* AVUNA WADHAMINI ZAIDI YA ELFU ISHIRINI NA MBILI (22,755).
* Aongozana na Wenyeviti wa Mikoa (CCM) lukuki
* Wa~NEC 6 wote wa Mkoa wa Singinda wamuunga Mkono...
Hii sasa sio mafuriko wala gharika bali ni hali inayotafsiriwa kuwa Lowassa leo Mkoani Singida kafunga kazi. Lowassa leo alipokuwa Mkoani Singida kadiriki kujivunia wadhamini zaidi ya elfu ishirini na mbili (22,755) na hii kwa mara nyingine tena kavunja rekodi yake mwenyewe aliyoiweka akiwa Mkoani Kigoma kwa kupata zaidi ya wadhamini elfu kumi na tatu....
Hii ya leo haijawahi kutokea, tokea tupate Uhuru wa nchi hii wamesikika wanachama wa chama hicho wakiongea na kufurahia idadi hiyo "huyu Mh (Lowassa) ni wa kipekee kwa kweli, huwezi amini kapata zaidi ya wadhamini elfu ishirini na mbili, ni maajabu manake haijawahi kutokea kabisa.. Pamoja na hilo Wa~Nec wote 6 wa Mkoa huu (Singida) leo hii wapo hapa na wamesema wazi kumuunga mkono Lowassa".... E. Kundya akiongea..
Katika zoezi hilo la kutafuta wadhamini Mkoani humu Lowassa ameongozana na wenyeviti wa Mikoa (CCM) zaidi ya 11 wakiwemo wenyeviti wa Mikoa ya Kigoma, Rukwa.... Pia yupo Mkuu wa Mkoa wa Singida....
Mytake: Hii ndio safari ya Matumaini, Mchakamchaka wa Maendeleo....