TEAM 666
JF-Expert Member
- Dec 7, 2017
- 4,330
- 8,421
EDIBILY JONAS LUNYAMILA . Macho yangu yameshuhudia mengi na Moyo wangu umebahatika kujawa na hisia tosha kwa Uzalendo wa Taifa langu la Tanzania.
Miaka mingi tumekua tukiimba nyimbo za kuitukuza Nchi yetu na mashujaa na hata kuwasoma katika historia . " Tazama Ramani utaona Nchi nzuri, yenye mito na mabonde mengi ... " au hata ubeti mwingine maarufu " ... jina lako ni tamu sana, nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni Heri Mama weee . "Hii yote ni kuipenda Nchi yetu lakini tuna mengi hatuyaimbi na kuyatukuza.
Edibily Jonas Lunyamila, miguu ya Dhahabu, kichwa chenye mamlaka ya kusoma alama zote ndani ya Uwanja, kipaji maridhawa kabisa katika ukanda huu.
Ukienda Uganda hadi leo jina La Lunyamila ni Maarufu kuliko Emanuel Okwi ni kutokana na uwezo wa maajabu wa Winga huyu .
Mwaka 1992 katika mashindano ya UMISETA kule Zanzibar kiliibuka kipaji cha Dhahabu kutoka shule ya Sekondari ya Buhangija huko Shinyanga na mwaka huo akaitwa Timu ya Taifa, bahati iliyoje.
Inasemekana Abbas Gulamali ndiye aliyekwenda kumsubiri Edibily Jonas Lunyamila mlangoni mwa chumba cha mtihani ili ampeleke Mwanza kucheza timu ya Taifa.
Nafikiri hii ndiyo sababu akacheza Yanga na mwaka 1993 akaacha alama ya Maisha yake Kule Kampala Uganda. Kwangu Mimi maisha ya soka ya Lunyamila na kipaji chake kinastahili kuimbwa kama kivutio cha Taifa na ni Hadhi ya Nyota Tano.
Nikiwakumbuka watangazaji wa zamani kina Swedi Mwinyi, Juma Nkamia, Ahmed Jongo au Charles Martin Hillary walivyokua wakitangaza soka basi mie jina linalokuja ni Lunyamila.
Unamkumbuka Edibily Jonas Lunyamila kwa lipi au nyakati gani..?