Elewa sababu za kutaka Waziri Mwigulu ajiuzulu

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Imeandikwa na.
Abdul Nondo

Labda ili tuelewane sote twapaswa kuifahakumu *Wizara ya Mambo ya ndani* iliyo chini ya Mh.Mwigulu kama waziri.

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi ni moja ya wizara ambayo jukumu lake kubwa ni kuhakikisha nchi inakuwa na amani,kulinda usalama wa raia na mali zao na majukumu mengine.

Wizara ya mambo ya ndani,ina idara kadhaa hizi idara zipo chini ya wizara ya mambo ya ndani,idara ya *Jeshi la polisi*,jeshi la magereza,uhamiaji na idara zingine. hii ina maana usalama na amani kwa raia upo chini ya wizara hii ya mambo ya ndani.

Suala la amani kwa sasa tangu Mh.Mwigulu kuingia limekuwa tofauti si namna tulivyozoea *Watu hupigwa Risasi* ,watu hutekwa,watu kupotea na hakuna majibu ya kuridhisha kutoka kwa jeshi la polisi wala wizara yenyewe . Nape alitolewa bastola Mh.Mwigulu aliishia kuandika *Twitter* ikapotea juu kwa juu,watu wamepigwa Risasi,wametekwa,wamepotea hakuna kauli ya moja kwa moja kuwa namna gani masuala haya yanashughulikiwa jambo linalopunguza imani ya wananchi kwa jeshi letu la polisi.

Iliikuwa ni vigumu saana kuhukumu kuwa polisi hao baadhi wanafanya kazi kwa kufuata taaluma yao au laa.

Ila hii imejidhihirisha wazi kuwa polisi kadhaa sasa hawafanyi kazi kwa kufuata taaluma yao wala sheria yao jambo linalopelekea wananchi kuanza kupoteza imani .kwani polisi wamekuwa wakishuhudiwa Mara nyingi wakitumia nguvu kubwa katika hali ambayo nguvu haihitajiki.ukisoma *Sheria ya jeshi la polisi na huduma saidizi sura ya 322,kifungu cha 29* inaonesha mazingira ambayo polisi wanaruhusiwa kutumia silaha hasa.kwa kujilinda dhidi ya mwenye silaha ,au katika hali ya kuokoa wengine wasidhurike .ila sio kwa mazingira ambayo yametokea tarehe 16/2/2018 kwa Dada yetu *Aquiline Baftah Akwilini* na wala polisi hawatakiwi watumie Risasi ya moto katika maandamano ya wananchi nje ya mazingira ya sheria hiyo.

Suala hili la Dada yetu,ndio limetudhirishia kuwa kama hili limetokea kwa uzembe wa polisi wa chache hata hayo ambayo yamekuwa yakitokea ni kwasababu ya uzembe wa polisi wa chache ,Leo hii polisi kufyatua Risasi ni jambo la kawaida na bahati mbaya,sijawahi sikia neno bahati mbaya kwa jeshi ,hili neno ni taboo ila huita *Uzembe* nani wa kuangalia mienendo ya utendaji wa jeshi la polisi hao?

(Jibu)ni wizara ya mambo ya ndani

Hata kama waziri hajashiriki,au kushirikishwa.Maana ya waziri kujiuzuru kwa matendo yenye madhara kwa watu hata kama hajafanya yeye maana yake Nini ?

Tuelewe kwanza kuna kitu kinaitwa *Ministerial responsibility* (uwajibikaji wa serikali) humu kuna collective ministerial responsibility (uwajibikaji wa baraza lote pale maamuzi yao yamepelekea athari kwa jamii) pia kuna individual ministerial responsibility (hii inamuhusu waziri pale jambo linalotendeka baya katika wizara yake na lenye madhara kwa jamii hata kama hajafanya yeye ,au kushirikishwa ila limefanyika katika idara yeyote ndani ya wizara yake anatakiwa ajiuzulu,kwa kushindwa kusimamia wizara yake kikamilifu.

Maana ya waziri kujiwajibisha kwa kujiuzulu yeye badala ya waliotenda ni kwa sababu yeye ndio mkuu wa wizara na ndani ya wizara kuna idara zinazofanya mambo bila kufuata sheria na taratibu,kisiasa waziri anajua yanayofanyika hata kama hajui kisiasa ni kwamba anajua na kama anajua na ya nafanyika haya bila kufuata taratibu na sheria basi waziri huyo *hatufai* na kama hajui wala hashirikishwi basi waziri huyo *hatufai* sababu si muwajibikaji na mpelelezi kujua kipi kinafanyika ndani ya wizara yake aidha kibaya au kizuri anatakiwa ajue ili akemee matendo yote yanayokeuka sheria yanayofanywa na jeshi la polisi.,maana ya yeye kujiuzulu maana anakumbushwa awe muwajibikaji katika wizara yake hata kama hajatenda yeye.

Nendeni mkosome barua ya Rais Mstaafu ,Ally hassan Mwinyi,waziri wa mambo ya ndani 1977.Mtanielewa na mtaunga mkono katika kampeni hii ya kumshinikiza na kumtaka Mwigulu Ajiuzulu.

Kama unahitaji copy ya barua ya Rais Mwinyi(ni check whatsp no yangu chini,),ili upate jua Mwigulu hatakiwi kuendelea kuwepo ili aje waziri atakaye weza kukemea mabaya yanayofanyika chini ya wizara yake pia kuagiz mazuri yafanyike kwa usalama wa RAIA.

*Tunajikita kulinda amani badala ya haki ,wakati pasipo haki amani tuilindayo hutoweka*
 
Napata mashaka sana kama anaweza kuwa fair kwa Watanzania wenye itikadi tofauti kama yeye mwenyewe pamoja na kuwa Waziri mwenye dhamana ya kulinda usalama wetu anasimama majukwaani tena kumnadi wa Mbunge wa chama tawala kwa kuonyesha Upinzani si pahali sahihi....Likija swala la kuwathibiti upinzani kwenye maandamo ama kupora haki zao unadhani anaweza kusimamia haki ama yeye ndo ata toa go ahead...Nawaza tu mwenyewe...
 
Ninavyowafahamu viongozi wa Tanzania na viongozi wa Afrika kwa ujumla wake hawana utanaduni wa kuwajibika kwa kujiuzuru kutokana na madhara yanayowapata wananchi kutokana na uzembe Wao,wako tayari wananchi wateketee hata Kama wataishsha wote wako tayari kubaki na ng'ombe kuliko kuwajibika kwa kuachia madaraka.
 
Rais mstaafu MH. A.Mwinyi aliwahi kusema '' kila kitabu na zama zake"
Mambo ya kujiuzulu kwa kosa la mtu mwingine ilikuwa ni zama za Mwalimu Nyerere . Zimepita na sasa tuko kwenye zama mpya.
Mtu ajiuzulu kwa kosa alilofanya mwenyewe.
Polisi waliagizwa kwenda kuzuia maandamano na kiongozi wao na hawakuambiwa kwenda kuua.
Askari anaruhusiwa kujibu mashambulizi kulingana na silaha aliyonayo adui.
Kama kuna askari ameenda kinyume na kanuni na sheria katika kutekeleza majukumu yake basi sheria itachukua mkondo wake.
Mwigulu hana sababu ya kulazimishwa ajiuzulu. Ila akitaka kujiuzulu kwa utashi wake mwenyewe ni rukhusa.
 
Imeandikwa na.
Abdul Nondo

Labda ili tuelewane sote twapaswa kuifahakumu *Wizara ya Mambo ya ndani* iliyo chini ya Mh.Mwigulu kama waziri.

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi ni moja ya wizara ambayo jukumu lake kubwa ni kuhakikisha nchi inakuwa na amani,kulinda usalama wa raia na mali zao na majukumu mengine.

Wizara ya mambo ya ndani,ina idara kadhaa hizi idara zipo chini ya wizara ya mambo ya ndani,idara ya *Jeshi la polisi*,jeshi la magereza,uhamiaji na idara zingine. hii ina maana usalama na amani kwa raia upo chini ya wizara hii ya mambo ya ndani.

Suala la amani kwa sasa tangu Mh.Mwigulu kuingia limekuwa tofauti si namna tulivyozoea *Watu hupigwa Risasi* ,watu hutekwa,watu kupotea na hakuna majibu ya kuridhisha kutoka kwa jeshi la polisi wala wizara yenyewe . Nape alitolewa bastola Mh.Mwigulu aliishia kuandika *Twitter* ikapotea juu kwa juu,watu wamepigwa Risasi,wametekwa,wamepotea hakuna kauli ya moja kwa moja kuwa namna gani masuala haya yanashughulikiwa jambo linalopunguza imani ya wananchi kwa jeshi letu la polisi.

Iliikuwa ni vigumu saana kuhukumu kuwa polisi hao baadhi wanafanya kazi kwa kufuata taaluma yao au laa.

Ila hii imejidhihirisha wazi kuwa polisi kadhaa sasa hawafanyi kazi kwa kufuata taaluma yao wala sheria yao jambo linalopelekea wananchi kuanza kupoteza imani .kwani polisi wamekuwa wakishuhudiwa Mara nyingi wakitumia nguvu kubwa katika hali ambayo nguvu haihitajiki.ukisoma *Sheria ya jeshi la polisi na huduma saidizi sura ya 322,kifungu cha 29* inaonesha mazingira ambayo polisi wanaruhusiwa kutumia silaha hasa.kwa kujilinda dhidi ya mwenye silaha ,au katika hali ya kuokoa wengine wasidhurike .ila sio kwa mazingira ambayo yametokea tarehe 16/2/2018 kwa Dada yetu *Aquiline Baftah Akwilini* na wala polisi hawatakiwi watumie Risasi ya moto katika maandamano ya wananchi nje ya mazingira ya sheria hiyo.

Suala hili la Dada yetu,ndio limetudhirishia kuwa kama hili limetokea kwa uzembe wa polisi wa chache hata hayo ambayo yamekuwa yakitokea ni kwasababu ya uzembe wa polisi wa chache ,Leo hii polisi kufyatua Risasi ni jambo la kawaida na bahati mbaya,sijawahi sikia neno bahati mbaya kwa jeshi ,hili neno ni taboo ila huita *Uzembe* nani wa kuangalia mienendo ya utendaji wa jeshi la polisi hao?

(Jibu)ni wizara ya mambo ya ndani

Hata kama waziri hajashiriki,au kushirikishwa.Maana ya waziri kujiuzuru kwa matendo yenye madhara kwa watu hata kama hajafanya yeye maana yake Nini ?

Tuelewe kwanza kuna kitu kinaitwa *Ministerial responsibility* (uwajibikaji wa serikali) humu kuna collective ministerial responsibility (uwajibikaji wa baraza lote pale maamuzi yao yamepelekea athari kwa jamii) pia kuna individual ministerial responsibility (hii inamuhusu waziri pale jambo linalotendeka baya katika wizara yake na lenye madhara kwa jamii hata kama hajafanya yeye ,au kushirikishwa ila limefanyika katika idara yeyote ndani ya wizara yake anatakiwa ajiuzulu,kwa kushindwa kusimamia wizara yake kikamilifu.

Maana ya waziri kujiwajibisha kwa kujiuzulu yeye badala ya waliotenda ni kwa sababu yeye ndio mkuu wa wizara na ndani ya wizara kuna idara zinazofanya mambo bila kufuata sheria na taratibu,kisiasa waziri anajua yanayofanyika hata kama hajui kisiasa ni kwamba anajua na kama anajua na ya nafanyika haya bila kufuata taratibu na sheria basi waziri huyo *hatufai* na kama hajui wala hashirikishwi basi waziri huyo *hatufai* sababu si muwajibikaji na mpelelezi kujua kipi kinafanyika ndani ya wizara yake aidha kibaya au kizuri anatakiwa ajue ili akemee matendo yote yanayokeuka sheria yanayofanywa na jeshi la polisi.,maana ya yeye kujiuzulu maana anakumbushwa awe muwajibikaji katika wizara yake hata kama hajatenda yeye.

Nendeni mkosome barua ya Rais Mstaafu ,Ally hassan Mwinyi,waziri wa mambo ya ndani 1977.Mtanielewa na mtaunga mkono katika kampeni hii ya kumshinikiza na kumtaka Mwigulu Ajiuzulu.

Kama unahitaji copy ya barua ya Rais Mwinyi(ni check whatsp no yangu chini,),ili upate jua Mwigulu hatakiwi kuendelea kuwepo ili aje waziri atakaye weza kukemea mabaya yanayofanyika chini ya wizara yake pia kuagiz mazuri yafanyike kwa usalama wa RAIA.

*Tunajikita kulinda amani badala ya haki ,wakati pasipo haki amani tuilindayo hutoweka*
Tusubiri wahusika wakuu watangaze kuachia madaraka walio nayo.Kujiuzulu ni utashi wa mtu na sio kulazimishwa.
 
Swala si Mwigulu peke yake bali ni mamlaka nzima kuanzia juu mpaka chini
 
Mawaziri sio kama hawataki kujiezuru, ila wanashindwa , magu atawafanyizia,
 
Suala la amani kwa sasa tangu Mh.Mwigulu kuingia limekuwa tofauti si namna tulivyozoea *Watu hupigwa Risasi* ,watu hutekwa,watu kupotea na hakuna majibu ya kuridhisha kutoka kwa jeshi la polisi wala wizara yenyewe . Nape alitolewa bastola Mh.Mwigulu aliishia kuandika *Twitter* ikapotea juu kwa juu,watu wamepigwa Risasi,wametekwa,wamepotea hakuna kauli ya moja kwa moja kuwa namna gani masuala haya yanashughulikiwa jambo linalopunguza imani ya wananchi kwa jeshi letu la polisi.
Mwigulu Nchemba
 
Rais mstaafu MH. A.Mwinyi aliwahi kusema '' kila kitabu na zama zake"
Mambo ya kujiuzulu kwa kosa la mtu mwingine ilikuwa ni zama za Mwalimu Nyerere . Zimepita na sasa tuko kwenye zama mpya.
Mtu ajiuzulu kwa kosa alilofanya mwenyewe.
Polisi waliagizwa kwenda kuzuia maandamano na kiongozi wao na hawakuambiwa kwenda kuua.
Askari anaruhusiwa kujibu mashambulizi kulingana na silaha aliyonayo adui.
Kama kuna askari ameenda kinyume na kanuni na sheria katika kutekeleza majukumu yake basi sheria itachukua mkondo wake.
Mwigulu hana sababu ya kulazimishwa ajiuzulu. Ila akitaka kujiuzulu kwa utashi wake mwenyewe ni rukhusa.

Endelea kuona nwigulu hana shida mwigulu ni chui. Aliejivika ngozi ya kondoo.

Yakikukuta ndo utaelewa kwanini watu wanataka ajiuzulu. Usifikiri watu wote wanaotaka ajiuzuli ni wajinga au hawajui sura halisi ya mwigulu.
 
kwani waziri wa wizara ni nani ambae hasikii....? haoni au yeye ndio command...?
 
Back
Top Bottom