Edward Lowassa: Ni kweli nitagombea Urais 2020

Edward Lowassa: Ni kweli nitagombea Urais 2020

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
IMG-20170716-WA0005.jpg
Waziri mkuu mstaafu na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Mh. Edward Lowassa akifanyiwa mahojiano na kituo cha televisheni cha Nation TV cha jijini Nairobi nchini Kenya.

" Watu wengi wananiuliza kuhusu 2020, Jibu ni Moja Tu. NITAGOMBEA"
Edward Lowassa
Nairobi Serena
16 July 2017

Huyu anazo sifa za kuitwa rais wa nchi maana anazo hekima na busara katika maneno yake, hivyo ni rahisi kwake kuunganisha jamii yote ya Watanzania na kuwa kitu kimoja, siyo huyu ambaye anaamini wakosoaji wake ni maadui wa taifa hili
Ana hekima na busara sana. Sikuwahi hapo nyuma kufikiri kuwa siku moja angekuwa kinara wa siasa za chadema.

Anajua kuztumia turufu zake.
 
Kiukweli Lowassa anaweza kufanya interview za kimataifa vyema, anajiamini na anajua nini cha kujibu, yote kwa yote ile Lugha ya Malkia inakwenda vizuri.

Kama angekuwa yule "Uchwara" wa Tz ndio anahojiwa ungesikia kakimbia interview au akaishia kuporomosha matusi ya nguoni ya kiswahili na kisukuma.
Ila jamani Mungu fundi.... anajua wapi aweke tofali wapi aweke bawaba..... Sizonje angeijua lugha ya malkia vizuri haki tusingelala hapa mjini.... baba mpenda sifa kuliko malaika wa sifa ibilisi
......

Na Ule moyo ungekua unatulia angekata mawimbi kuliko Vasco da Gama.... ama kweli Mungu fundi.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Huyu aliyesema to develop you have to improve poverty, au lowasa mwingine?!
Acha kabisa kumfananisha Lowassa na yule 'uchwara' ambaye anapata hasira na Presha ukimuuliza swali kwa lugha ya malkia.
'Uchwara' kila kukicha anakariri tu salamu za kimakabila na matusi ya kisukuma tu ili kwenda kuropoka kwa watz wajinga.
 
Njooni nyie mtakaosema CHADEMA walifanya kosa kumpokea ama ni kwa nini walimwita fisadi sasa wako naye!
 
Kiukweli Lowassa anaweza kufanya interview za kimataifa vyema, anajiamini na anajua nini cha kujibu, yote kwa yote ile Lugha ya Malkia inakwenda vizuri.

Kama angekuwa yule "Uchwara" wa Tz ndio anahojiwa ungesikia kakimbia interview au akaishia kuporomosha matusi ya nguoni ya kiswahili na kisukuma.

🙁🙁 aaah, aiseee..... hii nayo ni comment eti !!

Basi sawa bwana....
 
Ila jamani Mungu fundi.... anajua wapi aweke tofali wapi aweke bawaba..... Sizonje angeijua lugha ya malkia vizuri haki tusingelala hapa mjini.... baba mpenda sifa kuliko malaika wa sifa ibilisi
......

Na Ule moyo ungekua unatulia angekata mawimbi kuliko Vasco da Gama.... ama kweli Mungu fundi.

Post sent using JamiiForums mobile app
Ha ha ha, umewaza vema! Na nina hakika angesema mwanafunzi akifika form two bado hawezi kuongea lugha anayosomea atumbuliwe hatufai huyo. Pia ufanywe Uhakiki kujua walio maliza kidato cha sita na wako makazini na lugha hiyo hawaijui ili waondolewe au kushtakiwa kwa kufoji.
Lakini kingine nilichogundua ni huu unafiki wa wanaccm, wanamsifia usoni ila moyoni wanachuki naye mbaya sana. Ndio chanzo cha yeye kujisahau. Majuzi nimemsikia kiongozi wa ngazi ya kati ambaye ukimsikia jukwaani au akihojiwa anamwaga sifa utadhani anasifiwa Muumba, akiponda huku faragha na kusema wazi "namchukia sana huyu hatufai ni mbishi"
 
kama Kenya wanampenda agombee hukohuko na linchi lao la kifisadifisadi, naona Uhuru anatuchokonoa kilichompata joice banda naona anakitafuta
 
Siku zote ukiona mtu anaongea amekunja ndita na kurusha mikono fahamu ana matatizo na hajui kuzungumza kimkakati.

Angalia picha ya Wa awamu 1,2,3,4 wanazungumza huku wametulia. Walikuwa hawana cha maneno "Nimesema, Mimi ndio mkubwa, nitafanya n k" Walikuwa na "Tutafanya, Serikali yetu n.k".
 
Back
Top Bottom