Edward Lowassa ni mwanamikakati au mwanasanaa?

Edward Lowassa ni mwanamikakati au mwanasanaa?

Lowassa is simply a failure.
Tumempoteza Dr.Slaa kwa ajili ya huyu mwanamaigizo.
CCM watatutandika mpaka akili ziturudie.
 
Lowasa angeweza kukikuza Chama chochote proportionally kwa wakati ule anahama CCM. Tatizo kubwa la wanasiasa wetu wala si vyama ambacho wanaamua kujiunga navyo, bali huwa wanaamua kujiunga na opposition baada ya kuwa - denied some opportunities ndani ya CCM. Mrema alianza kuhangaika baada ya uteuzi wake wa mambo ya ndani kutenguliwa na kuwa waziri wa kazi. Lowasa naye alijiunga na opposition baada ya kukatwa CCM. Masha naye baada ya kukaa kijiweni bila kazi akajiunga na CDM. Ili kujenga upinzani imara inatakiwa mtu ajiuzulu madaraka yake bila matatizo na kujiunga na opposition- hii itathihirisha wazi tatizo la mtu kama huyo si cheo wala njaa bali ni kutoa ku- practise sera mbadala
Well said. Niliwaambia wenzangu wakati ule mpinzani wa kweli toka CCM kwenda opp. Ni yule atakaetofautiana na wenzake ki sera ndani ya CCM na kuamua atoke kwenda other side kwa ajili ya ku practice anachokiamini.
Kwa anaetoka CCM kwa kukosa nafasi uteuzi huyo c mwana mageuzi ni msaka nafasi na mara nyingi ni kwa faida yake binafsi kwangu mimi hafai kuaminiwa sbb anakosa agenda ya kutufanya tuambatane nae.
Hapa pia ndio niliwalaumu waliompokea kwa kukosa agenda ya kuwaambia wapiga kura ni nini kiliwafanya wampokee na tungefaidika vp. "Asset or liability?" Refer Dr Slaa.
Kuongeza kura za upinzani ni kweli ziliongezeka lkn naweza sema wapiga kura hawakuwa na agenda ya mgombea zaidi ya mgogoro uliotokea ndani ya CCM.
 
Wanasiasa wanaweza kuimba pambio kanisan huku ni mwislamu na vile vile anaweza aimba kaswida huku ni mkiristo muda mwingi anawaza kutimiza malengo yake tu na si ya watu wote
Wanasiasa Lengo Lao Kubwa Ni Kubwa Ni Kushinda Uchaguzi Tu Basi. Yuko Tayari Kukupa Nauli Ya Kwenda Kumpigia Kura Au Kukodi Chopa Na Siyo Kukuchimbia Kisima
 
Huyu jamaa anafikiri anaweza kupata urais kwa kuhonga na usanii. Sanaa aendelee nayo ila urais atauota. Aliupata rafiki yake Kikwete inatosha.
Yaa kabisa maana wewe kwasasa ndio rais
 
Sio lazima kila mtu awe rais Wa nchi hii tufike mahali tuwe wakweli Lowassa ilikuwa ni kete ya hatari sana kumpa nchi......

Mtu ambaye alishinda Makanisani na misikitini akitoa Rushwa na marafiki zake wakina Rostam Aziz ungetegemea nini kipya kutoka kwake?.............

Ni bora mabadiliko yachelewe lakini si kumpa mtu asiyeaminika kwa jamii.......

Wacha tusubiri mabadiliko ya kweli hata kama watayaona wajukuu zetu..........

Maneno yake yana ukweli mwingi ila unawaudhi na kuwaumiza kundi kubwa wasioamini kuwa giza ni usiku na jua ni mchana.Utajibiwa kwa matusi ,usijibizane nao acha waendelee kudhihirisha walivyo.
 
Huyu jamaa anafikiri anaweza kupata urais kwa kuhonga na usanii. Sanaa aendelee nayo ila urais atauota. Aliupata rafiki yake Kikwete inatosha.
Inachoshangaza badala ya kuwaombea kura madiwani alichokuwa anafanya ni kujiombea kura kama vile huo ni uchaguzi wa Rais wa Tanzania.

Inawezekana huyu jamaa bado anadhani uchaguzi mkuu 2015 haujafanyika!
 
1.Mkuu wa mkoa
2.Mkuu wa wilaya
3.Mkurugenzi wa halmashauri
4.Katibu tawala
5.Mwenyekiti wa CCM Mkoa
6.katibu CCM mkoani
7.Katibu CCM wilaya
8.Mwenyekiti CCM wilaya
9.Viongozi wa CCM vijiji na kata



umefululiza kuandika thread toka juz uchaguz mdogo ulipofanyika lakin usisahau na hayo unapotoa lawama magufuli aliwateua hao aliwaambia nendeni mkatekeleze ilani ya ccm na unajua yule bwana kuna mkurugenz alisaidia chadema kushinda kwa kutoa ushahid alitumbuliwa na ushahid wake ulikuwa sahihi
Nenda Kenya kajifunze walivyomtoa Moi.
Tatizo la wapinzani wa bongo ni vigeugeu, watu wa kulialia na kuchumia tumbo.
 
1.Mkuu wa mkoa
2.Mkuu wa wilaya
3.Mkurugenzi wa halmashauri
4.Katibu tawala
5.Mwenyekiti wa CCM Mkoa
6.katibu CCM mkoani
7.Katibu CCM wilaya
8.Mwenyekiti CCM wilaya
9.Viongozi wa CCM vijiji na kata



umefululiza kuandika thread toka juz uchaguz mdogo ulipofanyika lakin usisahau na hayo unapotoa lawama magufuli aliwateua hao aliwaambia nendeni mkatekeleze ilani ya ccm na unajua yule bwana kuna mkurugenz alisaidia chadema kushinda kwa kutoa ushahid alitumbuliwa na ushahid wake ulikuwa sahihi
Don't berate the player, blame the game!

Katiba ya Tanzania na katiba ya CCM vimempa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa madaraka ya kuteua hao viongozi.
 
Nenda Kenya kajifunze walivyomtoa Moi.
Tatizo la wapinzani wa bongo ni vigeugeu, watu wa kulialia na kuchumia tumbo.


Kuna sehemu zingine wanatolewa kwa vita usiishi kwa kukariri kila mahali na plan zao
 
Don't berate the player, blame the game!

Katiba ya Tanzania na katiba ya CCM vimempa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa madaraka ya kuteua hao viongozi.

Yea hata ushindi wa ccm unatokana na nguvu ya raisi sio maamuz ya raia hiyo ndo katiba inavyimtaka kuwa nguvu nyingi.



Kwa nini usimalizie na lugha moja tu?
 
dr.slaa alitaka mjiulize hilo swali kama ni asset au liability mwaka juzi mkamwita msaliti na kumfungulia mlango atoke.
Tukipata jibu sahihi ndipo tutajua kosa letu ili tuweze kujirekebisha.
 
Lowassa mweupe kabisa, hana jipya lolote.

Upinzani ndio byee byee

CHADEMA wamebeba mzigo wasiofahamu uzito wake!

Jamaa anaweza kutengeneza mazingira yanayovutia watu wasioweza kuangalia masuala kwa kutumia 3D thinking.

Mbaya zaidi kwa sasa anajaribu kupambana na CCM ambayo inamfahamu vizuri kutokea akiwa kijana mdogo.
 
Kila siku tukiwaambia ccm mnaiba kura hamuamini. Huyo Lowassa alipokuwa ccm alikuwa anashinda kwa kishindo, leo unatupangia matukio kibao yw udhaifu wake. Ukweli ni kuwa ukiwa ccm una nafasi ya kushinda kivyovyote kwani tume yako, dola yako na hata ukitoa rushwa unafumbiwa macho. Sasa hiv Lowasa yuko upinzani hata kusalimia watu anawekwa ndani. Hizo ndio siasa za kipuuzi za bara la Africa.
Bandiko langu limeonyesha hata wakati Lowassa akiwa CCM, aliwahi kugaragazwa kwenye chaguzi. Kama CCM inaiba kura kwa nini hakuiba hizo kura?

Kama wapinzani wanafahamu CCM wanaiba kura kwa nini hawapeleki malalamiko mahakamani na kama mahakama hawaziamini, kwa nini wanaingia kwenye chaguzi ambazo wanafahamu wataibiwa kura?
 
Back
Top Bottom