Elimu bila Nidhamu..

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Kwahiyo elimu ni mafunzo yahusianayo na nguvu za kiakili, yaani kuendeleza akili na maadili, kwa kusoma na nidhamu, ili kumfanya binadamu kutenda katika usahihi. Elimu hii ni lazima iunganishwe na maarifa ya kazi bila hivyo elimu yetu itakuwa haijakamilika.
Kwahiyo mtu aliye elimika tutampima katika matendo yake. Ina niwia vigumu kuamini na kutia akilini mtu asiye kuwa mwaminifu na mwizi kuwa ameelimika.

Tutamuona mtu aliyeelimika anavyoendesha familia yake na anavyoishi na jamii inayomzunguka. Tutampima katika nidhamu yake. Elimu bila nidhamu ni maarifa tu. Haina faida yeyote. Haiwezi kujenga kitu chochote endelevu.
Elimu bila nidhamu ni sawa sawa na mto bila kingo. Mto bila kingo hukosa mwelekeo na huleta uharibifu. Ni jinsi gani fundi seremala mwenye maarifa ya kazi na asiye na nidhamu anaweza kulifaidisha taifa? Ikiwa watu watampelekea mbao awachongee thamani kisha kuwatapeli? Mtu huyu atakuwa na faida gani kwa jamii?


Ni jinsi gani mkandarasi tuliyemfundisha maarifa ya kazi ili ajenge nyumba zetu na madaraja yetu katika ubora atalifaidisha taifa?, ikiwa akipewa kazi anachakachua? Tutapataje mwelekeo kama taifa tukiwa na watu kama hawa? Hawa watu ni sawasawa na mto bila kingo. Je sisi kama taifa tutapigaje hatua kama tutaendelea kuzalisha watu kama hawa wanaotuibia na kujiita wasomi? Kwanini tunafundisha watu wetu stadi za kazi? Je ni kwa manufaa binafsi au kwa faida ya taifa kwa ujumla?


Huu ndio umuhimu wa nidhamu katika elimu yetu. Hatutaweza kujenga kitu chochote bila nidhamu hii.

Taifa letu halitoendelea bila nidhamu kwa watu wetu. Hatutaweza kulinda na kuendeleza taasisi zetu bila nidhamu hii.
Bila nidhamu hii, watu wetu wataendelea kuyaibia mashirika na taasisi zetu ambazo ziko kwa faida ya watu wenyewe, katika misingi hii taifa letu halitoweza kupiga hatua kimaendeleo.



Note from the book: KIU ya uzalendo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom