Vijana mbalimbali mkoani kigoma,wameapa kuwapa UKAWA ushindi katika uchaguzi mkuu ujao iwapo CCM kwa makusudi itaamua kuondoa jina la lowasa bila sababu za msingi.
Vijana hao ambao wengi ni green guard wamesema wako tayari kuwapa ushindi UKAWA,na hata kurudisha kadi ya chama chao kama haki haitatendeka kwa lowasa.Wamesema kuwa hawalazimishi lowasa awe rais wa tano ila wanataka fair game kwa kila mgombea.Namnukuu kijana lugweso"hii ni tahadhali tunatoa kwa viongozi wetu maana tetesi kuwa jina la lowasa litaondolewa hatua za awali katika mchakato wa kumpata mgombea wetu,zimepea sana,hivyo sisi kama vijana tunaomba haki itendeke,lasivyo UKAWA wajiandae kuchukia nchi,mwisho wa nukuu"
Wamebainisha kuwa wapo wagombea wana hofu na EDO,hivyo wanajaribu kutengeneza mizengwe ili jina lake liondolewe kitu ambacho wanakipinga kwa nguvu zote.
CCM ujumbe ndio huo,sauti ya wengi ni sauti ya MUNGU,kazi kwenu.