Edward Lowassa Nimewakosea nini Watanzania? (Huyu SI LOWASSA) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Edward Lowassa Nimewakosea nini Watanzania? (Huyu SI LOWASSA)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fake Lowassa, Jun 5, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Fake Lowassa

  Fake Lowassa New Member

  #1
  Jun 5, 2011
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,
  Sikutaka kabisa kushiriki katika hii mitandao ya kijamii ambayo mimi niliiona kama ni ya kihuni, lakini nimegundua kwamba kuna vitu vya msingi sana ambavyo huwa vinajadiliwa humu na hii imenifanya niamue kushirikii.

  Nimesoma michango yenu mingi sana humu, kimsingi michango mingi imejaa chuki dhidi yangu na wenzangu, huwa nashindwa kuelewa sababu hasa ya kunichukia kiasi hiki. Sitaki Malumbano na yeyote, lakini sipendi pia muendelee kuendesha propaganda za kunichafua.

  Kuna watu ambao watahakikisha napotea kisiasa, sijui ni kwa maslahi ya nani, najua sababu ni kwamba na wala sijisifu, mimi ni kati ya watu ambao pamoja na matatizo ya kibinadamu niliyonayo, nina uwezo mkubwa wa kuliongoza taifa hili na hii inanifanya nionekane tishio kwa wale wote ambao wanataka kuliongoza hili taifa. Mimi sina nia ya kuwa rais wa Tanzania kwa vyovyote vile lakini ningependa kuwaongoza watanzania iwapo wananchi wangependa iwe hivyo.

  Kuhusu hizi shutuma ninazopewa, nadhani ni uonevu tu kwa kuwa hakuna hata mmoja wa wale wanaonishutumu ambaye ana ushahidi wa moja kwa moja kwamba mimi nilishiriki katika kuihujumu nchi, na kwa uzalendo wangu niliamua kuuacha uwaziri mkuu, sijui watanzania wanataka nifanye nini. Najua kama binadamu nina mapungufu yangu na kila mtu anayo lakini hiki kisiwe kigezo cha kuyaacha mazuri yote niliyoifanyia nchi hii na kunisakama, kunitushi na kunidhalilisha kwa kila njia.

  Naomba watanzania mnielewe kuhusu Richmond nilifanya kwa nia njema lakini bahati mbaya na kwa makosa ya kibinadamu kampuni ile ikawa feki, ni nilikubali kubeba lawama kwa kujiuzulu. Watanzania kosa langu ni nini hasa? Nihukumuni kwa haki tafadhali sio kwa propaganda.

  Ya CCM na dhana ya kuendelea kuchafuana ya magamba nitaileza siku nyingine. Naomba leo niishie hapa, nitaendelea kueleza ukweli wangu popote nitakapopata fursa ikiwa ni pamoja na kupitia mitandao hii ya kijamii.
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mheshimiwa EL,...
  kwanza nakupongeza kwa kujitokeza Jamii Forums,hilo peke yake
  kwangu ni ujasiri wa ajabu,nimefurahi sana na ghafla kukuona JF,...!
  Karibu sana!

  Kwa upande wa kusema hutaki malumbano JF mheshimiwa kwa hilo pole sana
  naomba uwe tayari kuyapokea na kuya-punch malumbano yote!

  Jamii Forums ni kipimo cha uvumilivu wako!
  Uta kebehiwa,uta fanyiwa kila kitu,ila mwisho wa siku watu watataka kujua
  wewe ni nani (the inside of you)!!
   
 3. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Mmmmmhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh.......

  Tutafika tu....
   
 4. Brutus

  Brutus Senior Member

  #4
  Jun 5, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Si mchezo.. Karibu sana Ukumbini!!!!!
   
 5. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mhe Lowassa,
  Nimefarijika kukuona kwenye huu mtandao na hayo maelezo yako. Kweli unashutumiwa na mambo mengi na kama unavyokiri mwenyewe wewe ndio gamba ambalo CCM wanataka kulivua pamoja na wenzako Chenge na Rostam. Binafsi, nilikuwa napenda sana staili yako ya utendaji kazi kama kiongozi (Ukiwa Waziri Mkuu) ingawa mimi si mwananchama wala mpenzi wa CCM.
  Pole sana kwa shutuma nyingi lakini nadhani umefika muda sasa wa kusikia the other side of the story kutoka kwako pengine pamoja na wenzako.

  Ahsante.
   
 6. n

  ngwini JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mr.Lowassa karibu sana JF...na mimi swali langu kwangu ni kwann mnatajwa nyie watatu 2 kuhusu ufisadi? Je ni kweli wewe ni fisadi?
   
 7. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Huna nia ya kuwa rais wa tz kwa vyovyote vile lkn ungependa kuwaongoza watz kama wangependa iwe hivyo! what do u mean can u elaborate? yaan watz wamchague mtu asiyekuwa na nia ya urais, si utatuburuza unavyotaka wewe mkuu coz tumekutaka wenyewe pasipokuwa na ridhaa yako.
  Kuna mazuri umefanya tz hii, yapi hebu yaweke hapa jamvin ili tucompare na mabaya yako.
   
 8. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Muheshimiwa Karibu sana, hata mimi naamini una uwezo kuliko JK, jitahidi kujisafisha unaweza ukafanikiwa.
   
 9. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mweshimiwa edward lowassa nafikiri ni jambo jema sana kujitokeza hapa,nakuhakikishia watanzania wote wanakuheshimu sana!!kuna baadhi ya watu ndani ya chama chako wanajitahidi sana kukumaliza!!!neno moja nataka ujue sisi watanzania tunaangalia kwa makini hatma ya hii vita!!lakini najua utatoka mshindi!!mwisho tunakutaka uwe rais wetu 2015!!thats all!
   
 10. Moseley

  Moseley Senior Member

  #10
  Jun 5, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Provided wewe ni Lowasa kweli::

  Kwanza karibu jukwaani mheshimiwa!!

  Kuna mambo mengi yameelekezwa kwako kama mmoja wa watu waliohujumu taifa hili.. Yamesemwa mengi, kwa hiyo sisi kama wananchi tunataka kujua tatizo liko wapi hasa.. Kwa ujumla chama chako, kimekumbwa na kashfa za matumizi mabaya ya raslimali za umma..


  Na kikao kilichokaa cha NEC kikawa-point ninyi kama ndo chanzo cha matatizo hayo..


  Wewe kama Mbunge, uliewahi kuwa waziri mkuu, na mwenye uelewa wa mambo mengi ya CCM na serikali, tunaomba basi ututhibitishie, tatizo hasa liko wapi, na ni nani wanaolihujumu taifa.. Vinginevyo sisi kama wananchi tutaendelea kuamini kuwa wewe ni mmoja wa walioliltea matatizo taifa hili..


  Ndugu Mheshimiwa, haingii akilini nchi yetu yenye raslimali nyingi kiasi hiki watu bado ni maskini.. Wakati huo huo viongozi wengi wa CCM wanaishi maisha ya anasa kwa kutumia hovyo mali za umma..


  Kwa nafasi yako, tunaomba basi utujulishe, tatizo hasa ni nini mpaka nchi inaendelea kuwa maskini.. Vinginevyo tutaendelea kuamini kua wewe ni mmoja wa viongozi walioliletea matatizo taifa hili..


  Jaribu kujibu hoja zinazoelekezwa kwako moja baada ya nyingine..
   
 11. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2011
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Ama kweli UVCCM Arusha mumeamua kumbeba baba yenu. Kwa kifupi tokea Mwalimu Nyerere akukatae umekua kama una laana. Kabla sijaanza kumwaga data ambazo hazijawahi kusikika popote ikiwa ile ya kumtuma UAE Naibu Gavana,ushirikiano wako na Wasomali na safari zote za Geneva, fafanua uliposema umeshiriki Richmond.
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  karibu sana mkuu, ni huu huu uhuni ndio ulioleta mabadiliko nchi za uarabuni na vuguvugu lake linazidi kuendelea hasa kutokana na simu za kisasa kutupa access zaidi.

  hapo kwenye red mkuu ndipo ulipoanza vibaya, kwanza umesema hutaki malumbano na mtu yoyote, in JF hilo haliepukiki, kwani huku hakuna bosi wala mkuu, lakini la pili ni generalization yako... you have just fallen to the same problem.... at least ungesema baadhi ya members, kwani nafahamu kuna threads humu ziliwahi kukupamba sana tu!
  hapa sasa mkuu umechemka... Hivi wewe tangu uzaliwe hujawahi kutamani kumpoteza mtu kisiasa kweli?? i doubt, hivi wewe sio tishio kweli? i doubt, unasema huna nia ya kuwa rais lakini at the same time unasema ungependa kuwaongoza watanzania... HOW?

  :A S 100::A S 100:

  ulifanya nini tena mkuu?

  hayo ya kuchafuana si mlianza wenyewe tangu enzi zile za hizbo au ??
   
 13. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mkuu una kazi kubwa na ngumu sana mbele yako, kutufanya watanzania tukuone msafi na usie na mawaa ni kazi kubwa sana, hii inatokana na chama chako cha magamba kutujengea dhana watanzania tuwaone kuwa nyie ndio mnaorudisha nyuma na kutufanya tuishi katika umaskini mkubwa katika nchi yetu yenye utajiri uliotukuka. Leo umeweza kutueleza yaliyoko moyoni mwako sisi tulio na uwezo wa kupata internet na kuingia JF Je yule mtanzania aliyeko kijijini ambaye hajui hata mchana wa leo atakula nini utamuambiaje? Kiufupi hapo mlipofikia panatosha na kwa sasa watanzania tunahitaji mabadiliko, tunataka tupate viongozi wengine wenye uchungu na nchi yao na sio nyie mliojilimbikizia mali na kufikiria matumbo yenu tu.
  Samahani kama nitakuwa nimekukwaza ila na mimi ni mmoja wa wananchi wenye uchungu na nchi yao tusiopenda mafisadi kama nyie
   
 14. g

  graceirene Member

  #14
  Jun 5, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hongera kwa kuamua kujitokeza na walau itatupa fafanuzi za kina kuhusu hizo unazodai kuwa shutuma na propanda zinazoelekezwa kwako kwa lengo la kukuchafua.
  Karibu mbunge wa monduli
   
 15. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Pole sana muheshimiwa omba sana mungu lakini ukumbuke mungu wako ww ndio wetu ss watanzania,ukweli wa kila kitu kama unaonewa au kucngiziwa unaujua ww na upo moyoni mwako,hata watanzania wameona utendaji wako uliotukuka ulikuwa na lengo zuri tu la kujenga shule za kata,na hii ilikuwa na maana ya quality education for the people of quality ss watanzania wa hali duni tuendelee kuwa na elimu duni tunashukuru kwa hili
   
 16. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  EL, can you tell us how wealthy you are? Can you account for all your wealth?? Mradi umejitokeza humu, tafadhali jaribu kujibu maswali yetu
   
 17. Fake Lowassa

  Fake Lowassa New Member

  #17
  Jun 5, 2011
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama umesoma vizuri hapo juu, nimeeleza mengi, lakini kubwa nchi yetu imeingia katika siasa mbaya sana ya kuchafuana. Nakiri nina ukaribu na Mhe Chenge na Rostam na labda hii ndio sababu mmoja wetu akiwa na kashfa wote tunaingizwa humo. Lakini kama nilivyoeleza mwanzo, mimi ni kati ya watu tishio wa urais na hivyo lazima nitafanyiwa mizengwe. Ufisadi sijui nimeufanya wapi mimi, naamini mimi ni mtu safi, nina mali lakini zote naweza kuaccount nimezipata vipi, si kwa hila, za halali na Mungu wangu ndie anajua.
   
 18. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Karibu Mheshimiwa katika JF, Mengi tumeyasikia kuhusu wewe lakini tunashindwa kujua kulikoni, ingekuwa vizuri sana kama tungepata your side story kuhusu mambo ya Richimond, EPA na habari nyingine ili Watanzania tuwezekujua ukweli na kuchagua pumba na mchele.
   
 19. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mweshimiwa naomba tuhakikishie kama kweli ni real edward lowassa
   
 20. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  napata tabu sana kuamini kama ni wewe au kuna mtu ameingia kwa jina lako but kama ni wewe tutafahamu tu hasa kupitia majibu yako...

  karibu sana jamii forums mheshimiwa..... wewe ni miongoni mwa watu ambao jamii ina sintofahamu nyingi kuhusu kashfa, maisha na mustakabali mzima wa matumizi ya rasilimali za nchii hii. kujiunga kwako jamii forums kutatoa fursa ya kupata majibu ya maswali yote na naomba uwe mvumilivu tu kwa michango yote na maswali utakayo ulizwa kwa sababu watu humu jamvini hatupo kusifiana kama facebook na mitandao mingine.

  pili naomba majibu yawe yanatoka direct kwako na si kwa msemaji wako au secretary or anybody else. me kwa sasa hv ni hayo tu ntaruci badae kuanza kutoa duku duku langu...
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...