Edibily Jonas Lunyamila,"Lunya"

Dah,huyu jamaa alitutesa sana simba,enzi hizo mtangazaji akisema"na nambari 11 ni kama kawaida edibily lunyamila!" mapigo ya moyo yalikuwa yana change ghafla kwa kusikia tu jina,akishika mpira ndo salaleee! Jamani Lunya Lunya!
Hata mie simba.... Lunya hakika alikua kiboko, natumaini anaendesha vema maisha yake nje ya soka.
 
Alisoma shy bush kama sikosei.nakumbuka matokeo yake yalipotoka wapenzi wa simba walifurahia sana maana alitaga yai

Siyo Shy Bush Mkuu, ni Buluba Sekondari iko mjini Shinyanga karibu kabisa na Shinyanga Government Hospital. Shule hiyo inamilikiwa na Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shy (SHIRECU). 'Buluba' ni jina la kikwetu maana yake 'Pamba'.
 
na wewe umekosea,sio buluba ni BUHANGIJA
 
Haya yalikuwa ni matangazo ya moja kwa moja kutoka Uwanja wa taifa mjini Dar es salaam kupitia redio Tanzania Dar es Salaam,"Mpira unatoka katika lango la timu ya Dar Yanga Afrikans kuelekea katika lango la timu ya Simba "Taifa Kubwa", Golikipa wa Yanga Steven Nemes anaupiga mpira vizuri kabisa hukuuuuu anauchukua Said Mwamba Kizotaa Kizotaa anampasia Method Mogella Mogella pembeni kabisaaaa anampelekeaaa kwakeeee Salum Kabunda Kabundaa Kabunda kwakeee Constatine Kimanda Kimandaaa anapeleka mpira kwa Ken Mkapa Ken Mkapa Mkapa Mkapa anatoa pasi ndeeeefuuuuu kwake Lunyamila Lunyaamiilaaaaaa Lunyamilaaaa chenga ya kwanza chenga ya piliii Lunyamila bado Lunyamilaaaa Lunyamilaaaa hatari katika lango ya timu ya Simba lalalalalalalal gooo lalaa goooo alalalalal Gooooooooooooooooooooooooo!!!
Ha ha ha! Mkuu.
Goooooooooooooooooooooo!!!!
Simba anatandikwa goli la pili hapa.
 
Siyo Shy Bush Mkuu, ni Buluba Sekondari iko mjini Shinyanga karibu kabisa na Shinyanga Government Hospital. Shule hiyo inamilikiwa na Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shy (SHIRECU). 'Buluba' ni jina la kikwetu maana yake 'Pamba'.
Aliesoma BULUBA ni Nteze John
 
hajasoma tambaza bhana

Alisoma shy bush kama sikosei.nakumbuka matokeo yake yalipotoka wapenzi wa simba walifurahia sana maana alitaga yai

Siyo Shy Bush Mkuu, ni Buluba Sekondari iko mjini Shinyanga karibu kabisa na Shinyanga Government Hospital. Shule hiyo inamilikiwa na Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shy (SHIRECU). 'Buluba' ni jina la kikwetu maana yake 'Pamba'.
amesoma Buhangija wakati wa headmaster Kija na alihitimu 1992!ukiyataka hata matokeo yake naweza kuku pm!
 
Mpira wa bongo njaa ndo inatumaliza huyu jamaa ni wa enzi za kina giggs wenzake hadi leo wanasumbua yeye tushamsahau
 
Labda 1998 PCB enzi la ouroch na mtera.hakuana bana huyu jamaa alitaga shinyanga huko

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Huyu jamaa alikuwa na talent ya ukweli,nakumbuka alivyowatesa Wazambia katika mashindano ya Challenge Cup pale Mwanza mwaka 1992 akiwa ndo kwanza anamaliza form 4.
 
Ilifikia sehemu kama nasikiliza boli enzi za kina Dominic Chilambo (RIP), Mzee wa maguu kumi na mbili (huyu simkumbuki jina vizuri) na wengineo, Lunya akishika mpira tu mi nazima radio mpaka kama dakika moja au mbili ndio nawasha tena kusikilizia vipi kimetinga?

Jamaa alikuwa ananipa presha sana.
 
papa mopao hapo mtangazaji (afu awe swedi mwinyi) anaposema "sasa anao lunyamilaaa! Kweli nilikuwa nataka kuzimia! Huyu mtu itachukua muda nchi ku produce kipaji cha aina hii!

Lunyamila alikuwa mzuri lakini by that time nilikuwa nimesha-loose interest na mpira wa bongo.

Mie nilikuwa natetemeka zaidi Sanifu Lazaro "Tingisha" akikamata mpira.

Hata Tom Kipese "Uncle Tom" alikuwa ananiweka roho juu, though alikuwa anaogopa sana ngwara.

Siku moja nikaja kukutana nae baada ya kustaafu, nilimwangia kuanzia juu hadi chini nikatikisa kichwa.

Akaniuliza kwani vipi? Nikamwambia basi acha tuu, bora tumekutana umeshastaafu ningekupiga mtama hapa hapa.

Yaani enzi hizo walikuwa wakichukuwa mpira nilikuwa natama kiredio kikate mawimbi, lakini ndo kwanzaaa redio ilisikika kwa ufasaha.
 
Back
Top Bottom