Edward Lowassa special thread


Hongera kwa kufanya utafiti wazi wa kisayansi. Kuna sehemu inahitaji kuniwekea sawa. Mantiki ya kujumlisha na kura za ukawa
 
Hesabu zingine hizi hapa,

Lowassa naurais
Ndani ya CCMkuna udicteta ndani ya democrasi ya kwao,kuna chombo kinaitwa kamati kuu(CC)chombo hiki kina maamuzi mkubwa ambayo hayaruhusiwi kukatiwa rufaamahakamani,Lowassa alilaaniwa na Nyerere kila mtu anajua kwamba hafai kuwa Raiswa Tanzania kwa ajili alijilimpikizia mali,Mangula aliitwa kwenye chama tokakijijini kwake Mtwango alikokuwa analima viazi akawa makamo wa mwenyekiti nakuwa mjumbe wa CC kwa mjibu wa wadhifa wake, aliitwa aingie kwenye chombo hichokwa kazi moja tu, KULIPIGA LULA JINA LA LOWASSA PINDI WAKIANZA KUWAJADILIWAGOMBEA WATAOCHUKUA FORM KWA TIKITI YA CCM, hiyo ni moja.
Pili raismwenyewe majuzi alisema atapenda amwachie urais kijana,siyo mzee kama yeye
Kwa mantikihiyo Lowassa hawezi kuwa rais wa inchi hii
Mwisho Lowassaanautaka urais kwa udi na uvumba hivi anataka afanye nao nini?
 
lowasa kuwa rais bora tumpe mzanzibar japo najua ni kazi ngumu sana kumuuza tanzania.
 
Hongera kwa kufanya utafiti wazi wa kisayansi. Kuna sehemu inahitaji kuniwekea sawa. Mantiki ya kujumlisha na kura za ukawa
Nimeweka kura za UKAWA, iwapo jina lake litakatwa na CCM na iwapo ataamua kukimbilia katika mwavuli wa UKAWA
 
Hayati Moringe Sokoine alimuamini ndugu yake Lowassa na ndio maana akampeleka akapigane Vita vya Idd Amin akiwa kati ya wasomi vijana toka Chuo Kikuu Dar-es-salaam, na baada ya vita kapelekwa na Nyerere UK kusomea Uchumi.

LOWASSA NA AWAMU ZOTE 4

Awamu ya 1: Imani juu ya Lowassa ipo pale pale kwa Nyerere alipomteua Katibu katika taasisi nyingi za Serikali japo alikuwa mdogo sana kiumri.

Awamu ya 2: Mzee Mwinyi alimuamini sana Lowassa na kumteuwa Mkurugenzi wa AICC japo alikuwa kijana mdogo, na pia kumpeleka katika Baraza la Mawaziri.

Awamu ya 3: Mzee Mkapa alimuamini sana Lowassa, alimpa Wizara zinazohitaji uchapaji kazi wa hali ya juu na uzalendo ulio tukuka.

Awamu ya 4: Prof Jakaya Kikwete kwa zaidi ilidhihirika imani juu ya umakini na utendaji wa Lowassa, kwani alimpa Uwaziri Mkuu wa Tanzania na hadi sasa Serikali nzima bado ina imani kubwa kwani yeye ndie Mwenyekiti katika Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

CCM: Wadhamini aliowapata Lowassa peke yake ni zaidi ya 90% ya wagombea wengine wote wa CCM.

ZANZIBAR: Sultani wa Pemba Maalim Seif pamoja kuwa ni Kiongozi wa CUF lakini aliwataka Wapemba wachukue haraka Kadi za CCM ili Lowassa apate udhamini wa kutosha Pemba, na kweli Lowassa pekee alipata Wadhamini 450 ndani ya nusu saa, wengine walisota siku kibao na kuondoka bila udhamini.

Baada ya hayo, sisi Wananchi sasa ni zamu yetu, tuleteeni Lowassa tumpe kura za Watanzania wote hadi upinzani.

By Sipano Kilimanjaro
Kiwengwa Zanzibar
 
Nimeuona uchambuzi wako. Nauheshimu sana
 
Ungejua kilichocjiri kwenye baraza la wazee ungesikitika sana,kule mwenyekiti alikuwa mzee Mwinyi ila mzee Mkapa alikitawala kikao kiasi kwamba akawa kama ndiye mwenyekiti,kwa ujumla Lowassa ameishakatwa,na wazee wamewapendekeza Sumaye na Magufuli,kwa mawazo yao ni kwamba litengenezwe zengwe ili Jaji Agustino awe rais,Sumaye makamu na Magufuli waziri mkuu,ndiyo mpango wa Mkapa huo.
 
Hesabu zingine hizi hapa:-

Lowassa,Lowassa hadi kero Kila kukicha Lowassa, Lowassa, oooo mtu mawazo yake binafsi tu anakuja na kusema ametumwa na wanainchi katika eneo lake mfano mkoa au kanda amshauri lowassa agombee Urais.

Lowassa jamani hafai, mtu anayejitajirisha kwa kutumia wadhifa wake katika utumishi wa umma hafai kuwa kiongozi kwa sababu siyo mfano wa kuigwa, yaani kuiba mali za umma siyo sifa ambayo inafaa mtu mwingine aige.

Lowassa kuwa kiongozi wa ofisi ya juu kutavutia wezi wenzie kuinajisi ofisi hiyo, yaani kama ukifuga fisi tegemea fisi wenzie kumtembelea fisi mwenzao hawezi kutembelewa na swala.Jamani Lowassa hafaiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.

Kikwete, Mangula hebu mwambieni huyo mtu kwamba hana sifa za kiti cha urais, anaweza mambo mengine na siyo urais, ni nyie mnamlealea mnamchelewesha mpeni makavu ya moja kwa moja na wala siyo mafumbo mafumbo

CC. 1. Jajaya Mrisho Kikwete
2. Jack Zoka
3. Philip Mangula
4. Abdrahiman Kinana
5. Benjamin Mkapa- Uliwakemea maaskofu ukasema na majoho yao haiwezekani serikali tatu kwa sababu baba wa taifa alikataza mbona Lowassa humkemei? Mnafiki mkubwa wee.
6. Ali Hassan Mwinyi
7. Nape Nnawiye
8. Delvis Adolf Mwamunyange
9. Ernest Hamis Mangu
10. John Komba-na unafiki wako, kama Lulu Michael kakukomba mali zote usitegemee uibukie katika kumpigia dabe fisadi Lowassa, kufa na lywako
11. Rostam Azizi –ikulu siyo pango la walanguzi unatumia mapesa yako ya wizi ili umweke Lowasaa ikulu ili uwe ndio uchochoro wako
 
Hizi Hesabu za wapi tena?
(1.)Naona umechukulia hakuna mabadiriko ya wapiga kura(hakuna vifo hakuna wapiga kura wapya hakuna ambao hawatapiga kura kwa sababu moja au nyingine)
(2.)Kwa nn umejumlisha idadi ya kura za upinzani ina maana upinzani una msupport jamaa?
ILA HONGERENI KWA MATUMAINI.
 
EL alikuwa mwanajeshi pia
 
TAARIFA KWA 4U MOVEMENT DODOMA.

Habari, Wana 4u movement mliopo Dodoma na Watanzania wote wenye mapenzi mema na Edward Lowassa tunawaasa kutovaa T-shirt zozote za 4u movement au zenye jina la Edward Lowassa katika kipindi chote cha mikutano ya Chama.

Najua na kutambua hadi jana tarehe 07/07/2015 zaidi ya wana 4u movement 3600+ plus wamewasili Dodoma lakini wingi wetu usiwe sehemu ya kuwa chanzo cha vurugu ya Aina yeyote.

Tuna Taarifa za kuaminika kuna watu wenye mpango wa kutumia T-shirt zetu za 4u movement kufanya vurugu ndani ya Mji wa Dodoma kwa makusudi ili kuiondelea sifa ya utulivu na umakini wa Movement yetu. Yeyote atakae husika kufanya fujo au vurugu zozote kwa Makusudi huku akitumia jina letu tutakuwa msatari wa Mbele kumshughulikia.

Tunawaasa na kuwaomba wana 4umvt na Watanzania wote kuwa watulivu na wavumilivu na kuwapa nafasi Wajumbe wote wa vikao vya Maamuzi kwa kutii na kufuata kanuni za chama kufanya maamuzi kwa Utulivu maana ule wakati mabadiliko uliotabiriwa na Baba wa Taifa kuwa ukifika Basi mabadiliko tutayapata ndani ya CCM na tukikosa tutayapata nje ya ccm lakini ipo nafasi kubwa sana ya kuyapata Mabadiliko haya ndani ya CCM chini ya Balozi wetu wa 4u movement Mh Edward Lowassa.

Ahsanteni

Hemedy Ally
Mratibu Taifa (National Coordinator)
@4u movement
# UTUMISHI
# UWAJIBIKAJI
# UMOJA
# UZALENDO
 
Mkitokea na mchapwe tu maana hakuna namna ya kumsaidia mtu mjinga
 

Mabadiliko yapo, vifo vipo pia. Ila katika hesabu za kisiasa hivyo vitu huviangalii sana kwa kuwa wanaokufa na wanaozaliwa hawaathiri upande mmoja. Wanakufa wa CCM na Wanakufa wa UKAWA. Wanakufa supporters wa Lowassa na wa wapinzani wake pia Wanakufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…