mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,588
- 11,668
Edward Ngoyai Lowasa. Bingwa wa siasa za kistaarabu, mpole anayeudhi wapinzani wake, fisadi asiye na hatia, malaika wa duniani, shetani aliyekubalika kwa Mungu. Binadamu anayeogopwa sana na kupendwa sana kwa wakati huohuo.
Basi tu! Leo nimewaza namna mtuhumiwa huyu wa ufisadi anavyojizolea wafuasi kila kukicha, kiasi kwamba watawala 'waliochaguliwa' hawapati usingizi kila wanaposikia jina lake. Nadhani kuna shida kubwa sana kwenye vichwa vya watanzania, au labda shida hiyo ipo kwenye vichwa vya watawala wao.
Je! Ni kweli kwamba uongo ulipanda lifti mwaka 2008, kisha ukweli ukapanda ngazi na kuwafikia watanzania baadae?