Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

Wewe ni kiongozi mwenye mamlaka,wewe ni mkweli na kiongozi mvumilivu sana,wewe ni kiongozi ambaye ana weza kuwajibika......NDANI YA CCM hawataki jamii ambayo sio yenye asili ya sahel hivyo unaweza kuwa rais wa ardhi hii ya babu yako kupitia chama kingine.Hivyo fanya mazungumzo ya kina na UKAWA ili mkomboe nchi hii.Ujio wako ukawa itawaongezea UKAWA nafasi ya kushinda.

Una nyota ya urais ni juu yako kushawishi maadui wako wawe marafiki na kujiaminisha.

Usiende katika chama ambacho ndio unakwenda kukijenga.Angalia hiyo.
 
Ukawa with Lowasa pamoja na wapambe wake imekufa. Walioko ukawa si watafuta vyeo wala maslahi. Ni watu ambao wako tayari kuumia kuona nchi hii inatoka kwenye lindi la umaskini! Lowasa is for power and money. Wapi na Wapi Akishindwa huko ccm basi aende waliko kina Malecela, Msekwa, Msuya na wengine. Huo ndo uungwana!
 
Mimi nasubiri mpango mbadala.wa mh.LOWASA

huwezi kutumia mabilioni ya fedha halafu ukawa huna mpango mbadala.
Tusubiri tuone.
 
Mimi nasubiri mpango mbadala.wa mh.LOWASA

huwezi kutumia mabilioni ya fedha halafu ukawa huna mpango mbadala.
Tusubiri tuone.

Naona wenye timu yao wameukimbia huu uzi aisee, hapo sasa ndio tutajua kama ni mtu wa watu ama vipi maana zile harambee alizokuwa anashiriki kama ni za heri basi ataendelea kushiriki huku akisaidiana na marafiki zake kuleta mabadiliko lakini asipoendelea nadhani timu yake itajua kwamba huo ulikuwa ni mpango maalumu
 
Kiongozi yyt maskini atakaechaguliwa hapo Tz ataiendesha nchi hii kifisadi tu.
Mtu mwenye Njaa ni vigumu sana kumjali masikini mpk ashibe yeye kwanza.

Hamuoni mifano ya nchi za wenzetu? Mchagueni Slaa muone balaa hapa nchini.
 
Kwisha kazi lowasa ata kugombea ubunge tena ni aibu kwake....wampe ubalozi nje akapumzike au aachane na siasa alishaonja nafas ya juu ya uwazir mkuu atulie tu
 
Kiongozi yyt maskini atakaechaguliwa hapo Tz ataiendesha nchi hii kifisadi tu.
Mtu mwenye Njaa ni vigumu sana kumjali masikini mpk ashibe yeye kwanza.

Hamuoni mifano ya nchi za wenzetu? Mchagueni Slaa muone balaa hapa nchini.

Kinyume chake, mafisadi ndio hawashibi. Hata hivyo ndugu yangu, Rais wa kwanza alikuwa maskini, angekuwa na tamaa angeweza kufanya lolote baya. Sifa inayotakiwa hapa ni roho na dhamira safi kwa taifa lako. Mengine yote mlikuwa mnadanganywa tu ili afike ikulu, yeye na maswahiba wakahomole. Tumshukuru Mungu kwa kutuepushia hilo balaa.
 
Wewe ni kiongozi mwenye mamlaka,wewe ni mkweli na kiongozi mvumilivu sana,wewe ni kiongozi ambaye ana weza kuwajibika......NDANI YA CCM hawataki jamii ambayo sio yenye asili ya sahel hivyo unaweza kuwa rais wa ardhi hii ya babu yako kupitia chama kingine.Hivyo fanya mazungumzo ya kina na UKAWA ili mkomboe nchi hii.Ujio wako ukawa itawaongezea UKAWA nafasi ya kushinda.

Una nyota ya urais ni juu yako kushawishi maadui wako wawe marafiki na kujiaminisha.

Usiende katika chama ambacho ndio unakwenda kukijenga.Angalia hiyo.

PIA mshauri akatubu kwanza, halafu atangaze na kuachana na ufisadi pamoja na kwakana maswahiba mafisadi
 
Jonh p m kaoa jirani na kwetu, nijiandae
kuwa usalama wa taifa, hahaaa nishaula
mazee
 
SAFARI ya matumaini kuelekea ikulu imewadia. Tulianza pamoja kwa umoja na tutamaliza pamoja kwa umoja. Tumaini letu ni kwa mgombea mwenye maamuzi.

Njoooni hapa wana LOWASSA tupeane update kwa yanayojili tangu sasa mpaka magogoni. TAREHE 30 mei 2015 Mr Edward Ngoyai lowasa kwa kishindo kikubwa azindua safari ya matumaini jijini arusha. Maelfu wamiminika. Mzee msukuma, kangi lugola na Mzee Kingungwe wasababisha mtikisiko taifa.

Endelea kufahamu kidogo kidogo kuhusu Lowassa

Lowassa alizaliwa tarehe 26 August 1953 mkoani Arusha. Ni waziri wa 8 wa JMT akipokea kijiti kutoka kwa Mh Fredrick Sumaye kutoka 30 Desemba 2005 hadi 7 Februari 2008 na kumuachia Mh Mizengo Pinda ambaye hadi tunavyooandika hapa ndie waziri mkuu wa JMT nae ametangaza nia ya kugombea urais kwa tiketi ya ccm mwaka 2015!


Kabla ya kuwa waziri mkuu, Lowassa alikuwa waziri wa Maji na Maendeleo ya mifugo kuanzia mwaka 2000 hadi 2005 akiwa chini ya rais Mkapa. Wizara hii alimuachia Mh Stephen Wassira baada ya yeye kuteuliwa kuwa waziri mkuu mwaka 2005. Aliingia bungeni kama mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM mnamo Novemba, 1995.

Lowassa aliwahi kuwa waziri katika ofisi ya waziri mkuu kipindi cha pili cha urais wa Mh Ali Hassan Mwinyi. Mwaka 1995 alianza harakati zake za kuwania urais wa JMT ndani ya CCM. Hakufanikiwa kupata ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM mwaka huo wa 1995 hivyo aliamua kugombea ubunge wa jimbo la monduli na kushinda kwa zaidi ya 90%.

Mnamo mwaka 1997 aliteuliwa kuwa waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais - mazingira na umaskini. Lowassa alidhihirisha uwezo wake wa kiongozi zaidi akiwa waziri wa Maji na Mifugo kuanzia mwaka 2000 hadi 2005.

Mwaka 2005 Lowassa aliacha harakati zake za kuusaka urais badala yake akaanza harakati za kumuunga mkono Mh Jakaya Kiwete kwenye mbio zake za urais. J Kikwete alikuwa ni rafiki yake wa muda mrefu sana, naye Lowassa alikubali kuwa campain manager kwenye mbio zake urais, ambapo Mh Jakaya Kikwete alishinda urais wa JMT kwa zaidi ya 80% chini ya menejimenti ya Lowassa

Elimu ya Edward Lowassa

Lowassa alipata shahada yake ya sanaa na elimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Shahada ya uzamili ya Maendeleo ya jamii kutoka Chuo Kikuu cha Bath kilichopo UK.

Elimu yake ya sekondari alipata kutoka shule ya Ilboru moja ya shule maalum kwa ajili ya wanafunzi wenye vipaji maalum darasani wakati huo; na kumalizia elimu yake ya kidato cha 5 na 6 kutoka shule ya sekondari Milambo mwaka 1977. Lowassa anapozungumzia maendeleo anajua anachozungumzia, habahatishi.

General summary kuhusu utumishi wa Lowassa


  • Mkurugenzi Mtendaji, AICC, 1989 - 1990
  • Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais (Sheria na mambo ya bunge), 1990 - 1993
  • Waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi, 1993 - 1995
  • Waziri wa nchi, makamu wa rais - mazingira na umaskini, 1997 - 2000
  • Waziri wa maji na mifugo, 2000 - 2005
  • Waziri Mkuu, 30 Desemba, 2005 - 7 Februari 2008

Alianza kuwa mbunge tangu mwaka 1990, na kuteuliwa kuwa waziri kama tulivyoonyesha hapo juu! Hadi sasa bado ni mbunge alietia nia kuwania urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2015

Kauli mbiu yake: Safari ya matumaini.

=====
update
=====

TeamLowassa imeishinda TeamJK. JK kashindwa kumuweka mgombea wake kwa namna yoyote ile!

JK kaweka mizengwe, TeamLowassa tukafanya yetu!

Hongereni TeamLowassa mmepambana sana!

Team EL mmeshinda kwa lipi wakati jamaa ndio kashakosa uraisi hivyo na kwa taarifa ndio kashapotea kwenye system na no room ya yeye kurudi tena in the future.

Sijui ushindi wenu ni kuunga mkono mtia nia mwenza na EL au ilikuwa mnapambana kwa nguvu zote na vurugu za pesa kubwa kuhakikisha El anashinda.

Polee weeeeeeeeeeeeeeeee. Mwenzeni Pombe yuleeeeeeeeeee kama chopa.
 
Back
Top Bottom