karamabyabato
Member
- Jan 19, 2014
- 6
- 2
Kwa nchiyetu historia itajirudia tu!, Amini .
Kwa nchiyetu historia itajirudia tu!, Amini .
ni upuuzi kufikiri kuwa hatuna viongozi tena sio sawa tu na sokoine bali kumzidi tena kwa mbali sana. tatizo ni mfumo tu uliopo.
"Juu ya suala hili la mapato kutolingana na matumizi ni kwamba tungependa kupunguza uongezaji wa wataalam wasiohitajika katika Serikali na katika mashirika ya umma mpaka hapo hali yetu ya uchumi itakapokuwa katika hali nzuri" - Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1982.Ndugu yangu kama unajua basic principles za uchumi ni kwamba hali iliyokuwa inajitokeza ni supply ilikuwa ndogo ukilinganisha na demand - ndo maana Salim Ahmed Salim alipoingia alilishughulikia hilio na tukaondokana na fedheha za kuvaa mifuko mitupu ya mbolea maarufu kama vi-sulfate. kina mama walianza kuvaa kaniki kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni- what a shame!!. nchi huru watu wanapanga misululu ya kupata sukari ya siku mbili, waTanzania wanakwenda ng'ambo na kuvamia maduka kununua dawa ya meno kuja nayo kama bidhaa ya matumizi ya nyumbani na udhalimu wa kiuchumi kibao.
unajua kwa nini moringe alisusa na kurudi kwao Monduli hadi akafuatwa arudi.
mfumo wa uchumi wa kibabe ume-prove failure popote duniani.
Mkuu kwa kizazi hichi sahau hata mfumo ukibadilika tayari umeshawaathiri iwe ni ndani ya chama tawala au upinzani ndio maana nasema itachukua miongo kadhaa kumpata mtu kama Sokoine believe me or not.
Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
Jamani ninahitaji kupata hotuba za Sokoine (R.I.P).Ziwe za. Audio, video , ama maandishi. Hotuba 15 za mwanzo kila moja nitailipia 20000. Malipo yatapitia kwa Invisible. Nichukue furusa hii kumuomba Invisible kulishughulikia hili.
Utaratibu, Tuma hotuba hiyo kwa Private message kwa kutumia account yako Ya JF kwa Invisible. Na mimi nikapata hotuba hiyo kupitia kwake. Nitakuwa nalipa kwa idadi ya hotuba nitakazopokea. Itakuwa kuwa vizuri zikipatikana za audio au video. Nimeamua zipitie kwa Invisible kwa ajiri ya kuzihakiki kama ni fake ama genuine.
Hotuba hizi nitazitoa hapa JF moja baada ya nyingine kwenye ule mwezi wa kumbukumbu ya kuzaliwa (siyo kufa ) Edward Moringe Sokoine.
Ni wakati sasa waTz kuungana kwa pamoja kumwombea Hayati SOKOINE na kuamini ipo siku atatokea mtu wa kuyatimiza yale matakwa yake ya kuifikisha Tz mahali pazuri kiuchumi na maendeleo pia AMEN
"Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi" - Edward Moringe Sokoine, 1Februari 1977
MY TAKE:
Kwa sasa sidhani kama watawala wanaweza kulitekeleza hili kwa ufanisi.