Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,794
Kuna siku ukweli utajulikana, nakumbuka kuona mabunda ya noti nyekundu yakiwa yametupwa kandoni mwa ziwa la Bernatt, semi trailer za KAUDO na KAUMA enzi hizo zilikuja kumwaga bidhaa kwenye msitu wa miquinine1983 Mwl Nyerere alienda kwny Mapumziko Butiama Nchi akaachiwa Edward moringe enzi hizo PM ndie alikuwa pia Makamu wa kwanza wa Rais!
Mwl alikatiza likizo, jamaa alikamata na kutupa ndani wale Wazee wafadhili wa TANU waliomfadhili mpaka Nyerere Mwenyewe kina Mzee Rupia, kuna watu walikuwa wanamwaga sukari, Mchele na kuna wahindi walifikia mpaka kutupa pesa baharini pale salenderbridge!
Watu wakakaa kama kamati April 12 Msouth Africa akakwepa magari yote ya Msafara akaenda kumgonga kwa "bahati mbaya" kwa mbele lakini aliekufa ni PM aliekuwa kakaa siti ya nyuma na amefungwa Mkanda! Bodyguard na Dereva wakapona kwa "bahati nzuri" japo ndio walikuwa wamekaa mbele!
Ile mtu hata Mwl alikuwa anazima sigara.