Edward Lowassa na Fredrick Sumaye Washiriki Uwanzishwaji wa Dayosisi ya Mwanga KKKT

Mawaziri wa kuu wastaafu na wajumbe wa kamati kuu Y CHADEMA ndugu EDWARD LOWASA na FREDRICK SUMAYE siku ya leo tar 06/1112016 walipata wasaa mzuri wa kushirika katika uzinduzi wa dayosisi mpiya ya KKKT jimbo la Mwanga.

Katika uzinduzi huo ambao raisi wa Jamuhuri ya muungano ndio slikua mgeni rasim lakin alituma mwakilishi ambaye ni mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Bwana Meck Sadick,viongozi hawa walipokelewa kwa bashasha na nderemo huku wakiwapongeza wakazi wa Mwanga kwa kupata dayosisi ambayo waliitafta kwa miaka mingi.
Waziri mkuu mstaafu na waziri mkuu aliyejihuzuru kwa kashfa ya wizi.
 
Huyu mze amepiga ziara wilaya zote za mkoa wa kilimanjaro, moshi, same, siha, Hai, rombo, na mwanga kukagua, na kuzindua miradi ya maendeleo bila kujali kwamba ni CHADEMA, nccr, au ccm aloshinda katika eneo husika, huwez Amina amepiga route mpaka same - upareni huko juu milimani ambapo CHADEMA imeshinda kiti cha ubunge kwenda kuangalia maendeleo mpaka akapata ajali ndo yule mwandishi wa tbc akafariki, anachofanya huyu mzee ndo siasa za kweli na zenye kujenga, hanaga siasa za kitoto toto kama za Gambo na makonda, mkulu mwenyewe anatakiwa achukue busara toka kwa meck sadick.

Huwezi Amini kabisa, kuna kila dalili kuwa Mzee Meck Sadick ambaye ndiye mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro atatumbuliwa.

Na sababu ziko wazi kabisa, "Mtukufu" hamtaki huyu mzee, na hapendi kabisa hiyo style yake ya kuishi vizuri na Upinzani.

Hiyo nafasi yake anaandaliwa kupewa Kapwe Warioba ambaye kwa sasa ni mkuu wa wilaya ya Moshi Mjini.

Kama ilivyokuwa kwa Makonda hapo Dar, kwa Gambo pale Arusha, Kapwe Worioba naye yupo mbioni kupewa mkoa wa Kilimanjaro. Akijiongeza tu, hata leo hii, basi ukuu wa mkoa unaupata!

Jipe Muda tu.
Huu mchezo haitaki Haraka.
 
Ilipatikana kwa vurugu na vita lowasa na sumaye kuwapongeza kwa kupigania kivita kuipata si sawa dayosisi kikawaida viongozi wa dini ndio huangalia na kugawa au kuanzisha mpya.lowasa na sumaye kuwapongeza watu wa mwanga kwa njia hiyo ya kivita waliyotumia si sahihi ni kuhamasisha vurugu Ndani ya KKKT ni kama kuhamasisha wengine kuwa mkitaka dayosisi yenu tumieni vurugu na vita kama wenzenu wa mwanga.
Mkuu hebu ongea kitu ulicho na uhakika nacho na sio kuongea tuu kwa kuwa uko nyuma ya keyboard yako unaongea mambo ambayo huna uhakika nayo
 
Hiyo dayosisi ilipatikana kwa vita sio kwa amani ni zao LA damu lowasa na sumaye kushabikiwa sidhani kama ni jambo zuri sana inaonyesha walihusika kwa namna moja au nyingine kujitenga kwao kivita
Hakuna damu iliyomwagika Mwanga acha uongo wewe nani aliuawa mimi ni mzaliwa wa Mwanga udanganya wasio na dini wenzako
 
You are very right naamin hata hao maaskofu wamekuja tu ila kifupi ni moja ya dayosisi zikizopatikana kwa vurugu na hata kuharibu mali za kanisa. Askofu sendoro aliokoa jahazi akasema na wapewe na kulikuwa na uhusiano na viongoz flan wa kiserikali/kisiasa.kifupi kujitenga kwao hakukuwa kwa amani. Pole dayosisi ya pare na hongera kuzaa dayosisi ya mwanga
Umeamua kupotosha historia na imani za watu kwa makusudi kabisa hapa.

UFAFANUZI.
1/Harakati za kuwepo kwa Dayosisi ya Mwanga zilianza zaidi ya miaka 20 iliyopita, na sababu ya msingi kabisa zilikuwa ni.
-Dayosisi mama ya Pare kushindwa kuendesha eneo lote la Pare(Same na Mwanga). Na athari kubwa kuonekana kwa upande wa Mwanga kwa sababu ya Geografia yake.

-Kuzorota kwa Huduma ya Injili katika eneo la Mwanga(Huko ndiko Ukristo wa Madhehebu Kilutheri kwa Wapare ulipoanzia kiasili)

-Kufa na kufifia kwa miradi mingi ya Afya na Elimu iliyokuwa ikiandeshwa na kanisa la Lutherani Dayosisi ya Pare, miradi hii mingi ilikuwa upande wa Mwanga.(Miradi hii yote ilikuwa ina hudumia watu wa dini zote)

-Mbegu ya Ubaguzi na Chuki iliyopandikizwa kwa Makusudi na Viongozi wachache wa juu wa kanisa la lutherani dayosisi ya Pare dhidi ya Waumini wenzao waliokuwa wanatokea upande wa Mwanga(Kifupi Ubagani uliingizwa Kanisani kwa makusudi ili viongozi wale wavune mali ya kanisa kirahisi sana kwa njia ya kuwagawa maumini kwa kutumia maeneo wanayotoka kiasili).

2/Mchakato wa Kupata dayosisi ya Mwanga ulichukua muda mrefu sana(Zaidi ya Miaka 20) japokuwa vigezo na masharti ya kupewa dayosisi hiyo ulikuwa umefikiwa, lakini Kanisa la Lutherani Tanzania halikuwa tayari kuruhusu hilo kwa sababu kuu Tatu tu(Woga wa kuonekana umeruhusu hilo kwa kushinikizwa, Wasiwasi wa Dayosisi mama ya Pare Kufa kwa sababu waumini wengi wake wanatoa upande wa Mwanga, Maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi wa juu wa Kanisa la Lutherani Tanzania).

3/Fujo zote zilizowahi kutokea zilizotokana na mambo haya..
-Mvutano wa makundi makuu mawili ya waumini waliokuwa wanavutana(Mwanga Vs Pare, mizozo hiyo ilikuwa inatokea Eneo la Mwanga tu, mahali ambapo wakazi wake wa kiasili ni Kutoka Mwanga tu. Hivyo wakazi wa Mwanga mwenyewe kwa wenyewe walikuwa wamegawanyika, mzozo huo haukuwa baina ya watu wa Mwanga na Same)

-Kitendo cha viongozi wa juu wa Dayosisi ya Pare kupiga marufuku Waumini au wachungaji wowote wenye mwelekeo wa kudai uwepo wa Dayosisi ya Mwanga kuingia kanisani. Kifupi walizuiwa hata kuzikwa kwenye maeneo ya Kanisa. Jeshi la Polisi lilitumika sana kuwapiga, kuwafunga wazee, waumini au wachungaji wenye msimamo wa kudai Dayosisi ya Mwanga.
 
......Kila kitu kipo kwenye maandishi.
Wazee wengi wa maeneo ya Kaskazini wanapenda sana kuweka kumbukumbu za matukio kwa kuandika kwenye maandishi ya vitabu kila kitu kinachohusu historia za matukio ya maisha yao na kuyatunza kwa umakini wa hali ya juu sana.

Historia kuhusu Dayosisi ya Mwanga ipo kwenye maandishi hata sasa. Jaribu kudadisi na utagundua mengi.

Kwa wapare kuna mambo mengi sana, hasa wale wazee wa Kisangi, Jakaya Kikwete anawajua sana wale wazee na mila zao, Hata Magufuli anawajua vizuri sana, maana kabla hajachukua fomu au kutangaza kutaka kugombea urais ndani ya CCM, kwanza alienda kule kuongea na wale wazee....
Mpaka leo sijajua ni kwanini?

Sijui mpaka leo kama kuna watu wanajua siri ya kwanini Serikali ilitumia kila njia kuhakikisha Edward Lowassa haendi kule Usangi kumzika mzee Peter Kisumo mwaka jana alipofariki?...
Kuna sababu nzito.

NOTE:
Mengi nimeyajua kuhusu hao watu kupitia maandishi yao, binafsi nimeyajua kupitia mzee mmoja wa Kipare, Msomi mzuri na Muislamu mzuri sana. Ni mfuatiliaji mzuri sana, kila tukio alikuwa analichumbua kwa kina
 
Back
Top Bottom