El Niño yabadili ratiba ya mitihani ya taifa

El Niño yabadili ratiba ya mitihani ya taifa

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,112
Kutokana na tahadhari ya mvua za El Nino Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limefanya marekebisho ratiba ya mitihani ya kitaifa na upimaji iliyotakiwa kufanyika Oktoba na Novemba mwaka huu.

WANU.png
Akizungumza leo Ijumaa Septemba 25, 2026 Naibu Waziri wa Elimu, Wanu Hafidh Ameir amesema uamuzi huo umefanyika ili kuhakikisha usalama wa mitihani hiyo, wanafunzi na wasimamizi.

Amesema pamoja na taarifa zilizopokewa kutoka katika mikoa kuhusu maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo, wizara imeona kuna umuhimu wa kufanya marekebisho ya ratiba ya uendeshaji wa Upimaji na Mitihani ya Taifa kwa mwaka 2026.

“Lengo la marekebisho ya ratiba ni kuhakıkisha usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi na maofisa wengine wanaohusika na uendeshaji wa mitihani, pamoja na kulinda mitihani, vifaa na nyaraka za mitihani. Iwapo mvua kubwa zitatokea mwezi Novemba 2026,” amesema.

Kwa mujibu Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohamed, Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne utafanyika Oktoba 5 na 6 badala ya Oktoba 21 na 22, huku Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili uliopaswa kufanyika Novemba 17 na 18 sasa utafanyika Oktoba 7 na 8.

Aidha, Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili uliopaswa kufanyika Novemba 2 hadi 13 sasa utafanyika kuanzia Oktoba 12 hadi 23 wakati Mtihani wa Kidato cha Nne ilioapaswa kuanza Novemba 9 hadi 27 sasa utaanza Oktoba 19 na kumalizika Novemba 6, 2026.

Ratiba Mpya ya Mtihani wa Kidato cha Nne 2026

1790330748574.png

Ratiba Mpya ya Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili 2026

1790330805656.png

Ratiba Mpya ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne 2026
1790330897891.png
​
 
TAARIFA KWA WAZAZI

Kutokana na tahadhari kuhusu uwezekano wa mvua kubwa za El Niño, Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limefanya marekebisho ya ratiba ya mitihani na upimaji wa kitaifa iliyokuwa ifanyike katika miezi ya Oktoba na Novemba 2026.

Akizungumza leo, Ijumaa, Septemba 25, 2026, Taar Wanu Hafidh Ameir, amesema uamuzi huo umefanyika kwa lengo la kuhakikisha usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi na maofisa wengine wanaohusika na uendeshaji wa mitihani.

Amesema licha ya Wizara kupokea taarifa kutoka mikoa mbalimbali kuhusu maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo, imeona umuhimu wa kufanya marekebisho ya ratiba ya uendeshaji wa Upimaji na Mitihani ya Taifa kwa mwaka 2026.

“Lengo la marekebisho ya ratiba ni kuhakikisha usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi na maofisa wengine wanaohusika na uendeshaji wa mitihani, pamoja na kulinda mitihani, vifaa na nyaraka za mitihani iwapo mvua kubwa zitatokea mwezi Novemba 2026,” amesema.

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohamed, Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne utafanyika Oktoba 5 na 6, 2026, badala ya Oktoba 21 na 22.

Aidha, Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili, uliokuwa umepangwa kufanyika Novemba 17 na 18, sasa utafanyika Oktoba 7 na 8, 2026.

Kwa upande mwingine, Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili, uliokuwa umepangwa kufanyika Novemba 2 hadi 13, sasa utafanyika kuanzia Oktoba 12 hadi 23, 2026.

Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne, ambao awali ulipangwa kuanza Novemba 9 hadi 27, sasa utaanza Oktoba 19 na kumalizika Novemba 6, 2026.
 
Hapo semen usalama wa wanafunzi hamjawahi kuzingatia usalama wa walimu
 
Wakuu, kwa El Nino ni serious ishu, msiichukulie kimzaha mzaha hasa kwa Dar na mikoani sehemu ambapo mvua inaathiri shughuli za kawaida za kila siku.

1997/8 wanajua hiki ninachozungumza, huo mwaka ilipiga mvua moja kali saana kuwahi kushuhudiwa. Na hadi sasa dalili za El Nino ni zinazidi kuongezeka kila siku.
 
Kuna shule moja iko moshi vijijini huko kata ya arusha chini/TPC yenyewe ilishazoea kukumbwa na mafuriko. Mitihani ikifanyika wakati wa mvua gari haiingii huko, inabidi wanafunzi wavushwe mito waende kufanya mitihani shule nyingine kijiji kingine ambacho hakijaathiriwa na mvua. Kiangazi huwa hakuna maji mengi na gari la mitihani hupita vizuri. Ukijitia kiherehere kuvushwa na ngalawa unaweza kudondosha nyaraka za serikali majini zikaenda na maji. Ngalawa haziaminiki kuvusha mitihani ya taifa ni hatari. Mitihani ya mkoa, wilaya na kata hiyo unavuka nayo tu haina gharama kubwa hata ikisombwa na mafuriko itachapishwa mingine. Ya taifa ni kimbembe, hata wasimamizi hawavuki huko ni hatari
 
Back
Top Bottom