EFD: Wafanyabiashara Kariakoo wagoma!

sio kila mashine ina kata 18%
14m hadi 3999999 mashine inakata 0%
40m hadi ..................................18%

watu wanahofu mashine ikirekodi imerekodi haifutichi karne na karne
kwa hiyo ujanja hamna
 
Mgomo huu si kuhusu mashine tu. Vile vile tunalalamikia kutopewa nafasi ktk Bunge la katiba mpya ( Wafanyabiashara hatuna wakilishi wakati hata wakulima,wavuvi,wafugaji. n.k wamewakilishwa).
 
Jk anahusikaje hapo?
Waache ujinga kulipa kodi ni lazima tatizo wameshazoea kukwepa kodi.

Kwanini asihusike wakati yeye ndo analea ujinga ndani ya serikali yake,
 
Mpaka uchaguzi mkuu ufike tutajikuta hata tukiongea au tukipumua tunatozwa kodi za kifisadi ili chama cha baba kipate pesa za kushinda.Bora punda afe mzigo wa baba ufike.

Wajinga ndio tuliwao
 

Je vyote hivyo vimepatikana tangia awali ambapo kodi zililipwa pamoja na rasilimali kibao tulizoko nazo? Kama havikupatikanika angali uongozi serikalini ni ule ule?
 

Hata mie leo kwa kweli amenifurahisha ametoa wazo la uhakika.Hebu jitahidi uwe hivyo kila siku
 
Last edited by a moderator:

acha ukabila ndugu yangu
 

Umeandika kwa kuchapia sana angekosea Dr. W. Slaa hapa kila tusi la zamani ungetukana.
 
Last edited by a moderator:
Hawataki kulipa kodi? Wao si maajenti tu wa kukusanya kodi? Hapa serikali inabidi ikae kimya, wakipitisha siku tatu iwanyanganye leseni zao za biashara kuonyesha kuwa 'the system works..'


Sio rahisi kufanya kama unavyofikiri ,tena kwa kuongozwa na akili ndogo.
 


Hakuna mgomo kariakoo ,ni wafanyabiashara wameamua kufunga maduka yao.Sijui wewe kama Serikali untaweza kuwalazimisha watu wafungue maduka ,watu wamejiajiri kariakoo hakuna alieajiriwa.Ingekuwa ni rahisi kufanyika hivyo Serikali ingalikuwa imeshachukua hatua hizo mapema sana.
 
Kukwepa kulipa kodi ni kurudisha nyuma maendeleo ya nchi..!!!


Katika taarifa zinazowasilishwa na TRA ndani ya wizara husika T.R.A huwa wanasema wamevuka lengo katika ukusanyaji wa kodi kutoka vyanzo mbali mbali(hapo mashine hamna),kwa nini sasa mashine iwe ni lazima?.Umewahi kujiuliza ni nani alikaa na kuliasisi hili suala la wafanyabiashara watumie mashine?.Je waliwashirikisha wafanyabiashara katika hili au ni kikundi cha watu wachache walikaa na kuamua jambo hili kwa manufaa yao?
 
Hii sredi imenifungua sasa. Nimegundua changamoto zifuatazo:

1. Kuna matatizo ya kiufundi na elimu duni kwa watumiaji -Nadhani hoja ya msingi hapa iwe ni kuboresha na kuimarisha utoaji elimu, maana hakuna teknolojia isiyokuwa na changamoto zake

2. Kuna tatizo la gharama za mashine kwa kuwa TRA imetoa exclusive rights kwa wakala maalum. Pengine dhamira ya hili inaweza kuwa ni nzuri (kudhibiti uchakachuzi) lakini hili linahitaji kuangaliwa upya. Udhibiti wa bei ni jambo la msingi.

3. Inaonekana mashine hizi zinawabana wafanya biashara kutokwepa kodi. Kama tatizo ni kwamba kodi imekuwa kali nadhani ni bora waweke bayana, badala ya kupindisha hoja. Maana kukwepa kodi si jambo la kizalendo hata kidogo!.

Najaribu kutafakari ukubwa wa laki saba (mara moja kwa miaka) kwa hawa wafanyabiashara wa Kariakoo..

Waungwana tulipe kodi tujenge nchi. Hao wanaoibomoa kwa kutafuna kodi zetu dawa yao ipo jikoni!
 
Ukabila ni nini, kwani uongo? nani waliojazana TRA?

Rished Bade ni mchaga..? Mama Masele ni mchaga...? Au kwa sababu mlimuona Kitilya kakaa pale juu mkaona kila mtu ni mchaga..? Kachunguze TRA ujue nafasi nyeti zimeshikwa na watu gani then uje hapa kuongea..
 
Hawataki kulipa kodi? Wao si maajenti tu wa kukusanya kodi? Hapa serikali inabidi ikae kimya, wakipitisha siku tatu iwanyanganye leseni zao za biashara kuonyesha kuwa 'the system works..'

Mfumo wa kulipa kodi sio mzuri, tunaiga bila kuiga namna ya matumizi na kulipa kodi hizo.

Inavyotakiwa bei ya bidhaa na faida ni mali ya mfanyabiashara. Baada ya hapo kuna asilimia kadhaa za kodi zianatakiwa baada ya hiyo gharama ya manunuzi na faida, tax hiyo anayetakiwa alipe ni mnunuzi si mfanyabiashara. Kwa mtindo unaofanywa tax Tanzania mlipaji wa kodi ni mfanyabiashara badala ya mnunuzi, ndio kosa linalifanyika kuiga kuwa na cash registers bila kujua mfumo sahihi wa matumizi ya kodi.

Nchi zinazotumia mfumo huo hasa zilizoendelea bidhaa madukani zimeandika bei yake hiyo ni pamoja na faida ambayo mfanyabiashara ameshaijumlisha kwenye bei ya bidhaa. Hivyo kama soda ni $ 1.00 na ndio bei iliyoonyeshwa, mfumo wa tax pengine ni 9% ya bei hiyo, basi mnunuzi atalipia $1.09. Uwazi huo ndio unaotakiwa, lakini kwa mfumo unaofanywa na watathmini wetu wa kibongo ni mwendo wa kibongobongo ndio unaolalamikiwa kuwaminya mno wafanyabiashara. Biashara ngumu siku hizi hawa kwa hawa wa rejareja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…