Kama kweli wewe Mheshimiwa Lowasa basi tunakukaribisha kwenye JF. Kama kiongozi ni lazima ukubali kukosolewa hapa JF. Umungu mtu hapa hakuna. Mimi naomba utueleze ni biashara gani ulioifanya katika siasa (hasa katika kile kipindi cha ujamaa kuelekea ubepari baada ya Azimio la Zanzibar) mpaka ukapata utajiri mkubwa wa kifedha ulionao? Pili kama unakiri kwamba kuidhinisha Richmond ni udhaifu wa kibinadamu mbona mpaka leo ujawaomba msamaha watanzania kwa hasara uliosababisha badala yake ukawa unasema kinachotakiwa ni cheo cha WAZIRI MKUU?