TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Aliyekuwa mgombea urais kupitia CHADEMA, Edward Ngoyayi LOWASSA akiwa Mjini Tabora wakati wa Kampeni za kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alinukuliwa akiwaasa waumini wa dhehebu la KKKT kumchagua yeye kwa kuwa ni Mlutheri na kwamba kwa awamu zote rais alipotokana na dini ya kikristo alitoka dhehebu la Kikatholiki.
Ni kauli hiyo ya Lowassa iliyopelekea hata baada ya uchaguzi , kukatokea matamko mbalimbali yalioashiria kutoikubali serikali ya awamu ya tano kutoka kwa viongozi wa dhehebu hilo. Hii siyo hali nzuri kwa msatakabali wa umoja na mshikamano wa Taifa letu.
Januari 31, 2016 katika kanisa kuu la KKKT, mjini Moshi, wakati askofu mkuu wa Kanisa la KKKT, Fredrick Shoo anasimikwa kuwa askofu mkuu wa kanisa hilo alinukuliwa kushutumu kitendo cha Polisi kuingia Bungeni kutuliza ghasia zilizosababishwa na Wabunge wa Upinzani. Shutuma hizi za Askofu Shoo kwa serikali alizitoa mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kasim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi kwenye ibada hiyo maalum. Wengine waliohudhuria ibada hiyo walikuwa ni Edward Lowassa na Fredrick Sumaye wote wakiwa ni waumini wa dhehebu la KKKT.
Jana wakati wa Ibada ya kushukuru uchaguzi kumalizika salama iliyofanyika katika Usharika wa Nshara katika Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT, Mbowe ameibuka na kuishambulia serikali ya JPM kwa sera yake ya kutumbua majibu kwa madai kuwa watumishi wa Umma wanafukuzwa bila kupewa nafasi ya kujitetea. Ameyasema hayo mbele ya Askofu Mkuu wa KKKT, Fredrick Shoo, Maaskofu wakuu wastaafu, Erasto Kweka na Martin Shao. Mbowe anataka kuuambia Umma wa Tanzania kwamba, rais ni kichaa mpaka achukue uamuzi wa kumfukuza mtumishi wa Umma bila ya kuwa na kosa?*
Kuna haja ya CHADEMA mjitafakari vyema na kauli zenu ndani ya nyumba za ibada kuhusiana na utendaji wa serikali ya awamu ya tano. Kwa mwendo huu, itakuwa ni vigumu sana kuwafikirisha watanzania vingine tofauti na chuki zinazotokana Mlutheri kukosa urais katika uchaguzi mkuu uliomalizika oktoba mwka 2015.
Ni vyema kama cha chama cha siasa na chenye haki ya kuhakikisha kila mtanzania anatendewa haki, mkafanya utafiti na kujiridhisha na majina ya watumishi wa Umma walioonewa katika operesheni tumbua majipu na mkafuata taratibu na sheria ya Utumishi wa Umma mkawatetea badala ya kukimbilia katika nyumba za ibada kuponya majeraha yaliyotokana kukosa kuingia Ikulu. Mnaikosanisha Serikali na viongozi wa dini pasipo na sababu.
*Kwa upande mwingine mtambue kuwa wachache hao mnaowaona wanaonewa wamesababisha wengi kuumia kutokana na uhujumu wao wa rasilimali za nchi. Msitegemee Watanzania walio wengi kuwaelewa katika hili.