MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Mwanamikakati ni mtu ambaye ana uwezo mkubwa wa kupanga mikakati ambayo huzaa matokeo chanya.
Mwanasanaa ni mtu mwenye uwezo wa kutengeneza mazingira yanayovutia lakini ambayo hayana ukweli au uhalisia.
Mwaka 2010 alipewa kazi kuhakikisha Mkoa wa Arusha unabaki kuwa ngome ya CCM kwenye uchaguzi wa Madiwani na Ubunge lakini akapata ‘’kipigo cha mbwa’’ kutoka kwa Godbless Lema.
Mwaka 2012, CCM walimpa tena jukumu la mikakati na kusimamia Uchaguzi wa Arumeru Mashariki lakini akagaragazwa na kijana Joshua Nassari wa tiketi ya CHADEMA.
Mwaka 2015 akajitosa katika kinyang’anyiro cha kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM huku akitumia mbinu ya ''mafuriko ya wanachama'' kama nguzo yake lakini jina lake halikukatiza hata kwenye Kamati Kuu ya CCM.
Baada ya miezi michache, CHADEMA walimpa jukumu la kuwapeleka Ikulu lakini akaishia kulalamika kuwa ameibiwa kura wakati alisema wamwachie kazi ya kulinda kura.
Mwaka huu, CHADEMA wamempa tena kazi ya kuwanadi wagombea udiwani wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliomalizika juzi, matokeo yanaonyesha amefanikisha ushindi wa mgombea mmoja kati ya 20 waliogombea.
Huyu ni Mwanamikakati au Msanii?
Huyu katika siasa ni assset au Liability?