Education Financial Support Needed

Ramthods

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
515
186
Ndugu wana JF,

Nchi yetu Tanzania ni moja ya nchi masikini sana hapa duniani kwenye nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu. Mamia kama sio maalfu ya vijana walio katika umri wa kwenda shule wanashindwa kuendelea na masomo au kuanza shule kutokana na uwezo duni wa kifedha ukilinganisha na gharama za elimu zinazohitajika.

Binafsi nina vijana wawili ambao nawalea kama mentor. Wote hawa nilikutana nao nyakati tofauti tofauti. Kutokana na uwezo wao kifedha na hali yao halisi kimaisha niliona ni vyema kuangalia uwezekano wa kuwasaidia kielimu ikiwa ni pamoja na ada, ushauri na vitu vingine muhimu.

Hawa vijana hawana baba, wote wanaishi na mama zao ambao kiuchumi uwezo wao ni duni sana. Mimi nawasaidia ada nusu, na mama zao wanamalizia nusu nyingine.

Lengo la kuandika hii post ni kwamba, hivi karibuni nimekutana na kijana mwingine tena. Huyu kijana ana kiu sana ya elimu na sijui nitamsaidiaje. Tofauti ni kwamba, huyu sio yatima - ana wazazi wote wawili isipokuwa hawa wazazi wake hawana habari na elimu. Kwenye familia yao wote wameishia lasaba, ila yeye ameamua kujisomesha mwenyewe - na hapo ndipo mambo yalipoanza kumwia vigumu.

Tatizo jingine ni kwamba huyu kijana hayupo kwenye formal education. Lengo lake yeye ni asome miaka miwili (Form I - IV) alafu afanye mtihani wa NECTA. Hivyo yeye anajisomea kupitia tuition ambazo wanafunzi wenzake hutumia kwa masomo ya ziada.

Ni vyema kila mwanafunzi kuwa katika formal sector - yaani katika shule fulani na sio kujisomea na kutegemea kufanya mtihani mwisho wa siku. Lakini pia, kuingia shule kwa miaka minne nako kunahitaji fedha.

Binafsi, siwezi kuongeza tena mzigo mwingine. Hawa wawili nilionao tayari naona ndio mwisho wa uwezo wangu.

Ningependa kufahamu kama kuna jinsi yoyote ile watoto kama hawa wanaweza kupatiwa msaada kifedha wakaendelea na masomo. Kama unafahamu sehemu/organization yoyote ile ambayo tunaweza kuwaelekeza watoto kama hawa waende kwa msaada zaidi, mchango wako utakuwa wa dhati mno.

Huyu mtoto yupo hapa Dar, ila wazazi wake wapo Tanga. Anaishi na mtu baki tu ambaye anamsaidia gharama nyingine kimaisha na ameshindwa kumsaidia kwenda shule.

Natumaini sote tupo pamoja.

Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom