EFD: Wafanyabiashara Kariakoo wagoma!


$99.99 Each
Each[h=1]Sharp XE-A107 Business Cash Register[/h]Item: 117579 Model: XE-A107


  • 8 Pre-Programmed Departments - Easily separate product types
  • 80 Price Look-ups - For fast print speed and quiet operation
  • Clear Removeable Keytops - convenient and easy-to-clean
Niliwahi kutumia Cash register nilikuwa nazo kama mbili hivi nje ya bongo nilipojaribu ujasirimali huko, ukweli bei yake ndogo sana na ujuavyo cash register ni kubwa kuliko hizi calculator walizotuletea.

Cash Register huanzia na bei ya $ 99.00. Za bai mbaya ni zile zinazotumika kwa malipo pia ya electronic money transfer kama bank card, credit card, zinazotumika kwenye vituo vya mafuta ambazo zimeunganishwa na control ya pump za mafuta, nk ambazo huanzia na bei ya $250 and up.

Hizi walizoleta TRA hakuna tofauti na calculator zitumikazo kwa wanafunzi katika masomo ya sayansi, ingekuwa labda $50 hivi na bei halali isingezidi laki moja na nusu. Kinachoendelea ni wizi mtupu na pengine ni miradi ya vizito kuwanyonya wafanya biashara.
 
Watu wengine bwn, sasa nyie mnafikiri zile 700,000/= za kuwalipa wabunge wa bunge la katiba zinatoka wapi? Hiyo ndio habari ya mujibi kwasasa!
 
Rished Bade ni mchaga..? Mama Masele ni mchaga...? Au kwa sababu mlimuona Kitilya kakaa pale juu mkaona kila mtu ni mchaga..? Kachunguze TRA ujue nafasi nyeti zimeshikwa na watu gani then uje hapa kuongea..

Rished Bade ni Mmasai, na usimchukulie kama mfano, hajamaliza hata mwaka pale, tena mpaka sasa ni kaimu tu.

Wewe unaongelea nafasi za juu? mimi naongelea TRA yoote.

Wewe mwenyewe hapo ulipo ni mchaga, bisha!
 

Mfumo wa kulipa kodi sio mzuri, hali kadhalika tathmini ya utaratibu wa ulipaji kodi ni tata, tunaiga bila kuiga namna ya matumizi na utaratibu wa mfanyabiashara kulipa kodi hizo.

Inavyotakiwa bei ya bidhaa na faida ni mali ya mfanyabiashara. Baada ya hapo kuna asilimia kadhaa za kodi zianatakiwa baada ya hiyo gharama ya manunuzi na faida, tax hiyo anayetakiwa alipe ni mnunuzi si mfanyabiashara. Kwa mtindo unaofanywa tax Tanzania mlipaji wa kodi ni mfanyabiashara badala ya mnunuzi, ndio kosa linalifanyika kuiga kuwa na cash registers bila kujua mfumo sahihi wa matumizi ya kodi.

Nchi zinazotumia mfumo huo hasa zilizoendelea bidhaa madukani zimeandika bei yake hiyo ni pamoja na faida ambayo mfanyabiashara ameshaijumlisha kwenye bei ya bidhaa. Hivyo kama soda ni $ 1.00 na ndio bei iliyoonyeshwa, mfumo wa tax pengine ni 9% ya bei hiyo, basi mnunuzi atalipia $1.09. Uwazi huo ndio unaotakiwa, lakini kwa mfumo unaofanywa na watathmini wetu wa kibongo ni mwendo wa kibongobongo ndio unaolalamikiwa kuwaminya mno wafanyabiashara. Biashara ngumu siku hizi hawa kwa hawa wa rejareja.

Nchi ambazo tumeiga mfumo huo wa matumizi ya cash registers mfanyabiashara ni mkusanyaji wa kodi badala yakuwa mlipaji kama Tanzania. TRA wanatakiwa kuweka mfumo wa ongezeko la % za kodi baada ya bei za bidhaa zilizoko. Kosa linalofanyika ni pale TRA inapodai faida ya mfanyabiashara iwe ndio kodi ya kupa serikalini.

Faida ya mfanyabiashara hufanyiwa tathmini mara moja kwa mwaka anapofanya renewal ya leseni ya biashara yake, hivyo kuangalia net profit aliyopata ili agawana na serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…