Edward Moringe Sokoine 1938-1984 | Historia na wasifu wake

Nicholaus Kilunga

JF-Expert Member
Feb 15, 2014
1,188
567
HUYU NDO EDWARD MORINGE SOKOINE SHUJAA WA WANYONGEMZALENDO WA TANGANYIKA,ADUI WA WAHUJUMU UCHUMI NA WATENDAJI WAZEMBE1/8/1938 -12/4/1984

"Ole wao wale wanaotumia nafasi zao za umma na serikali,kuiba,kuhujumu uchumi,kupokea rushwa,maana salama yao ni kudra za Mwenyezi Mungu labda nisiwajue"

Hayo ni maneno aliyowahi kuyatamka hayati kaka na mzalendo wa taifa hili shujaa Moringe Sokoine,wakati akilihutubia kwenye mkutano kikao cha NEC mjini Dodoma 12/04/1984,takribani miaka 30 iliyopita,wakati huo vita ya kupambana na suala la uzembe makazini,ulangunguzi,rushwa na biashara ya magendo,enzi hizo taifa lilikuwa la moto kila sehemu ilikuwa moto,lakini mpaka leo kauli yake inaishi,inatumika,inaamsha hali ya uzalendo na maadili ya taifa hasa wakati huu ambapo wanasiasa na serikali kwa ujumla wanaishi kinyume na misingi mikuu ya taifa hili,misingi mikuu ya chama chao na msingi mkuu wa uwajibikaji wa serikali,leo tunamkumbuka,tunakumbuka kifo cha mpendwa wetu huyo kwa yale mazuri aliyoifanyia Tanganyika kwa ujumla wake,lakini pindi tunakumbuka kumbukumbu hii tujiulize je?utakapofariki utakumbukwa kwa lipi?je viongozi wetu wanaishi kimatendo kma hayati wetu Sokoine?

ALIPOTOKA MH SOKOINE NA SAFARI YAKE NDEFU KUELEKEA KULETA TANGANYIKA TUITAKAYO.

Hayati Sokoine alizaliwa mnamo mwaka 1/8/1938 katika wilaya ya MAASAI LAND ambayo kwa sasa inafahamika kama wilaya ya Monduli,wilaya iliyoko mkoani Arusha,hayati Sokoine alipata elimu yake ya msingi Monduli,akafaulu kujiunga na shule ya sekondari Umbwe,hii ilikuwa ni kuanzia mwaka 1948 mpaka 1958,alipomaliza hapo alijiunga rasmi na chama cha TANU 1961,kisha alipata nafasi ya kwenda nchini Ujerumani mwaka 1962 mpaka 1963 kusomea mambo ya uongozi na utawala na aliporudi akateuliwa kuwa afisa mtendaji wilaya ya Maasai Land,na kutiokana na ufanyakazi wake uliotukuka wilayani Monduli wananchi hawakuwa na budi kumchagua kuwa mwakilishi wao bungeni yaani mbunge wa Monduli na ufanisi wake kiutendaji ulionekana machoni mwa watendaji wakuu wa serikali na hayati baba wa taifa Nyerere na akachaguliwa kuwa Naibu wa wizara ya mawasiliano na Usafiri hii ilikuwa mwaka 1967,kama hiyo haitoshi nyota ya kiuongozi ilizidi kumwangazia ambapo mwaka 1972 aliteuliwa kuwa waziri wa Usalama na hatimaye mwaka 1977 aliteuliwa rasmi kuwa waziri mukuu wa iliyokuwa serikali ya Tanganyika,na Muungano wa Tanzania,

Hayati sokoine alikuwa hasa mzalendo na aliependa siasa za ujamaa na hata kupelekea kumwomba baba wa taifa ruhusa ya kusisimama kwa mda kama waziri mkuu ili aende kusomea zaidi mambo ya ujamaa nchi za nje,hii ilikuwa mwaka 1981,1983 alirudi kuendelea kama waziri mkuu kuanzia wa Tanzania mpaka siku ya tarehe 12/4/1984 alipopata ajali mbaya ya kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na mkimbizi wa kisiasa kutoka nchini Afrika kusini aliyejulikana zaidi kwa jina la Dube,eneo la Wami Dakawa sasa Wami Sokoine mkoani Mororgoro,ajali iliyopelekea mauti yake palepale,kifo ambacho mpaka leo kinaacha maswali mengi na kwa bahati mbaya hakuna hata mwandishi mmoja aliefanya mahojiano na bwana Dube ambaye kwa sasa yupo nchini Afrika kusini anakula bata,,

UTATA WA KIFO CHAKE NA MASWALI MAGUMU YASIYOJIBIKA KIRAHISI

Itakumbukwa kwamba karibia viongozi wakubwa wote wa serikali waliondoka mjini Dodoma kwa ndege mara baada ya kikao cha NEC,Isipokuwa hayati Sokoine ,yeye alisema wazi ni muumini wa sera ya kilimo ni uti wa mgongo wa taifa,hivyo alipendekeza kusafiri kwa njia ya barabara ili ajionee Mashamba makubwa na maendeleo ya kilimo kwa ujumla,

2:Gari lililomgonga liliwezaje kupenya magari yote yaliyokuwa kwenye msafara wa waziri mkuu Sokoine mpaka kulifikia gari la marehemu Sokoine na kuligonga?vp trafiki walikuwa wapi mpaka lori hilo limfikie kiongozi huyo?vipi maafisa wa ulinzi ambao kazi yao ni kumlinda?

3:Katika ajali hiyo aliyefariki ni hayati Sokoine pekee,vpi kuhusu wengine kwani hakuna hata aliyejeruhiwa pakubwa

4:Aliyesababisha ajali hiyo alikuja kuachiwa huru na akarudishwa kwao A,kusini,

TETESI JUU YA UTATA WA KIFO CHAKE

Ni ukweli kwamba ukiwa kiongozi unaetimiza majukumu yako kikamilifu ni lazima utakuwa na maadui wengi na wanaokutafta kwa kila namna,hayati sokoine kutokana na vita yake dhidi ya Wahujumu uchumi,mtakumbuka wakati wa vita hiyo kuna watu walienda kuficha bidhaa mapolini na wengine kumwaga mitoni,baharini na ziwani,hali ilikuwa tete kwa wahujumu uchumi pia Walanguzi,wazee wa Magendo,wala rushwa na watendaji wazembe wa serikilini,na hapa anatajwa mzee Kawawa kuwa alikuwa miongoni mwa watu waliokemewa na maremu wakati wa kikao hicho cha mwisho mjini Dodoma,
Pia inadaiwa aliiva katika misingi ya kijamaa kupita kiasi,hali ambayo ilimtisha hata baba wa taifa
Je ni ajali ya kawaida iliyotokana na mikono na mapenzi ya Mungu?ama mkono wa binadamu?swali hili ni gumu na lina dead end

MCHANGO WAKE KWA TAIFA NA MISIMAMO NA MITAZAMO YAKE

1:Aliamini katika Haki,Usawa na uwajibikaji
2:Aliamini katika siasa za ujamaa zaidi ya siasa yeyote ile.
3:Aliamini kwamba maendeleo huja kwa watu kujituma kufanya kazi halali na bidii.
4:Aliamini katika mabadiliko chanya
5:Alikuwa mzalendo hasa kwa taifa hili
6:Aliichukia vitendo vya rushwa,hujuma,uhujumu uchumi,ulanguzi na magendo.
7:Alikuwa mtu wa vitendo na kamwe alikuwa si mtu wa kupenda kulalamikalalamika.

MCHANGO WAKE KITAIFA

1:Alikuwa mstari wa mbele enzi za vita ya Kagera pindi tunampiga Nduli Idd Amini.
2:Alianzisha vita dhidi ya uhujumu uchumi,biashara ya Ulanguzi,Magendo na aliichukia Rushwa kwa vitendo
3:Alikuwa mzalendo wa kweli wa taifa hili.
4:Aliamni katika siasa na kilimo,akiamini kilimo ni uti wa mgongo wa taifa hii ilipelekea kutotaka kupanda ndege ili ashuhudie juhudi kubwa za Watanganyika katika suala la kilimo
5:Alitunza na kutukuza tamaduni za kiafrika na utaifa wa mtanzania.

Hitimisho, leo ikiwa imepita takribani miaka 30,tangu shujaa wetu na mzalendo hayati Edward Moringe Sokoine tangu atangulie mbele ya haki, je viongozi wetu wa sasa wanaishi na kutenda kwa ajili ya manufaa ya umma kama hayati Sokoine?je?Pengo lake limezibika ama bado?wito wangu kwa wanasiasa wetu nchini wasilitumie jina la kiongozi wetu huyu na baba wa taifa kwa ajili ya kunufaika kisiasa tu?wakati hawamaanishi kwani kuchagua uovu kwenye njia ya haki ni dhambi,na sikuzote ukiwa safarini huwaulizi njia wasafiri wenzako bali wale watokao huko.

(Mungu aipe pumziko la amani nafsi yake na amlaze pema peponi hayati Sokoine)
special thanx kwa

Joseph Moses OleshangayAanyor Engai Ole Lenga na Cosmas Makune

kwa msaada wa baadhi ya taarifa nilizotumia katiaka makala hii maalumu ya kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine.


Niandikie,

Nicholaus Kilunga
kilunganicholaus@yahoo.com,0715926271,0754926271
Kibondo, Kigoma, Tanzania
 
Nilikuwa takribani miaka 5 tu ulipotangazwa na RTD kuwa umetutoka kwa ajali ya gari tarehe 12/04/1984.

Kifo chako miongoni mwa watu wako, mimi nikiwa mmoja wao bado kinaibua maswali mazito na ambayo mpaka sasa tangu nilipojiunga na Darasa la Kwanza mwaka 1986 hadi namaliza Shahada ya Uzamili (LL.M-Masters in Human Rights and Democratization in Africa), sijapata majibu ya kuridhisha na ya kutosha. Siamini sana kama tunaweza kuwa na fursa ya kujua ukweli wa kifo chako lakini cha muhimu kwetu tunaokukumbuka Daima na kukuenzi na kutaka kuishi namna ulivyoishi kwa uongozi uliotukuka nchini mwetu, ni kumshukuru Mungu kwa kukuleta duniani ili watu wote tuendelee kushuhudia kwa mataifa ya kwamba, “…binadamu mwema, kiongozi mwema katika nchi masikini kama yetu ya Tanzania inawezeka…”. Tunakukumbuka sana na tungali tunakuhitaji mno.

Hata hivyo sisi kama jamii uliyotokea, imetuchukuwa muda mrefu sana na kwa masikitiko makubwa kwamba, neno ‘HAYATI’ ilikuwa ni heshima uliyotunukiwa na serikali kutokana na uhodari wako na uchapakazi wako. Mkanganyo huu, umetokana pamoja na mambo mengine mengi, na ukosefu wa elimu miongoni mwa watu wako. Tunakukumbuka sana na tungali tunakuhitaji mno.

Hayati Edward Moringe Sokoine, natamani Mungu Akurudishe hata kwa mwaka mmoja tu uone ni kwa jinsi gani watu wako, “…tumegeuzwa watumwa katika nchi uliyoshiriki kutafuta uhuru wake, Tanzania...”. Katika kumbukumbu ya maisha yako na kukumbuka kifo cha aibu kilichokukuta wewe kama Waziri Mkuu wa Tanzania, ninaomba niyaseme yafuatayo kwa Watanzania ili sisi sote kama jamii tutafute ufumbuzi wa pamoja na wa kudumu katika kuenzi utumishi wako uliotukuka nchini mwetu. Tunakukumbuka sana na tungali tunakuhitaji mno.

HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE;

  • Tangu ulipoondoka duniani, Ardhi yetu imekuwa ya kumegwa kila kukicha na serikali kuliko ambavyo ardhi ya jamii nyingine ya kitanzania inamegwa. Tunaadhibiwa kwasababu sisi kwa mila na desturi zetu hatufanyi kitowewo wanyama pori na kutokana na hilo, tumewahifadhi na kuwatunza tukiishi kwa amani wanyamapori hao na mifugo yetu. Kwa kutumia mabavu kila siku mbuga na hifadhi zinaongezwa kwa kuchukua ardhi ya wafugaji wenzako. Hata kwa kutumia Mahakama ya Rufani chini ya Jaji Mkuu Mstaafu Nyalali, Mbuga ya Wanyamapro ya Mkomazi imechukuliwa na wafugaji kufukuzwa na kupewa fidia ya shilingi 250’000/= tu kwa familia chache eti kama fidia ya usumbufu na garama za kuwahamisha kutoka kwenye eneo lao eti kwasababu sheria za nchi zinatoa mamlaka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutwaa eneo lolote atakalo kwa manufaa ya umma. Leo hii tunapokuenzi na kukumbuka kutoweka kwako wakina mama wa kifugaji kwa maelfu wanalia na kuandamana Loliondo kwa ardhi aliyoongezewa Raia wa Kiarabu. Wanalia watu wako Simanjiro kwa kuongezwa kwa hifadhi ya Tarangire(Eneo la Mkungunero). Kilio cha wafugaji ni kila mahali tena kwa uchungu mkubwa sana. Wafugaji wanalia Morogoro, wakihamishwa na kutii amri hufukuzwa kwenye maeneo yote hata kwa kutumia jeshi la Polisi kama walivyofanyiwa Ihefu na pengine pote. Tunakukumbuka sana na tungali tunakuhitaji mno.


  • Tangu ushirikiane na Mwl. Julius Kambarage Nyerere kuwasomesha kina Mhe. Vincent Ole Kone, Mhe. James Kisota Millya (Mkuu wa Wilaya ya Longido), Mzee Ole Kambaine, Mzee Kimesera, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Mhe. Sodoweka, Mhe. Benedict Ole Nangoro, na wengine wachache kwa kutambua kuwa kihistoria waliachwa nyuma na jamii nyingine, serikali zilizofuata hazikutilia maanani mapungufu haya ya kihistoria hivyo basi, wengine kama sisi kama isingekuwa ni wazungu wachache waliotuonea huruma, tungekuwa miongoni mwa walinzi waliotapakaa mote nchini kama walinzi wa majumba na mali za matajiri katika mikoa mbalimbali ya nchi yetu. Hayati Baba yetu Sokoine, hata Zanzibar tumevuka pamoja na ukweli kwamba, maji tunayaogopa sana lakini shida humfanya binadamu yeyote apoteza utu wake na msimamo yake ya asili. Sasa tufanye nini? Tunakukumbuka sana na tungali tunakuhitaji mno.

Serikali ya wote, nchi yetu sote. Ni kwa namna gani mfugaji naye huweza kwa majivuno kabisa kusema, serikali hii ni yetu sote, nchi hii ni yetu sote na keki ya Taifa ni yetu sote?. Nani asiyefahamu ndani ya mipaka ya nchi yetu iliyobarikiwa ya kwamba, kihistoria wafugaji waliachwa nyuma kwa Nyanja mbalimbali na jamii nyingine nyingi baada ya uhuru wa Tanzania mwaka 1961? Nani hafahamu kuwa kutokana na ukosefu wa uadilifu, uzalendo kuisha, watu waovu, wabinafsi na wabaya toka makabila mbalimbali nchini mwetu huwatafuta ndugu zao ili kuwatafutia ajira, na fursa nyingine nyingi katika taasisi mbalimbali za nchi yetu? Leo vitengo fulani fulani vya serikali vimetawaliwa na jamii moja? Nani miongoni mwetu ambaye hafahamu walivyofanya waafrika ya kusini baada ya uhuru wa kweli mwaka 1994? Mzee Nelson Mandela (Madiba) baada ya kutawazwa Rais wan chi ya Afrika ya Kusini alitambua ukweli kwamba, watu weusi baada ya uchumi na nafasi nyingi kuhodhiwa na waafrika kusini weupe serikali ilikuja na SERA ya Utaifa ya “Black Economic Empowerement(BEE)”. Sera hii ililetwa mahususi ili kurekebishwa na kutatua makosa ya kihistoria miongoni mwa waafrika kusini?. Kwa lugha ya wageni wanasema, “positive discrimination”. Nani hafamu kuwa kuna ukweli usiopingika kuwa ukifanya tafti hata leo kuwa keki ya Taifa inaliwa na wachache na baadhi ya jamii nyingine ni wasindikizaji tu? Wachache wa vijana wa namna yangu waliofanikiwa kusomeshwa na wazungu hadi chuo kikuu miongoni mwa jamii yangu wamekimbilia Taasisi za Kirai (NGOs) kutokana na madhaifu makubwa niliyotaja hapo juu. Najua wengi wanajua ukweli ninaouongelea hapa lakini kutokana na uoga na kuambiwa Taifa letu halina ukabila watu wengi wanajua ukweli kwamba wafugaji ni kama wakimbizi kwenye nchi yao hivyo wazalendo wameamua kunyamazia ukweli huu na kusema, “Funika Kikombe Mwana Haramu Apite”. Tunakukumbuka sana na tungali tunakuhitaji mno.


  • Wachache miongoni mwetu ndani ya jamii yako, tunaotaka kuishi kwa mfano wako bila kuogopa na kusema ukweli ndani ya nchi yako, tunapingwa na kupigwa marungu yasiyostahili na mengine mazito sana ili mradi tunyamaze kimya na kulazimishwa pia tuseme, “funika kikombe mwanaharamu apite”. Tunakukumbuka sana na tungali tunakuhitaji mno.


  • Hayati Edward Moringe Sokoine, ulikuwa rika moja na Baba yangu mzazi na nakumbuka baada ya matangazo ya jioni ya kifo chako, kwa kuwa baba alikuwa ni mfanyabiashara wa ng’ombe alifanikiwa kuwa na radio ya mkulima, na kwa kuwa wakati fulani ulikuwa mbunge wake pia, alikufahamu na alilia sana. Mimi sikupata bahati ya kukuona kama baba yangu mzazi lakini historia na heshima uliotuachia miongoni mwa watanzania ni kubwa mno. Uliishi maisha ya kinabii, uliwapenda watu wote na ulitenda haki, ni kweli unakumbukwa kwa uongozi uliotukuka. Nami naahidi mbele ya kaburi lako, sitanyamazia maovu yote katika nchi hii ninayoijua kama nyumbani kwangu na ninaahidi kujaribu kuishi maisha yako hata kama nitakutana na pingamizi zozote za maisha ya uongozi katika uhai wa maisha yangu lakini nipo tayari pia kufa ili kutetea ukweli na kupinga kwa akili na nguvu zangu zote manyanyaso na ukiukwaji wa HAKI ndani ya Taifa langu la Tanzania, Afrika na Duniani. Tunakukumbuka sana na tungali tunakuhitaji mno. Watanzania wanakusalimia na Wanakukumbuka kwa wema ulionyesha katika uhai wa maisha yako.

Mungu Ailaze Roho Yako Baba Yetu, Kinara wetu Edward Moringe Sokoine Mahali Pema Peponi.
MUNGU ALITOA NA MUNGU ALITWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.


………………………….
James K. Millya
 
2.jpg
1.JPG



"Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu" - Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983.


"Juu ya suala hili la mapato kutolingana na matumizi ni kwamba tungependa kupunguza uongezaji wa wataalam wasiohitajika katika Serikali na katika mashirika ya umma mpaka hapo hali yetu ya uchumi itakapokuwa katika hali nzuri" - Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1982.


"Serikali inasimamia bei, lakini Serikali yetu itakwenda mpaka itasimamia bei ya mhogo, dagaa na bei ya kila kitu? Haiwezekani, vitu vingine ni lazima vizalishwe kwa wingi ili bei yenyewe iweze kujirekebisha" - Edward Moringe Sokoine, 24 Septemba 1983
"Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa" - Edward Moringe Sokoine, 4 Oktoba 1983.


"Vijana leo wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi asimuulize mwanae, 'mali hii umeipata wapi?'" - Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1983.


"Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi" - Edward Moringe Sokoine, 1Februari 1977
 
"Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote.usalama wake n wa kudra ya mungu na wananch pekee yake...'viongoz wazembe na waadilifu wahesabu siku zao labda tusiwajue.'hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu..,..' Vijana walio wengi leo wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathin hadi arobain lakin wanaitaka serikal ndio iwaulize mali hiyo wameipata wapi..hv kwa nini mzazi usimuulize mwanao mali hii umeipata wap?

--------------------

[h=1]Yakukumbukwa miaka 29 kifo cha Sokoine[/h]
Ilikuwa Jumatano ya Aprili 12, 1984 saa 11:30 jioni, siku ambayo Dar es Salaam ilinyesha mvua kutwa nzima. Wakati kipindi cha salaam cha Jioni Njema cha Redio Tanzania (RTD) wakati huo kikiwa hewani, mara matangazo yake yanakatishwa ghafla na wimbo wa taifa unapigwa.


Mara inasikika sauti iliyozoeleka ya Rais Nyerere wakati huo ikisema: "Ndugu wananchi, leo majira ya saa 10 jioni, ndugu yetu, kijana wetu na mwenzetu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine wakati akitoka Dodoma kuja Dar es Salaam, gari yake imepata ajali, amefariki dunia."


Takribani miaka 29 imepita tangu kufariki kwa, Edward Moringe Sokoine, aliyepata kuwa waziri mkuu wa Tanzania katika vipindi viwili tofauti kabla ya kufariki Aprili 12, 1984.


Sokoine alikufa baada ya kutokea ajali ya gari eneo la Wami-Dakawa, wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea mjini Dodoma alikokuwa akishiriki vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kumbukumbuka kila mwaka
Aprili 12 ya kila mwaka, taifa limekuwa likiadhimisha kumbukumbu ya kiongozi huyo kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kuendesha makongamano, midahalo, mabonanza, ibada, riadha na upandaji mlima Kilimanjaro.


Katika utawala wa hayati baba wa taifa na rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika eneo la Wami Sokoine kulijengwa nyumba moja na banda moja linalotumika kama jukwaa lakini kwa sasa majengo hayo yamechakaa, anasema msimamizi wa eneo hilo, Hamis Said Mpandachuri.


Mwananchi ilifika katika eneo hilo na kukuta mnara wa picha ya Sokoine ukiwa umepakwa rangi mpya za manjano, kijani, blue na nyeusi huku chini ya picha yake kukiwa na maneno "Alimtumikia Mungu kwa kuwatumikia watu, sauti ya watu ni sauti ya Mungu".


Mbali ya mnara huo na majengo yaliyojengwa katika utawala wa serikali ya kwanza, pia liko jengo jipya na la kisasa ambalo linaendelea kujengwa nyuma ya majengo ya zamani. Kwa mujibu wa uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero, jengo hilo ni kwa ajili ya shule ya sekondari ya Sokoine (Sokoine memorial high school), inajengwa kama sehemu ya jitihada za wilaya hiyo za kumuenzi Sokoine.


Mbali na jitihada za halmashauri hiyo, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ambacho pia kimebeba jina lake kimekuwa katika mikakati ya kuhakikisha kuwa kinamuenzi kiongozi huyo kwa kila hali. Kassim Msagati ni ofisa mawasiliano wa chuo hicho, anasema hayati, Edward Moringe Sokoine, alikuwa muhimili muhimu wa kuanzishwa wa chuo kikuu hicho cha kilimo ambacho ni chuo kikuu pekee cha kilimo cha Serikali nchini.


Aprili 12, 1984 bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo hayati Sokoine alishiriki lilipitisha sheria namba 6 ya mwaka 1984 ya kuanzishwa kwa chuo kikuu cha kilimo Morogoro. Hapo kabla chuo hicho kilikuwa ni kitivo cha kilimo cha kilimo na misitu cha chuo kikuu cha Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa Msagati, sheria hiyo iliyopitishwa na bunge ilikiidhinisha kitivo cha kilimo cha chuo kikuu cha Dar es salaam kilichokuwa Morogoro kuwa chuo kikuu na kutaka kiitwe chuo kikuu cha kilimo Morogoro.


Lakini chuo hicho kililazimika kubadilishwa jina hata kabla ya jina la awali kuanza kutumika na kuitwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA). Hii ilitokana na kifo cha kiongozi huyo, muda mfupi baada ya chuo hicho kuidhinishwa rasmi kwa sheria hiyo ambapo utekelezaji wake ulipaswa kuanza mwezi Julai, 1984, ndipo serikali ikakubali kiitwe Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo.




Kutokana na umuhimu huo, chuo hicho kinakila sababu ya kumuenzi Sokoine kwa vitendo na hatua hiyo imekuwa ikichukuliwa kwa kuhakikisha kila mwaka ifikapo Oktoba, chuo huandaa mdahalo maalum wa kumbukumbu ya Sokoine ambapo viongozi mbalimbali wa kitaifa hualikwa.


Historia yake
Kila kiongozi ana historia yake katika uongozi wa kisiasa, kijamii na ofisi za umma. Edward Moringe Sokoine inaelezwa alishawishiwa awe kiongozi.Kwa mujibu wa mzee Saiguran Kipuyo ambaye amekua pamoja na hayati Sokoine, ni kwamba hayati alishawishiwa kuingia kwenye uongozi.


"Kipindi kile alikuwepo Chifu mmoja akiitwa Edward Barnoti. Vijana tulimuona hatutendei haki wala kusimamia maslahi yetu hivyo tukaamua kumpenyezea mtu wa rika letu kama msaidizi wake," anasimulia Kipuyo


Kipuyo ambaye anasema amezaliwa kati ya mwaka 1928-1944 anaeleza kuwa vijana ndio waliokwenda kumchukua Sokoine kwa nguvu kutoka kwenye shughuli zake za kuchunga eneo la Mfereji alikoenda baada ya kumaliza elimu ya msingi katika shule ya kati ya Moringe mjini Monduli.


"Tulimlazimisha kuwa msaidizi wa chifu Mkuu wa Council ya Maasai land akimsaidia Chifu Barnoti na ilipofika kipindi cha uchaguzi wa mbunge tukamlazimisha kuchukua fomu kuchuana na mzee Barnoti, tulifanya kampeni ya chini chini hadi akashinda," anasimulia


Anasema baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge kwa mara ya kwanza mwaka 1965 akiwakilisha jimbo la Maasai Land inayojumuisha wilaya za sasa za Monduli, Simanjiro, Kiteto, Longido na Ngorongoro, Sokoine aliteuliwa kuwa waziri mdogo wa ujenzi kabla kuhamishiwa ulinzi na jeshi la kujenga taifa.


Tabia ya asili ya Sokoine
"Pamoja na Uwaziri Mkuu, Sokoine alikuwa yule yule. Alikuwa na tabia ya kipekee. Alikaa na kuzungumza na watu wa rika zote kuanzia wazee, akina mama, vijana na watoto, alitumia fursa hiyo kujua matatizo yao na kupata maoni kuhusu utatuzi kutoka kwa wahusika wenyewe," anasema Kipuyo


Waliopeleka majungu kwa Sokoine walifanikiwa?
"Alipopelekewa majungu ya mtu, alimwita anayefitiniwa na kumtaka mpika majungu kusema yote mwenzake akiwepo. Kwa tabia hii alikomesha majungu," anafafanua.


CCM na Chadema wanasemaje?
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mahojiano maalum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake wa CCM (UWT), wilaya ya Arumeru, Ester Maleko na Mwenyekiti wa baraza la vijana wa Chadema (Bavicha), mkoa wa Arusha, Ephata Nanyaro wanakiri Sokoine ni kiongozi aliyekuwa na tunu za kipekee aliyewahi kutokea nchini.


Hakuna kama Sokoine
Kwa upande wake, Nanyaro yeye anasema tangu uhuru, taifa halijawahi kupata kiongozi aina ya Sokoine na Nyerere ambao walipenda nchi na watu wao kwa dhati na kuwa tayari kujitolea nafsi zao kushughulikia matatizo yao.


Baadhi ya nukuu muhimu za Sokoine;
"Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu" - Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983


"Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi" - Edward Moringe Sokoine, 1Februari 1977.


Makala haya yameandikwa na Venance George na Peter Saramba


Chanzo: Mwananchi | April 12, 2013
 
Nguvu kazi, kila mwenye uwezo wa kufanya kazi ni lazima afanye kazi.

''Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa''.

RIP Edward Moringe Sokoine.
 
Tumeruhusu walanguzi na wahujumu uchumi kuongoza nchi, wananchi wamefikia mahali ambapo wanashindwa kutofautisha kati ya viongozi wa chama na serikali na walanguzi na wahujumu uchumi wa nchi”.
Walanguzi na wahujumu uchumi wote ni maadui wa taifa, ni lazima kuwapiga vita na kuwatokomeza waelekezwe katika shughuli za kilimo ili waweze kuishi kwa jasho lao.”
 
"Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi" - Edward Moringe Sokoine, 1Februari 1977

MY TAKE:

Kwa sasa sidhani kama watawala wanaweza kulitekeleza hili kwa ufanisi.
 
..mwandishi wa hotuba za Sokoine mnamjua??

..mara nyingi viongozi wanachukua sifa zote wakati kuna vijana wamekesha usiku mzima kuandika hotuba zao.
 
..mwandishi wa hotuba za Sokoine mnamjua??

..mara nyingi viongozi wanachukua sifa zote wakati kuna vijana wamekesha usiku mzima kuandika hotuba zao.
Kiongozi hebu ongeza basi neno hapo..Mwandishi wake alikuwa nani.?
 
ukwelikitugani,

..I dont want to speculate.

..but I hope siku moja tutamjua mwandishi wa hotuba za Sokoine alikuwa ni nani.

..hata Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa, na Mzee Kikwete,walikuwa na waandishi wao ambao mpaka leo hakuna anayetambua mchango wao.

..Senator Ted Kennedy wa USA anakumbukwa kwa hotuba yake ya 1980 "the dream shall never die." lakini ukweli ni kwamba maneno hayo yaliandikwa na speech writer anayeitwa Bob Shrum.
 
Last edited by a moderator:
safi sana SOKOINE...haya ndiyo majembe Tanzania iliyoyapoteza kwa kipindi cha muda mrefu sana.........
 
Edward Moringe Sokoine alikuwa Waziri Mkuu wa aina yake nchini akishika wadhifa huo mara mbili ktk vpnd tofauti.Uongozi wake ulikuwa mfano kutokana na uadilifu wake,ufuatiliaji wake kwa viongoz huku akikemea rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma.Namkumbuka kwa mambo mawili makubwa kwangu mim.

1.Alipokuwa kwenye ziara zake za kikazi wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani alipita shule moja ya msing alikuta wanafunzi wamemsubir tang asbh na muda huo ilikuwa saa tisa,akiwa na msafara wake akauliza "Hivi watoto hawa wamenisubiri tang saa ngap?akajibiwa tang asbh.Akuliza "Wameshakula?" hakupata jibu.Akasema mimi narejea dar na hvyo kila m2 akale kwake,hiki chakula wapeni watoto wale.

2.Alikataa kuitwa mheshimiwa yeye na Mwalimu na walipenda kuitwa ndugu.Wakiamini kama kuna mh. pia kutakuwa na mdharauliwa.Nani anaweza kuwajal wanafunz kama alivyofanya yeye?Siku waheshimiwa ni weng madiwan,mwenyekiti mpaka ma baamedi.Sokoine alipinga kutukuzwa.Huyu ndio Edward Moringe Sokoine ninaemkumbuka.

Hakika hakuna kama yeye kizazi hiki.
 
Kuna watu hawajui kwamba hatu hatujawahi kupata kiongozi kama sokoine, Hata JK the 1st hakumfikia, Siku ile niliganda kabisa, nilipoteza matumaini kabisa. Kwa sasa naanza kuyaona kupitia CHADEMA. Nilijua Tanzania inaingia matatizoni, na kweli ikawa hivyo. Yule alikuwa ni mwana wa watu, mwana wa Afrika, a man of action without partiality, egoism and coruption. He was so pure, actualy I have seen non so far, live alone Tanzania, even in Africa. A man with 3 pair of shoes, three pairs of trousers and shirts, at his level. Very submissive to God. He has been my role model, ole wao CDM tutakapoingia, wajue Sokoine kaingia madarakani.
 
Nimekuwa kama pinda,machozi yametoka nikamkumbuka ole milya atawakomboa yupo chama chawanyonge tofauti na alipokuwa mwanzo!
 
Ujumbe huu umenigusa sana wamasai wananyanyasika sana ktk nichi yao utadhani watumwa lkn siku inakuja
bila kusahau sisi wasukuma tumekuwa watumwa katika ardhi yetu.upole na uungwana wetu umetuponza.Hata hivyo mwisho u karibu sana.IN GOD WE TRUST,IN CHADEMA WE BELIEVE, IN M4C WE HOPE;ONE DAY YES!
 
RIP Edward Moringe Sokoine, ulikufa mwaka mmoja baada ya kuianzisha vuta dhidi ya Wahujumu wa Uchumi, sasa hivi hiyo ndio fashion.
 
koine_moringe.jpg
"​

Tutakutana tena kwa kikao kijacho cha Bunge hapa Dodoma. Mimi ninasafiri kwa gari kwenda Dar es Salaam, nitapitia Morogoro, naamini tutaonana huko." Edward Sokoine.

HAKUNA KIONGOZI WOWOTE HAPA TANZANIA ANAYEWEZA KUMFIKIA HUYU MMASAI " NDUGU Edward Sokoine. MPAKA MWISHO WA DUNIA MUNGU IWEKE PEMA PEPONI ROHO YAKE MPENDWA KIONGOZI WETU Edward Sokoine. AMEEN.

 
Ni wakati sasa waTz kuungana kwa pamoja kumwombea Hayati SOKOINE na kuamini ipo siku atatokea mtu wa kuyatimiza yale matakwa yake ya kuifikisha Tz mahali pazuri kiuchumi na maendeleo pia AMEN
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom