Mi naamini kuendelea tu kuamini kwamba kura huibwa ni kujiweka mahali pabovu zaidi. Kulisemwa hapa, wakuu wa mikakati ya wizi wa kura ndani ya ccm ni Lowasa na Kingunge, leo wapo upinzani na Lowasa ni bilionea, bado tu tuendelee kuyaamini haya?
Kuendeleza imani hizi zinawanyima wapinzani kuujua udhaifu wao wa kweli ktk chaguzi. Hata wizi ukiwepo, upinzani una madhaifu mengi sana kuweza kushinda ktk baadhi ya maeneo.
Nilishawahi kusema humu, kuna yahusishwayo na hivi vyama vya upinzani, mfano : udini, ukanda, ukabila, ubinafsi, uhitaji wa mali na vyeo, ufamilia nk.
Hata kama itakuwa ni propaganda za wapinzani wao, kushindwa kujinasua nazo ni udhaifu na ushahidi wa ukweli haya mambo. Kwanini wasijitengenezee kamkakati wa kujinasua? Yanasemwa na yanaendelea tu kuendelea, nini maana yake hapa?
Ushauri kwa cdm, kama chama kikuu cha upinzani nchini, watanzania hawahitaji demokrasia wala kelele hizo, wanataka ustawi wao tu. Tengenezeni sera nzuri, jengeni utaifa, ziuzeni na wananchi waone kweli neema itafika. Cdm hawatangazi sera siku hizi hata hakieleweki.
Watz waliamishwa ufisadi na mafisadi ndo kikwazo ktk ustawi wao, mkawabeza kuwa hakukuwa na ufisadi wala mafisadi nchini. Sasa mdandia hata mabaa yanayotokea kiasili tu, njaa na matetemeko, yakisha sijui mtasafiria yapi tena.
Mrejesheni Dr. Slaa, mumuombe radhi, fukuza Mbowe na mamluki wake wote, ondoeni ukanda, simamieni sera zenu. Mtashinda, kinyume na hapo, mtazidi kushuka hadi kife kabisa. Mtazamo.