Edward Lowassa Nimewakosea nini Watanzania? (Huyu SI LOWASSA)

Edward Lowassa Nimewakosea nini Watanzania? (Huyu SI LOWASSA)

Status
Not open for further replies.
are u the EDWARD LOWASSA dat i knw?mayb im dreaming!z it dat s1 anatumia hilo jna au ni the original,kama ni wewe kweli karibu sana in jf...i think u shuld find a way to make wanatz wakuamini,u knw tc easy to 4gv bt hard to 4gt...u are warmly welcome

hana cha kufanya watanzania wamuamini.... aachane na siasa akomae na biashara zake tu!!! umeshawahi kuona wapi mtu ananyonyoa kuku halafu badae anarudishia manyoya??

he has to do what he does best, biashara!!

nani alimwambia lazima awe mwanasiasa tu??
 
Karibu kwenye jamvi mkuu, nafikiri umefanya tathmini ya kutosha kabla ya kujitosa hapa, umesema hujui kwanini watanzania wana chuki na wewe wakati huo huo unataka kuwaongoza huoni hapo unajichanganya? Mwalimu Nyerere alishawahi kukunyoshea kidole kuwa hufai kuwa kiongozi je ulishakaa chini na kutafakari kwanini alisema au aliliona hilo mapema? Na huoni sababu hizo ambazo wewe hutaki kuzijua ndiyo zinakuweka kwenye wakati mgumu kisiasa hivi leo? Ni hayo kwa leo.
 
Kama umesoma vizuri hapo juu, nimeeleza mengi, lakini kubwa nchi yetu imeingia katika siasa mbaya sana ya kuchafuana. Nakiri nina ukaribu na Mhe Chenge na Rostam na labda hii ndio sababu mmoja wetu akiwa na kashfa wote tunaingizwa humo. Lakini kama nilivyoeleza mwanzo, mimi ni kati ya watu tishio wa urais na hivyo lazima nitafanyiwa mizengwe. Ufisadi sijui nimeufanya wapi mimi, naamini mimi ni mtu safi, nina mali lakini zote naweza kuaccount nimezipata vipi, si kwa hila, za halali na Mungu wangu ndie anajua.
mkuu hujaeleza mengi, umegusia tu kidogo aisee
 
Samahani baba mimi naomba niulize hivi kuchafuliwa,kuzushiwa na kusingiziwa kuna tofauti?
 
moderators sasa mnapaswa kufanya kazi ya ziada.............. tunaomba kama mtaweza mconfim moja kwa moja na Lowasa au mtu mwingine anaueaminika aliye karibu naye ili tunapojadili tuwe na uhakika kuwa ndiye ili naye apate maoni mazuri na yatakayomsaidia katika maisha yake ya kijamii na kisiasa .................. hata mimi binafsi nasita kukubali mojak kwa moja kuwa mh lowasa ninayemfahamu ndiye yuko hewani sasa hapa JF, nijuavyo mimi, mtu wa nafasi kama yake ana njia nyingi sana anaweza kutumia kuwasiliana na umma na kwa njia hii sijajiridhisha kuwa ni kweli.................
 
Ndugu zangu,
Sikutaka kabisa kushiriki katika hii mitandao ya kijamii ambayo mimi niliiona kama ni ya kihuni, lakini nimegundua kwamba kuna vitu vya msingi sana ambavyo huwa vinajadiliwa humu na hii imenifanya niamue kushirikii.

Nimesoma michango yenu mingi sana humu, kimsingi michango mingi imejaa chuki dhidi yangu na wenzangu, huwa nashindwa kuelewa sababu hasa ya kunichukia kiasi hiki. Sitaki Malumbano na yeyote, lakini sipendi pia muendelee kuendesha propaganda za kunichafua.

Kuna watu ambao watahakikisha napotea kisiasa, sijui ni kwa maslahi ya nani, najua sababu ni kwamba na wala sijisifu, mimi ni kati ya watu ambao pamoja na matatizo ya kibinadamu niliyonayo, nina uwezo mkubwa wa kuliongoza taifa hili na hii inanifanya nionekane tishio kwa wale wote ambao wanataka kuliongoza hili taifa. Mimi sina nia ya kuwa rais wa Tanzania kwa vyovyote vile lakini ningependa kuwaongoza watanzania iwapo wananchi wangependa iwe hivyo.

Kuhusu hizi shutuma ninazopewa, nadhani ni uonevu tu kwa kuwa hakuna hata mmoja wa wale wanaonishutumu ambaye ana ushahidi wa moja kwa moja kwamba mimi nilishiriki katika kuihujumu nchi, na kwa uzalendo wangu niliamua kuuacha uwaziri mkuu, sijui watanzania wanataka nifanye nini. Najua kama binadamu nina mapungufu yangu na kila mtu anayo lakini hiki kisiwe kigezo cha kuyaacha mazuri yote niliyoifanyia nchi hii na kunisakama, kunitushi na kunidhalilisha kwa kila njia.

Naomba watanzania mnielewe kuhusu Richmond nilifanya kwa nia njema lakini bahati mbaya na kwa makosa ya kibinadamu kampuni ile ikawa feki, ni nilikubali kubeba lawama kwa kujiuzulu. Watanzania kosa langu ni nini hasa? Nihukumuni kwa haki tafadhali sio kwa propaganda.

Ya CCM na dhana ya kuendelea kuchafuana ya magamba nitaileza siku nyingine. Naomba leo niishie hapa, nitaendelea kueleza ukweli wangu popote nitakapopata fursa ikiwa ni pamoja na kupitia mitandao hii ya kijamii.

Karibu sana! kusema ukweli hii siku ya wewe kujitokeza hadharani na kuzizungumzia tuhuma mbalimbali zinazokukabili nilikuwa naisubiri kwa hamu kubwa sana, kujitokeza kwenye mtandao huu ni ujasiri mkubwa sana, maana kuna kila aina ya mawazo na challenge nyingi mno. Nasema huu ni ujasiri ambao ni watu wachache wanao, hata hivyo karibu.
 
Mimi naamini pamoja na mapungufu ya mh lowasa,pia kuna fitina dhidi yake...but first and foremost,MOD please tuthibitishie identity hii...
 
Nadhani huyu ni Orignal EL! ngoja tusubirie maana mkuu nina maswali mengi sana na muhimu! Karibu sana JF! pia hongera kwa ujasili wa kujiunga na JF!
 
Kama umesoma vizuri hapo juu, nimeeleza mengi, lakini kubwa nchi yetu imeingia katika siasa mbaya sana ya kuchafuana. Nakiri nina ukaribu na Mhe Chenge na Rostam na labda hii ndio sababu mmoja wetu akiwa na kashfa wote tunaingizwa humo. Lakini kama nilivyoeleza mwanzo, mimi ni kati ya watu tishio wa urais na hivyo lazima nitafanyiwa mizengwe. Ufisadi sijui nimeufanya wapi mimi, naamini mimi ni mtu safi, nina mali lakini zote naweza kuaccount nimezipata vipi, si kwa hila, za halali na Mungu wangu ndie anajua.

i bet to my last peny ... huyu si Edward Lowassa
 
Mh EL, nimefarijika kuona posti yako hapa jamvini, ingawa bado siamini kama kweli ni wewe halisi uliyetitokeza humu, bado nachelea kuamini. Pamoja na hayo Napongeza uwepo wa watu wenye kaliber kama ya Mh Lowasa na michango yao humu jamvini. Naukubali utendaji wako na uwezo wako katk kusimamia mambo ya msingi. Mimi binafsh pamoja na ukweli huu ju ya uwezo wako ktk uongozi bado nataka kusikia ukija na maelezo ya kutosha juu ya uhusika au kutohusika kwako kwenye kashfa mbalimbali kama ujenzi wa jengo la UVCCM, Richmond nk. Kuwa mkimya na kudharau kilio cha watanzania juu ya kufahamu waziwazi ju ya uadilifu wa kiongozi wao, bado inatia shaka kubwa na sio kuja na kutuliza umetukosea nini? Na hoja nyepesi nyepesi, juu ya tuhuma nzito. Tunahitaji zaidi ya hoja hizi. Asante sana whoever is this na karibu sana.
 
i bet to my last peny ... Huyu si edward lowassa

unaweza kudanganya watu wengi kwa muda mfupi sana!!!macho yangu yanaangalia tutajua baada ya muda mfupI!!!
 
Kama umesoma vizuri hapo juu, nimeeleza mengi, lakini kubwa nchi yetu imeingia katika siasa mbaya sana ya kuchafuana. Nakiri nina ukaribu na Mhe Chenge na Rostam na labda hii ndio sababu mmoja wetu akiwa na kashfa wote tunaingizwa humo. Lakini kama nilivyoeleza mwanzo, mimi ni kati ya watu tishio wa urais na hivyo lazima nitafanyiwa mizengwe. Ufisadi sijui nimeufanya wapi mimi, naamini mimi ni mtu safi, nina mali lakini zote naweza kuaccount nimezipata vipi, si kwa hila, za halali na Mungu wangu ndie anajua.

naanza kuhisi kuwa wewe si EL ninayemfahamu, na unazidi kumchafua kuliko ulivyofikiri kuwa unamsafisha
 
Kwa upand wangu nimefurahi sana kuona kiongozi mkubwa kama wewe kuwepo na kuamini kuwa jamii forum inaweza kufanya mabadiliko ktk jamii
Lakini pia nikupongeze kwa kuwa muwazi bila kuficha kueleza kile ulichonacho ktk moyo wako na mabacho hupendelei kuona watu wakizidi kukiongelea,

Tambuwa kuwa SIASA ni mchezo mchafu sana tena sana,kila mtu ana taka kupata nafasi ya kuiongoza nchi hii hivyo kila mbinu itatumiwa ili kuwachafuwa wale wanao onekana wananguvu zaidi yao, na hii ipo wazi
angalia uchaguzi wa FIFA,angalia maandalizi ya kugombea uraisi UFARANSA,ni vituko vya kila aina

unachotakiwa ni wewe kuendelea kusimamia na kupambana na propaganda ambazo zipo mbele yako

watanzania wa sasa si wajinga wanauwezo mkubwa sana wa kuchambuwa mambo kama unaona CCM inataka kukunyima haki yako ya kuiongoza Tanzania hilo sio tatizo ni wewe kukubali na kuelekeza malengo yako ktk chama ambacho utaona kinaweza kukupa nafasi hiyo

Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko
 
Ndugu zangu,
Sikutaka kabisa kushiriki katika hii mitandao ya kijamii ambayo mimi niliiona kama ni ya kihuni, lakini nimegundua kwamba kuna vitu vya msingi sana ambavyo huwa vinajadiliwa humu na hii imenifanya niamue kushirikii.

Nimesoma michango yenu mingi sana humu, kimsingi michango mingi imejaa chuki dhidi yangu na wenzangu, huwa nashindwa kuelewa sababu hasa ya kunichukia kiasi hiki. Sitaki Malumbano na yeyote, lakini sipendi pia muendelee kuendesha propaganda za kunichafua.

Kuna watu ambao watahakikisha napotea kisiasa, sijui ni kwa maslahi ya nani, najua sababu ni kwamba na wala sijisifu, mimi ni kati ya watu ambao pamoja na matatizo ya kibinadamu niliyonayo, nina uwezo mkubwa wa kuliongoza taifa hili na hii inanifanya nionekane tishio kwa wale wote ambao wanataka kuliongoza hili taifa. Mimi sina nia ya kuwa rais wa Tanzania kwa vyovyote vile lakini ningependa kuwaongoza watanzania iwapo wananchi wangependa iwe hivyo.

Kuhusu hizi shutuma ninazopewa, nadhani ni uonevu tu kwa kuwa hakuna hata mmoja wa wale wanaonishutumu ambaye ana ushahidi wa moja kwa moja kwamba mimi nilishiriki katika kuihujumu nchi, na kwa uzalendo wangu niliamua kuuacha uwaziri mkuu, sijui watanzania wanataka nifanye nini. Najua kama binadamu nina mapungufu yangu na kila mtu anayo lakini hiki kisiwe kigezo cha kuyaacha mazuri yote niliyoifanyia nchi hii na kunisakama, kunitushi na kunidhalilisha kwa kila njia.

Naomba watanzania mnielewe kuhusu Richmond nilifanya kwa nia njema lakini bahati mbaya na kwa makosa ya kibinadamu kampuni ile ikawa feki, ni nilikubali kubeba lawama kwa kujiuzulu. Watanzania kosa langu ni nini hasa? Nihukumuni kwa haki tafadhali sio kwa propaganda.

Ya CCM na dhana ya kuendelea kuchafuana ya magamba nitaileza siku nyingine. Naomba leo niishie hapa, nitaendelea kueleza ukweli wangu popote nitakapopata fursa ikiwa ni pamoja na kupitia mitandao hii ya kijamii.

Karibu sana mzee. Nakupongeza sana kujiunga kwenye jamvi ila sahihisha ID yako watu wataogopa kukueleza ukweli kama umeingia kwa ID yako ya public.

Chuki ni matokeo ya broken communication ambayo sasa umechukua hatua kuunga daraja. Mimi binafsi nachukia ufisadi kwa hiyo kama hilo unalo I am sorry sina choice ila kukuchukia. Kifupi madhara ya ufisadi inaa dimension kubwa isiyopimika na effect kwa maisha ya watu dhaifu wasiyotarajiwa kwa hiyo si kitu kizuri.

Kuongoza watu ni maumbile ya Mungu. Vigezo vingi, vya haki na halali vinamchagua kiongozi hata asipotaka mwenyewe kuwa kiongozi. Wenzetu nyinyi kwenye Chama Cha Magamba mnalazimisha kuwa viongozi tena kwa gharama yo yote. Hapo ndipo ugomvi unapoanzia.

Uongozi ni kuonyesha njia kwa hiyo hauna kujinufaisha ila wote tufike tunakokwenda tunufaike pamoja. Wenzetu nyinyi uongozi ni kuswaga watu wapite nyinyi msipotaka kupita ili mradi mnaweka chenu mfukoni wakati wengine wanapigika.

Iko mifano mingi.

Elimu ya shule za kata - hakuna watoto wenu huko.

TANESCO (Richmond/Dowans) hata mashine zingewashwa leo suala ni malipo ya huduma hiyo si halali na yanakwenda kwenu tu wakati nchi inakonda..

Ubunge - mnataka wabunge wenu siyo wabunge wanaotakiwa na watu.

Uchumi - sijui kama unakumbuka una mashamba mangapi na vitega uchumi vingapi. Ni kweli maisha Bora kwa kila mtanzania yanawezekana lakini ndivyo ilivyo wenzetu mnavyo kwa visingizio na kutokana na nafasi za uongozi.

Rasilimani - mlishabinafsisha kwa manufaa yenu sijui kama unaweza kusimama hadharani na kusema tumefaidika nini na mbuga ya Loliondo, Dhahabu, Almasi. Ila tunajua ndizo zinagharimia chaguzi za CCM.

Misuguano kwenye chama chenu 1. Kinatukatisha tamaa kuhusu mstakabali wa nchi yetu. 2. Mnatumia rasilimali zetu kutafuta suluhu ya matatizo yenu (Mfano muda mwingi wa shughuli za serikali mnfanya vikao vya chama chenu kwa gharama zetu).

KIFUPI NAKIRI KUWEPO KWA CHUKI DHIDI YAKO. Lakini wewe ni mtu mzima mtu hawezi kukuchukia bila sababu. Bila shaka na wewe pia huchukia au humchukia mtu kwa sababu yote ile; basi ni hivyo hivyo kwa binadamu wote.

NGUVU YAKO: Ni mchapa kazi lakini hata wauaji ni wachapa kazi. Imarisha uchapaji kazi wako kwa manufaa ya jamii kwa dhamira yenye hofu ya Mungu.

NI MKWELI: Nakumbuka ushauri wako kwa vurugu za Arusha ulikuwa Bomba naomba pia ukiri kuwa watu walikujadiri vizuri hapa JF. Lakini kwa nini ilikuwa hivyo. Wewe ulijua undani wa ule mgogoro na busara za kuusuluhisha. Wenzio (CCM) walikuwa na hila zao na wanazo hadi sasa. Matokeo yake ni chuki kuongezeka hadi leo na wewe bado uko nao hueleweki.

Ushauri Wangu.

Una kila kitu kwa sasa; na cha thamani zaidi ni utu wako. Ondoka kwenye chama cha magamba kaa pembeni fanya shughuli zako wananchi wako wanokupenda watakufuata na utawahudumia bila kuwa na migogoro na chuku za kuchonga (Watakuomba Uwaongoze). Mimi kama mwana JF nitakuheshimu sana kama utasimama pembeni mwa uozo huu. Si hivyo tu, bali kama sababu za kukuchukia kama zinatokana na huko kwenye lichama lenyu basi zitakuwa hazipo. Lakini inzi kufia kidondani si ajabu TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Mimi naamini pamoja na mapungufu ya mh lowasa,pia kuna fitina dhidi yake...but first and foremost,MOD please tuthibitishie identity hii...
Hilo halina ubishi mkuu... lakini inaniwia vigumu kusympathise na yeye wakati ni mfumo huohuo uliomfikisha hapo... SIASA ZA CCM!!!
 
Mkuu EL!
Ni wewe au mwakilishi?
Karibu sana hapa JF
Ingawa mabosi wako wa Magamba party
Walisema ni mtandao wa kile chama kingine
Hivi nini lengo lako kuu kuja humu JF?
Uungwana ni kitu cha msingi na tunaomba uwe mkweli na muwazi ktk kujibu maswali na hoja zetu...
Naamini umekuja kwa nia njema tu!
Na sisi tunakukaribisha sana....
SWALI LANGU
Nini kilichokufanya ujiunge humu JF?
Kutafuta huruma ya watz?
Kuweka mambo sawa hasa tuhuma zako?
Kusafisha njia ya kwenda magogoni?
Kukisafisha Chama cha Magamba?
 
mweshimiwa edward lowassa nafikiri ni jambo jema sana kujitokeza hapa,nakuhakikishia watanzania wote wanakuheshimu sana!!kuna baadhi ya watu ndani ya chama chako wanajitahidi sana kukumaliza!!!neno moja nataka ujue sisi watanzania tunaangalia kwa makini hatma ya hii vita!!lakini najua utatoka mshindi!!mwisho tunakutaka uwe rais wetu 2015!!thats all!

Nape yuko wapi,aanze kwa kumjibu Lowasa hapa hapa tuondoe unafiki!
Napeeeee
 
Soon pacha wake naye ataingia humu ndani, ili ile movie ya mapacha watatu ikamilike, huo mwanzo wa movie tu tusubirie movie yenyewe, anyway karibu JF pia kaa ukijua kuwa hakuna mtanzania mwenye chuki na wewe chuki ni nyie wenyewe ndio mnayoitengeneza, hivi ulipoamua kufikiria kwenda Thailand kununua mvua je ulifikiria kuwa watanzania watafurahia hicho kitendo chako, badala ya kutafuta suluhisho la kudum nyie mnawaza namna ya kuwekeza mifukoni mwenu, binafsi nilifarijika sana ulipoachia ngazi ya uwaziri mkuu, nikiamini kuna mengi mliyotuficha tukiwa kama wananchi kwa malengo ya kulinda maslahi ya chama chenu ambacho kimekosa muelekeo hadi inafikia pahala mnaanza kutafutana uchawi ndani ya chama. HAKIKA HAKUNA MTANZANIA ATAKAEKUSAHAU KWA YALE MLOTUTENDEA WEWE NA WENZAKO
 
karibu JF,kama kweli wewe ni EL. Cha msingi itunze tu afya yako. .we ni next presdent. .haina ubishi nguvu yako ni kubwa na si kweli JF unaandamwa,humu kuna mashabiki wako kupita maelezo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom