Mhe. Edward Lowassa Na Familia yake washiriki ibada ya Mwaka Mpya KKKT Monduli

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Taifa Mhe.Edward Lowassa ameshiriki Ibaada Ya Mwaka Mpya Pamoja na Familia yake katika kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha.

Katika Ibaada hiyo Aliongozana na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe.Kalist Lazaro,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mhe.Isack Joseph,Wakili Msomi John Mallya pamoja na Viongozi wengine.

Pia Mhe.Lowassa aliwatakia Heri ya Mwaka Mpya Watanzania wote na kuwaambia wafanye kazi kwa bidii.
IMG-20170101-WA0055.jpg
IMG-20170101-WA0054.jpg
IMG-20170101-WA0053.jpg
 
Mnaposemav
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Taifa Mhe.Edward Lowassa ameshiriki Ibaada Ya Mwaka Mpya Pamoja na Familia yake katika kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha.

Katika Ibaada hiyo Aliongozana na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe.Kalist Lazaro,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mhe.Isack Joseph,Wakili Msomi John Mallya pamoja na Viongozi wengine.

Pia Mhe.Lowassa aliwatakia Heri ya Mwaka Mpya Watanzania wote na kuwaambia wafanye kazi kwa bidii.
View attachment 452851 View attachment 452853 View attachment 452855
Wakili Msomi? Ina maana gani? Yeye kasoma sana kuliko mawakili wengi au ? Ningependa kufahamu.
 
Hongera Lowasa kwa kuhamasisha watanzania wafanye kazi kuendana na kauli mbiu ya rais hapa kazi tu.

Ama kweli we Lowasa si Nyumbu tena
 
Mungu azidi kukulinda na wabaya wako,

Kwa kuwa siku zote umekuwa na Upendo na watanzania, umekuwa ukijitoa kwa hali na mali kuhakikisha unatimiza majukumu yako kwa nchi yako na watu wake, hakika Mungu huyu muumba Mbingu na dunia na vyote vilivyomo azidi kukusimamia na kukuongoza kwa kila jambo,

Siku zote Upendo wa kweli hauchoshi,
Moyo wako umejaa Upendo usio na husuda,
Moyo wako umejaa Upendo ambao hauwazii mambo yako mwenyewe,
Moyo wako umejaa Upendo ambao hauna hasira ya haraka,
Moyo wako una Upendo usio hesabu makosa,
Moyo wako una Upendo wenye nguvu kwa mambo yote yaliyofichika,
Moyo wako umejaa Upendo wa kuaminiana katika kila jambo,
Moyo wako umejaa Upendo unao amini yote
Umetuonesha Upendo ambao hauna mwisho, Mh Ngoyai wewe una Upendo wa kweli na watanzania na Tanzania,
 
Back
Top Bottom