Egypt kuivamia Libya?

Askari Kanzu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,598
1,233
73657374-qatari-newspaper.jpg
Cairo : Egypt | Feb 22, 2011
Gazeti moja la Qatari limemnukuu ofisa wa kijeshi wa Egypt akisema nchi yake labda italazimika kuivamia Libya ili kuwakomboa wananchi wake walioko huko. Ofisa huyo amesema hadi sasa kuna habari wamisri 13 wameuwawa katika machafuko yaendeleayo Libya kufuatia shinikizo la walibya kumng'oa Gadaffi madarakani.

Chanzo hicho kimesema uamuzi huo wa Egypt pia unafuatia matamshi ya mtoto wa Gadaffi kwamba nchi ya Egypt imeshiriki katika kuhamasisha vuguvugu la kimapinduzi ambalo limeikumba Libya.

Hadi kufikia jumatatu Egypt tayari imeshaunda kambi za kijeshi mpakani na Libya pamoja na kliniki za dharura ili kuwapokea wamisri wanaokimbia machafuko Libya. Inakadiriwa kuna wamisri zaidi 1.5 mill waishio na wafanyao kazi Libya.

Chanzo cha habari:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom