Eeeh Mungu, Mlinde, na Mkinge, Tundu Antipas Lissu

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
652
1,000
Kwa Tanzania, wafanyakazi wote tuna kila sababu ya kumuombea kwa Mungu, Ndg. Tundu Antipas Lissu pamoja na wana TLS wote. Hii ni kwa sababu moja kuu, kwamba, Tundu Lissu kama Rais wa chama cha wanasheria nchini—TLS, ndiyo walioona harufu ya dhuluma, ukandamizaji na unyonyaji dhidi ya wafanyakazi nchini kupitia mifuko ya jamii. Mwezi wa 5, kupitia vyombo vya habari, Tundu Lissu alinukuliwa akisema kuwa, anaipeleka ama kuiburuza serikali mahakamani kwa sababu ya kuzuia wafanyakazi kutokuchukua pesa zao ama fao la kujitoa. Wakati Tundu Lissu na wana TLS wakichukua hatua hii, wale ambao wamekuwa wakichukua ada zetu kwa kila mwezi toka mishahara yetu tena kwa asilimia mbili, yaani vyama vya wafanyakazi kupitia TUCTA, hawaoni hili, hawana habari na wala hawajali.

Ni aibu sana kuona vyama vya wafanyakazi vikikaa kimya wakati kila mwisho wa mwezi vinachukua pesa zetu toka mishahara yetu kwa asilimia mbili. Ni aibu kubwa kuona vyama vya wafanyakazi havishtuki kusikia kauli ya waziri Jenista Mhagama kwamba, FAO LA KUJITOA LAFUTWA RASMI. Eti ili watu waliopoteza ajira, ili waje kuchukua pesa zao, basi wanalazimika kuishi mpaka miaka 55 au 60. Ni nani aliye na mkataba na Mungu kwamba ataishi umri huo wa miaka 55 au 60. Je, kipindi hiki ambacho vijana wamepoteza ajira, wanaishi vipi, wanajikimu vipi kimaisha wakati pesa zao zimezuiliwa na hii mifuko ya jamii? Kodi ya nyumba, chakula, afya, vyote hivi vinahitaji pesa; kwa hali hii tunaishije. Vijana wanalizalishia vipi taifa wakati hawana matumaini kutokana na pesa zao kuzuiliwa na mifuko ya jamii? Vijana wanalizalishia vipi taifa, wakati hawana mitaji ya kufanya biashara ama kilimo kutokana na pesa zao kuzuiliwa?

Kwa dhati kabisa, nachukua nafasi hii kumuomba Mungu, amlinde, na kumkinga Tundu Lissu ili atupiganie wafanyakazi juu ya hili la fao la kujitoa. Kama wewe ni mfanyakazi na unaguswa na suala la fao la kujitoa, kwa imani yako, ungana nami kwa kusema AMENI.
Lissu.jpg
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,275
2,000
Na Alaaniwe amtegemeae mwanadam wewe badala ujiombee wewe na familia yako unahangaika na wanasiasa jipiganie mwenyewe
Kwani wewe, familia yako sio watu ni nguruwe? Mkurupuko na akili za mchanga tena! Muwe mnatafakari kwanza mnachotaka kukiandika.
 

NDUBWILA

Senior Member
Feb 7, 2017
113
225
Hivi hiyo aya unaielewa au unakurupuka tu?!

Wewe humtegemei au hukumtegemea mzazi kula, kuvaa, kusoma nk?!, Humtegemia daktari ukiumwa?, Humtegemei mwalimu kuelimika?....!!

Hovyoo!
Mkuu huyo ni wa kumsamehe hajielewi yeye mwenyewe ndio aielewe Biblia Takatifu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom