Edibily Jonas Lunyamila,"Lunya"

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
17,381
25,235
Dah,huyu jamaa alitutesa sana simba,enzi hizo mtangazaji akisema"na nambari 11 ni kama kawaida edibily lunyamila!" mapigo ya moyo yalikuwa yana change ghafla kwa kusikia tu jina,akishika mpira ndo salaleee! Jamani Lunya Lunya!
 
MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
17,381
25,235
ila akiwepo Kasongo Athumani kidogo najipa matumaini,Kasongo alikuwa anamkata viatu na kumchezea kibabe Lunya ile ilikuwa inasaidia sana
 
MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
17,381
25,235
kuna mechi kati ya Yanga na Ndovu ya Arusha,Lunya alipiga chenga mabeki hadi kipa! Ikabidi kipa ang'ang'anie miguu mbaya mbaya tu! Lunya Lunya bana!
 
VUVUZELA

JF-Expert Member
Jun 19, 2010
3,103
782
Ndo taabu ya kucheza mpira Bongo. Lunyamila sasa hivi ni driver taxi.

Lunyamila alikuwa na kipaji cha aina yake. Jamaa namfagilia. Inasikitisha mno hakupata chance ya kwenda kucheza soka ughaibuni kunakoeleweka sio umangani. Nakumbuka aliwahi kupata chance ya kufanya trials na FC Koln kule Bundesliga sasa sijui ilikuwaje
 
Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
3,894
1,667
Lunyamila alikuwa na kipaji cha aina yake. Jamaa namfagilia. Inasikitisha mno hakupata chance ya kwenda kucheza soka ughaibuni kunakoeleweka sio umangani. Nakumbuka aliwahi kupata chance ya kufanya trials na FC Koln kule Bundesliga sasa sijui ilikuwaje

Hakufit kwenye vigezo vinavyotakiwa kwa mchezaji wa hiyo timu.
 
Mwanagandila

Senior Member
Oct 9, 2011
182
100
Lunyamila yupo anaishi kwake mbezi, amemaliza kozi ya ukocha na kwa sasa ni kocha kamili kwani ameshapata cheti.
kuhusu kwamba ni driver tax hiyo sio kweli, nachofahamu ana biashara zake tu na hata leo nilikuwa nae uwanjani
 
Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,709
3,215
Lunyamila alikuwa na kipaji cha aina yake. Jamaa namfagilia. Inasikitisha mno hakupata chance ya kwenda kucheza soka ughaibuni kunakoeleweka sio umangani. Nakumbuka aliwahi kupata chance ya kufanya trials na FC Koln kule Bundesliga sasa sijui ilikuwaje

Alirudi kabla hata ya kupimwa afya, kina gulamali walikomaa arudi kucheza vs simba fainali ya kombe la hedex kama sikosei.
 
only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,524
Ndo taabu ya kucheza mpira Bongo. Lunyamila sasa hivi ni driver taxi.

Mkuu dont tell me so!! Plz may u change this statement? Real? jamaa ni dereva tax za wapi? lol!! kweli soka la Bongo halina adabu...
 
trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
722
Statement nyingine sio za kuamini humu ndani! Hivyo msomaji yeyote akiwa katika kijiwe akipeleka info kama hizi inaweza ikaleta matokeo hasi! Ila jamaa alienda German kweli? Sio UK?
 
Somi

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
2,187
2,345
Statement nyingine sio za kuamini humu ndani! Hivyo msomaji yeyote akiwa katika kijiwe akipeleka info kama hizi inaweza ikaleta matokeo hasi! Ila jamaa alienda German kweli? Sio UK?

alienda kufanya majaribio fc cologne ya ujerumani kama sijakosea ni mtangazaji wa sauti ya ujerumani sekioni kitojo alimuunganishia hiyo nafasi alifuzu kila kitu kasoro stamina aliambiwa akaongeze sijui akadharau au ilikuwa vipi sijui

kuna goli zuri sana alifunga aliwalamba chenga mabeki wote wa ghana kabla ya kufunga pale uwanja wa kasarani nairobi ikawa tanzania 3 ghana 2
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom