa mpango, kwani watu watashindwa kuzaa watoto hovyo hovyo kwa kuogopa kushindwa kulipa ada. Jamii zinazosomesha watoto bure huzaa sana tofauti na zile jamii zinazopeleka watoto shule za kulipia ada
8. Ada huongeza thamani ya mwanafunzi kwani hasomi bure bali anachangia sehemu ya kile anachofundishwa, hivyo hupunguza unyanyasaji unaofanywa na baadhi ya waalimu. Uchunguzi wangu umebaini kwamba, shule zinazotoa Ada kubwa unyanyasaji huwa ni mdogo, waalimu huwaheshimu wanafunzi, tofauti na shule wanaotoa ada ndogo. Tuliosoma shule za ada ndogo kila mmoja ataungana na mimi kuwa kuna yule mwalimu aliyekuwa anatoa maneno ya shombo akitunyanyasa enzi zile twasoma.

9. Mtoto akifukuzwa Ada, husaidia kujua ukweli kuhusu maisha, na kuachana na yale mawazo kuwa akimaliza shule atajenga ghorofa.
10. Ada hujenga mtazamo wa mtoto kuwa " hakuna kitu cha bure" kila kitu lazima ulipie
11. Ada humjengea mtoto kujiamini na kumuwajibisha mwalimu ikiwa hataingia darasani. Ni kawaida kwa wanafunzi wanaolipa Ada kubwa kumuwajibisha mwalimu mzembe asiyeingia darasani. Lakini wanaosoma bure hawana uwezo huo kwani mwalimu atawajibu kwani mnalipia ninachowagea, ninyi si mnasoma bure. Kisha mwalimu atamalizia, niingie nisiingie darasani mimi mwisho wa mwezi pesa inaingia. Lakini mwalimu hawezi thubutu kuongea hilo shudu mbele ya shule zinazotoza ada kubwa, kwani kitumbua chake kitaingia mchanga.

HASARA YA ADA
1. Baadhi ya watu wavivu waliojipa jina masikini watashindwa kupeleka watoto shule na hivyo kuwakosesha watoto haki ya elimu.

Nafikiri tumeona kuwa Faida ni nyingi kuliko hasara ambayo ni moja.

Mwisho, Serikali rudisheni Ada, achaneni na mawazo ya kivivu kivivu, mambo ya bure mara nyingi ni kwa jamii zilizobobea kwenye uvivu.
Nafahamu, wapo watu watasema kuwa mbona kuna nchi zinatoa elimu bure, hakuna nchi yoyote makini inayoweza kufanya jambo la kivivu kama hilo.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Mikumi, Morogoro
Habar naomba kuchangia
Mimi ni mmoja wa wanufaika wa elimu bure. Japo ni kwa mwaka mmoja tu 2016 nilikua form four. Advance elimu sio bure kuna ada kama kawaida. Nililipa kwa sasa nipo chuo kikuu. Ada ni laki na hamsini mbaka laki na themanini (ukichukua ada plus additional cost). Alaf kila mwanafunzi anapoanza kidato cha kwanza anapeleka vifaakulingana na wilaya anayotoka. Mfano temeke fagio la ndani na la nje. Vifaa vya shule havitoki serikalini. Pia quality of education haitegemei na ada inategemea na content ambazo zinafundishwa na userious. Kitu kingine cha muhimu hizo ada hazitoshi kufinance sekta ya elimu nchini. Sema labda kwa kiasi kidogo sana. Alaf elimu bure inasaidia watu wengi kupata access na elimu. Hayo ni mawazo yangu. Sina experience na vitu vingi bado.
 
Elimu Bure Tanzania hii au Tanzania gani ?, Unasema unampunguzia mtu huku kwenye kulipa elfu 20 alafu akifika chuo hapati mkopo (mkopo sio grant) eti unataka mzazi wake kabwela sijui aibe wapi hizo milioni kadhaa ili amsomeshe...

Kama nyie watu wenye exposure mnalishwa hizi propaganda za wanasiasa kweli we have got long to go..., na sijui kama tutafika

Pili kumbuka hakuna bure ni kodi zetu..., sasa kama unaona kuna tija kutumia kodi kununua mashangingi badala ya kuwapa elimu taifa la kesho..., (hayo pia ni mawazo)
 
Elimu Bure Tanzania hii au Tanzania gani ?, Unasema unampunguzia mtu huku kwenye kulipa elfu 20 alafu akifika chuo hapati mkopo (mkopo sio grant) eti unataka mzazi wake kabwela sijui aibe wapi hizo milioni kadhaa ili amsomeshe...

Kama nyie watu wenye exposure mnalishwa hizi propaganda za wanasiasa kweli we have got long to go..., na sijui kama tutafika

😀 😀 😀 😀 😀
Mkuu ninachokisema hapa nawatetea watu wote, kuondoa ada alafu kuruhusu michango mingine ni kuruhusu ukiritimba katika mashule.

Serikali irejeshe Ada ifahamike shule zote za serikali, mbona shule za Advance hakuna hayo mamichango zaidi ya 70000
 
Sijasema mtozwe hela nyingi😀😀😀 naona ushaanza kulia lia hapa.

Lazima mtoe ada acheni kupenda vya bure,
Kaka sijaajiriwa serikalini na wala sina huo mpango. Hela ya kulipa Ada sitoi kwa government school labda private na wala usishurutishe watu.

Hio elimu ya kulipia ada ni ipi? Hii ya kuja kujazana watu 40,000 Duce? Wakigombea nafasi ya Ukarani!?
 
Both team to score and total over 70K

Wewe unatoa Ada, alafu unasema elimu bure, wakati huku nyuma wazazi wanatoa michango zaidi ya mara tatu ya ada, na inategemea na shule na shule, huoni hapo ni janja ya nyani?

Ni bora ada iwepo, ili usimamizi uwepo kama zamani,

Pia, uzalishaji wa sekta ya elimu unategemea ada, pesa za mitihani, ili kusaidia kulipa wafanyakazi na kuboresha miundo mbinu
Sasa walimu watalilia waongezewe mishahara wakati hawazalishi chochote kweye serikali? Uliona wapi hii
 
Naona mkuu unaonesha umuhimu wa elimu an umesahau hasara za ujinga... Elimu kuwa bure kufuta ujinga! Kuna watu uzaramon huku hawajui umuhim wa elimu! Hawa kupewa bure ni sawa kuwafanya waone umuhimu kesho au after tommorow walipie.. Utakosa sabb ya kumfunga alieozesha mtoto kwa laki 2. Mm ilikosekan 70k Tu kuombea mkopo wa chuo na baba yupo mpka naeka bondi vyeti naenda kubeba zege nilipe deni [emoji57] mkuu wacha tufute ujinga kwanza
 
Kaka sijaajiriwa serikalini na wala sina huo mpango. Hela ya kulipa Ada sitoi kwa government school labda private na wala usishurutishe watu.

Hio elimu ya kulipia ada ni ipi? Hii ya kuja kujazana watu 40,000 Duce? Wakigombea nafasi ya Ukarani!?

Sishurutishi watu, bali nazungumza jambo lenye faida kwenye jamii.

Wewe mtu asome bure, unafikiri akili itaunda mtazamo gani kwenye maisha hasa katika jamii masikini?
 
Naona mkuu unaonesha umuhimu wa elimu an umesahau hasara za ujinga... Elimu kuwa bure kufuta ujinga! Kuna watu uzaramon huku hawajui umuhim wa elimu! Hawa kupewa bure ni sawa kuwafanya waone umuhimu kesho au after tommorow walipie.. Utakosa sabb ya kumfunga alieozesha mtoto kwa laki 2. Mm ilikosekan 70k Tu kuombea mkopo wa cheti na baba yupo mpka naeka bondi vyeti naenda kubeba zege nilipe deni [emoji57] mkuu wacha tufute ujinga kwanza

Asiyejua maana haambiwi maana.

Sio lazima watu wote wasome, huoni madhara ya kulazimisha watu wasome kwa sasa?

Nakuelewa Mkuu
 
Mbona kuna shule nyingi wanalipa Ada. Nenda au mpeleke mtoto wako huko akalipe Ada upate hiyo Elimu yenye thamani.
Wazazi wamesahau Ada. Ajira zenyewe hakuna unataka mtoto alipiwe Ada kutoka shule ya msingi mpaka secondary. Hizo pesa ni bora kufanyia biashara Au kujenga nyumba
 
Mbona kuna shule nyingi wanalipa Ada. Nenda au mpeleke mtoto wako huko akalipe Ada upate hiyo Elimu yenye thamani.
Wazazi wamesahau Ada. Ajira zenyewe hakuna unataka mtoto alipiwe Ada kutoka shule ya msingi mpaka secondary. Hizo pesa ni bora kufanyia biashara Au kujenga nyumba

Mkuu usipolipa Ada kuna uwezekano wa kutafuta ajira, ukilipa ada ajira zipo tuu,aidha ujiajiri au uajiriwe.

Mtu akishazoea dezo/vya bure anataka mpaka kazi apewe kirahisi tuu
 
Hakuna Mzazi anayeshindwa lipa hizo Ada bali ujinga wa Wanasiasa

Wewe umesema kweli kabisa,

Wanasiasa ndio wanapiga Propaganda kuwa watu wanashindwa kulipa 20,000 kwa mwaka.
Kumbe mtu halipi ada sio kwa sababu hana bali kwa sababu anasababu zingine kama vile anaona mtoto anapoteza muda wake shuleni, au anaona mtoto wake hapendi shule.

Umeongea ukweli kabisa
 
Back
Top Bottom